Kwa kifupi tusianze kutengeneza assumptions za ingekuwa hivi ama vile, hata India walidhani wataingiza hizo fighter jets Pakistan na kutoka kwa intel zao za kijeshi wakaona inawezekana, lakini kilichotokea ndio hivyo..
Ndio maana umejijibu nilipoweka bold kwamba kitendo cha India kuingia Pakistan walifahamu wangewamudu Pakistan, kilichotokea ndege zimepigwa....
Hakuna anayefahamu kama ndege zote tano zilikuwa zinakwenda kushambulia ardhini au la, kwa maana kwenye strike package kama hio ya ndege 5, unafahamu vipi hata mbili zilikuwa kwa ajili ya ulinzi wa ndege nyingine?
Mfano Mig-29 ni nzuri zaidi kwenye mapigano ya anga kwa anga..
Kuna hio ndege inasemekana ilikuwepo miongoni wa huo msafara ambayo ni SU-30MK1, hii ndege ndio yenye idadi kubwa katika jeshi la anga la India... na India wanatengeneza hii ndege kwa kushirikiana na Russia, sasa kama na yenyewe imeliwa kichwa basi tukubali tu Pakistan alikuwa amejipanga... kwa maana INdia wana utaalamu mkubwa wa hii ndege kuliko ndege nyingine yeyote..