Ubishi Wageuka Ushindi: Brown Anthony Avuka Mbeya–Dar kwa Pikipiki Ndani ya Saa 10

Bawabu wa pili

Senior Member
Joined
Nov 14, 2025
Posts
147
Reaction score
433
Kijana dereva wa bodaboda anayefahamika kwa jina la Brown Anthony ameibua gumzo kubwa miongoni mwa wananchi baada ya kufanikiwa kusafiri kutoka jijini Mbeya hadi Dar es Salaam kwa kutumia pikipiki aina ya Boxer 150 HD yenye namba ya usajili MC 473 FKT, ndani ya saa 10, safari iliyoanzia kwenye ubishani wa kawaida na kuhitimishwa kwa ushindi wa kihistoria.

Ubishani huo ulianza tarehe 14 Januari 2026 kati ya Brown Anthony na bodaboda mwenzake Alex Ndile, ambapo walitofautiana kuhusu uwezekano wa kufika Dar es Salaam kwa pikipiki ndani ya muda wa masaa 13. Baada ya majadiliano makali, walikubaliana kuyaweka madai yao katika makubaliano rasmi ya kisheria.

Makubaliano hayo yaliwekwa mbele ya mwanasheria Ambakisye Kibona, ambapo kila mmoja alikuwa na pikipiki yake binafsi, na pande zote zilikubaliana kuwa atakayeshindwa atalazimika kumpa mshindi pikipiki yake kama dau la makubaliano hayo.

Baada ya makubaliano kukamilika, Brown Anthony alianza safari yake rasmi tarehe 15 Januari saa 11:00 asubuhi, akitokea Mbalizi jijini Mbeya, akitumia pikipiki yake kama ilivyokubaliwa katika makubaliano hayo ya kisheria.

Katika safari hiyo ndefu na yenye changamoto, Brown Anthony alifanya mapumziko mara tatu kwa ajili ya ukaguzi na matengenezo madogo ya pikipiki, hatua iliyomwezesha kuendelea na safari bila matatizo ya kiufundi.

Hatimaye, alifanikiwa kuwasili jijini Dar es Salaam saa 9:35 alasiri siku hiyo hiyo, akitumia muda uliokuwa chini ya masharti ya makubaliano, na hivyo kuthibitisha ushindi wake dhidi ya mpinzani wake Alex Ndile.

Baada ya kukamilisha safari hiyo, Brown Anthony alianza safari ya kurejea Mbeya alfajiri ya saa 11 kutoka Dar es Salaam, na kufanikiwa kuingia Mbalizi jijini Mbeya jioni ya Ijumaa, Januari 16, 2026, ambapo alipokelewa kwa shangwe. Kufuatia ushindi huo, alikabidhiwa pikipiki ya ushindi, iliyokuwa mali ya Alex Ndile yenye namba ya usajili MC 695 EFE.

Pikipiki.jpg
 
Sema Mjinga aliichapa haswaa,
Maana katumia Saa 10 Kwamba 900km/10hr unapata 90km/hr.

Hiyo Speed kwa Boxer si ndogo
Na ukumbuke ndani ha hizo 10hr maelezo hapo alifanya vituo kwa Kufanya cheking na kujaza mafuta.
Bado tuta (lazima upunguze speed)
Ina maana alikuwa akipata mnyoosho anapiga 130km/hr+ ili kufidia muda alopoteza.

Sasa Boxer ukiwa kwenye 130km/hr+ sio poaa(kifo nje nje)

Usije shangaa Jamaa akapata shavu kwa Boxer kimasiara maana ni kama Tangazo kwao kuonyesha uimara wa hizo pikipiki.
 
Kijana dereva wa bodaboda anayefahamika kwa jina la Brown Anthony ameibua gumzo kubwa miongoni mwa wananchi baada ya kufanikiwa kusafiri kutoka jijini Mbeya hadi Dar es Salaam kwa kutumia pikipiki aina ya Boxer 150 HD yenye namba ya usajili MC 473 FKT, ndani ya saa 10, safari iliyoanzia kwenye ubishani wa kawaida na kuhitimishwa kwa ushindi wa kihistoria.

Ubishani huo ulianza tarehe 14 Januari 2026 kati ya Brown Anthony na bodaboda mwenzake Alex Ndile, ambapo walitofautiana kuhusu uwezekano wa kufika Dar es Salaam kwa pikipiki ndani ya muda wa masaa 13. Baada ya majadiliano makali, walikubaliana kuyaweka madai yao katika makubaliano rasmi ya kisheria.

