Uchaguzi 2020 Ubunge Kigoma Mjini, Zitto Kabwe vs Diamond Platnumz

Uchaguzi 2020 Ubunge Kigoma Mjini, Zitto Kabwe vs Diamond Platnumz

Umewasilisha kwa staili ya mtu mbeya. Hapa unatakiwa kuleta habari siyo vioha. Una elimu gani?
 
Alipo Diamond ni juu zaidi ya wabunge kiuchumi na kiumashuhuri.....sasa anafuata nini kule bungeni ni siku hizi hakuna dili? Hata Harmonize namuonea huruma sababu hajui sarakasi za sihasa...na washauri wake wanafuata upepo
Utakuwa ndio mwisho wa umaarufu wa Diamond. Ndani ya bunge hatakuwa na chochote cha kumpa umaarufu..
 
Huu ubunge siku hizi hauna maana tena. Niliona hata Mkulu akimpigia debe mwimba muziki wa kiume anae suka nywele kwamba nae anafaa kuwa mbunge.. Yaani haya ni mambo ya aibu mno.
Hii nchi imekua kituko kwakweli halafu eti akienda immigration au baadhi ya ofisi za Serikali ukiwa umevaa Jean's anazuiwa kuingia kwa sababu unaonekana muhuni Sasa huyu wa kusuka je ... jamani nakaa pembeni nachekiiii halafu nasema hiiiiii yaaani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TANZANIA TUTAKUWA HATUNA TENA BUNGE,TUTAKUWA WA LIDUDE LA AJABU AJABU LISILO NA FAIDA LISILO NA WASOMI YAANI IN SHORT HASARA TUPU.BORA WAFUTE NA BUNGE LENYEWE KUWE NA BARAZA LA CONGRESS.
 
Kabisa yaani. Wewe tuna mtazamo sawa. Diamond ni mkubwa kuliko ubunge. Akienda huko naona atapotea tu. Maana kwenye music yake yupo Ontop kabisa kwa sasa.
Sio lazima awe yeye,,inaweza pia kutumika influence yake kukipata hicho kiti
Sijamsikia mzee wa twitter sijui yupo likizo malibu
 
Na aibu kweli kabisa ila siasa ni ushetani kabisa
Huu ubunge siku hizi hauna maana tena. Niliona hata Mkulu akimpigia debe mwimba muziki wa kiume anae suka nywele kwamba nae anafaa kuwa mbunge.. Yaani haya ni mambo ya aibu mno.

Sent from my HTC Desire 626GPLUS dual sim using JamiiForums mobile app
 
Wewe ni gwiji wa kupika majungu - kwani kati ya Zitto Kabwe na Diamond nani hutumia twitter kwa kiwango kikubwa?

Zitto amepikwa kwa muda mrefu sana na ameiva kiasi cha kuweza hata kuaminiwa kwa nafasi za juu. Diamond hawezi labda agombee Ubungo si Kigoma.
 
Huu ubunge siku hizi hauna maana tena. Niliona hata Mkulu akimpigia debe mwimba muziki wa kiume anae suka nywele kwamba nae anafaa kuwa mbunge.. Yaani haya ni mambo ya aibu mno.
Yawezekana ni mbinu ya serikali kuwafanya vijana hawa waanze kutunga nyimbo za maadili. Maana wakiachwa kwa mwendo wao walionao, watapoteza kizazi chetu cha sasa na vijavyo kwenye mambo ya 'ufuska' na utovu wa nidhamu. Wewe huoni sugu alivyotulia baada ya kuwa mbunge.
 
Waendelee kucheza na maisha ya watu ila mwisho wao upo!
masoudkipanya_B62FJ1KDOIG.jpeg
 
Kabisa yaani. Wewe tuna mtazamo sawa. Diamond ni mkubwa kuliko ubunge. Akienda huko naona atapotea tu. Maana kwenye music yake yupo Ontop kabisa kwa sasa.
Ni bora aondoke akiwa bado yupo juu....
mabingwa wote hufanya hivyo....
 
Kwamba Diamond ndiye ataenda kuishi kigoma zaidi kuliko Zitto?

Mkata viuno anakuwa mbunge only in black continent!
Mbona Swazineger alikuwa Gavana wa Texas kwa miaka mingi, Man Paciao ni mbunge bobby wine sugu profJ, muda mwingine wananchi wanahitaji faraja zaidi.
 
Kwa akili za Watanzania, Diamond hata akigombea Urais anashinda. Ila Diamond hajijui tu kuwa yeye ni mkubwa kuliko wanasiasa.Tena akigombea Kigoma atashinda asubuhi kabisa.

Mwaka 2015 kituo nilichopiga kura mimi, alikuja mzee mmoja kupiga kura. Akapewa karatasi akaenda kwenye kibox cha siri aweke tiki kwa mgombea ampendae. Ghafla mzee alirudi akiwa mkali sana huki akiuliza anafanyiwa uhuni gani mbona haoni picha wala jina la Diamond? Akajibiwa si mgombea wa nafasi yoyote. Mzee akasema si kweli Diamond amezunguka nchi nzima akifanya kampeni iweje si mgombea? Aliahirisha hata kupiga kula
 
Back
Top Bottom