Makubaliano hayo yaliwekwa mbele ya mwanasheria Ambakisye Kibona, ambapo kila mmoja alikuwa na pikipiki yake binafsi, na pande zote zilikubaliana kuwa atakayeshindwa atalazimika kumpa mshindi pikipiki yake kama dau la makubaliano hayo.

Baada ya makubaliano kukamilika, Brown Anthony alianza safari yake rasmi tarehe 15 Januari saa 11:00 asubuhi, akitokea Mbalizi jijini Mbeya, akitumia pikipiki yake kama ilivyokubaliwa katika makubaliano hayo ya kisheria.

Katika safari hiyo ndefu na yenye changamoto, Brown Anthony alifanya mapumziko mara tatu kwa ajili ya ukaguzi na matengenezo madogo ya pikipiki, hatua iliyomwezesha kuendelea na safari bila matatizo ya kiufundi.

Hatimaye, alifanikiwa kuwasili jijini Dar es Salaam saa 9:35 alasiri siku hiyo hiyo, akitumia muda uliokuwa chini ya masharti ya makubaliano, na hivyo kuthibitisha ushindi wake dhidi ya mpinzani wake Alex Ndile.

Baada ya kukamilisha safari hiyo, Brown Anthony alianza safari ya kurejea Mbeya alfajiri ya saa 11 kutoka Dar es Salaam, na kufanikiwa kuingia Mbalizi jijini Mbeya jioni ya Ijumaa, Januari 16, 2026, ambapo alipokelewa kwa shangwe. Kufuatia ushindi huo, alikabidhiwa pikipiki ya ushindi, iliyokuwa mali ya Alex Ndile yenye namba ya usajili MC 695 EFE.
Kufuatia ushindi huo, alikabidhiwa pikipiki ya ushindi, iliyokuwa mali ya Alex Ndile yenye namba ya usajili MC 695 EFE.🥺😂😂😂
 
Sama Mjinga aliichapa aisee
Maana katumia Saa 10 Kwamba 900km/10hr unapata 90km/hr

Hiyo Speed kwa Boxer si ndogo
Na ukumbuke ndani ha hizo 10hr maelezo hapo alifanya vituo kwa Kufanya cheking na kujaza mafuta.
Bado tuta (lazima upunguze speed)
Ina maana alikuwa akipata mnyoosho anapiga 130km/hr+ ili kufidia muda wa alopoteza.

Sasa Boxer ukiwa kwenye 130km/hr+ sio poaa

Usije shangaa Jamaa akapata shavu kwa Boxer kimasiara maana ni kama Tangazo kwao kuonyesha uimara wa hizo pikipiki
Mim siwez endesha pikpik speed ya 80km/h kwa urefu hata wa km 4,nakuwa najihis kufa kufa
 
Sama Mjinga aliichapa aisee
Maana katumia Saa 10 Kwamba 900km/10hr unapata 90km/hr

Hiyo Speed kwa Boxer si ndogo
Na ukumbuke ndani ha hizo 10hr maelezo hapo alifanya vituo kwa Kufanya cheking na kujaza mafuta.
Bado tuta (lazima upunguze speed)
Ina maana alikuwa akipata mnyoosho anapiga 130km/hr+ ili kufidia muda wa alopoteza.

Sasa Boxer ukiwa kwenye 130km/hr+ sio poaa

Usije shangaa Jamaa akapata shavu kwa Boxer kimasiara maana ni kama Tangazo kwao kuonyesha uimara wa hizo pikipiki
Kabisa, wakiiweka vizuri hiyo anakula shavu kabisa na kubadilisha maisha kimasihara.

Boxer wajulishwe kuwa kuna mwamba ameiongezea thamani bidhaa yao
 
Kuna siku December fulani nilikuwa naenda Moshi. Kufika Maeneo ya Bagamoyo nikaipita pikipiki fulani imechoka. Nikaenda nikasimama Msata. Baadae natoka Msata ile pikipiki nikaikuta Wami nikaipita nikae da kufika Mkata tena tuasimama, kutoka hapo ile ile pikipiki nikaipita mbele ya Mkata nikawaambia jamaa huyu mtu anaenda Moshi. Mwenso wake nikimwangalia wa kawaida tu. Tukaenda tukasi.mama Korogwe hapa huwa tunakaa kama 1hr. Kutoka hapo ile pikipiki nikaipita maeneo ya Lembeni hapo tukajihakikishia mwamba anaenda kula Xmas na chonbo yake. Na anaendesha pembeni kabisaya barabara
 
Kwa sababu ya ugeni wake wa njia, labda iwe alishawahi fanya hivyo kabla, huyu mwamba kahatarisha maisha yake kwa watu wanoijua barabara ya Mbeya Dar haswa maeneo haya.

Kipande cha Mbeya <> Igawa - Hiki kipande barabara yake ni mbovu mno, ina mashimo, uwepo wa mlima nyoka na kwa pikipiki kutembea mwendokasi ni kujiweka hatarini ukichukulia huku alipita alfajiri kukiwa hakujapambazuka.

Uwepo wa mteremko mkali wa Kitonga - Kilometa takribani 9 za konakona fupi, mteremko mkali, ujenzi unaonendelea kutoka baada kidogo tu ya kibao Ikokoto hadi unapokaribia tuta la kibao cha Comfort.

Uwepo wa konakona za Iyovi - Kilometa 24 toka kona ya kwanza ya Iyovi pale mpakani mwa Iringa na Moro hadi karibia na Msimba kilometa chache toka Mikumi mjini, hizi ni kilometa za kibabe maana ukitaka safari iwe fupi mathalani ukiwa na gari inakupasa uwe jasiri na utembee wastani wa 100km/hr hadi 120km/hr. Sasa sijui huyu mwamba alikuwa speed kiasi gani wakati analala kushoti-kulia-kushoto tena....

Kipande cha mwisho ni Chalinze <> Mlandizi - Ubovu wa barabara, ukosefu wa alama za barabarani, ujenzi wa barabara maeneo ya Ruvu vyote ni vikwazo vinavyoshusha speed.

Hitimisho:
Pamoja na vikwazo vyote hivyo muda alioutumia inawezekana kufikiwa haswa kwa gari (nimeshaendesha muda huo mara kadhaa kama 3).Kutoka Mbeya kwenda Dar ni rahisi zaidi sababu kijiografia unakuwa unatoka uwanda wa juu kwenda wa chini (tunateremka).

Huyu mwamba kama katoboa na boda muda wa masaa 10, tukimwachia gari atafanya kitu mbaya zaidi.
 
Kwa sababu ya ugeni wake wa njia, labda iwe alishawahi fanya hivyo kabla, huyu mwamba kahatarisha maisha yake kwa watu wanoijua barabara ya Mbeya Dar haswa maeneo haya.

Kipande cha Mbeya <> Igawa - Hiki kipande barabara yake ni mbovu mno, ina mashimo, uwepo wa mlima nyoka na kwa pikipiki kutembea mwendokasi ni kujiweka hatarini ukichukulia huku alipita alfajiri kukiwa hakujapambazuka.

Uwepo wa mteremko mkali wa Kitonga - Kilometa takribani 9 za konakona fupi, mteremko mkali, ujenzi unaonendelea kutoka baada kidogo tu ya kibao Ikokoto hadi unapokaribia tuta la kibao cha Comfort.

Uwepo wa konakona za Iyovi - Kilometa 24 toka kona ya kwanza ya Iyovi pale mpakani mwa Iringa na Moro hadi karibia na Msimba kilometa chache toka Mikumi mjini, hizi ni kilometa za kibabe maana ukitaka safari iwe fupi mathalani ukiwa na gari inakupasa uwe jasiri na utembee wastani wa 100km/hr hadi 120km/hr. Sasa sijui huyu mwamba alikuwa speed kiasi gani wakati analala kushoti-kulia-kushoto tena....

Kipande cha mwisho ni Chalinze <> Mlandizi - Ubovu wa barabara, ukosefu wa alama za barabarani, ujenzi wa barabara maeneo ya Ruvu vyote ni vikwazo vinavyoshusha speed.

Hitimisho:
Pamoja na vikwazo vyote hivyo muda alioutumia inawezekana kufikiwa haswa kwa gari (nimeshaendesha muda huo mara kadhaa kama 3)

Huyu mwamba kama katoboa na boda muda wa masaa 10, tukimwachia gari atafanya kitu mbaya zaidi.
Gari vikwazo vingi. Bodaboda hasimamishwi na askari,hana 50kph zone matuta anapita na mwendo anaotaka. Ni rahiai kwake kupata average speed ya juu ingawa maximum speed yake hataifikia gari on some spots.
 
Back
Top Bottom