Ubungo, Mabibo, Mburahati, Manzese hakuna maji siku zaidi ya tano sasa

Ni udhihirisho kuwa hakuna mifumo inayofanya kazi. Siku 5 hakuna suluhisho kwa tatizo dogo lisilohitaji complez technology, je yakija makubwa, si tutaishi nayo milele?
Je ofisi zao zipo jf!
 
Mkuu mpigie simu Makonda aje asikilize hiyo kero ya wananchi na kuitatua hapo hapo.
Wacha amalize mission ya mikoa 20 akirudi tu anamaliza umeme na maji kazi kazi mwendo wa jpm mapigo na mwendo!
 
Nani kama Mama!
Hivi kwanini Samia alimuondoa Engineer Luhemeja pale DAWASA,pamoja na upungufu alionao wa kibinadamu ila jamaa alikuwa kichwa sana.
Sasa hivi eti ni Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu![emoji1787]
 
Ni udhihirisho kuwa hakuna mifumo inayofanya kazi. Siku 5 hakuna suluhisho kwa tatizo dogo lisilohitaji complez technology, je yakija makubwa, si tutaishi nayo milele?
Sijajua wanao mshauri Mama Kizimkazi;alimuondoa Engineer Luhemeja aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa DAWASA na sasa ni Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu!
Jamaa alikuwa vizuri sana na aliibadilisha DAWASA sana;sasa uko ofisi ya Waziri Mkuu sijui anafanya kazi gani!
Mambo ya viongozi wa Tanganyika ni magumu sana kuyaelewa!
 
Hivi tuna Mbundu Ubungo?. Nipeni jina tafadhali
 
Ni udhihirisho kuwa hakuna mifumo inayofanya kazi. Siku 5 hakuna suluhisho kwa tatizo dogo lisilohitaji complez technology, je yakija makubwa, si tutaishi nayo milele?
TANESCO na DAWASA ni watoto wa Baba mmoja na Mama mmoja, huyu DAWASA anasema TANESCO hampi umeme wa kuendeshea mitambo yake ndio maana maji yamekua ya shida Ila TANESCO hasemi nani anaesababisha yeye asimsababishie umeme wa uhakika DAWASA ili aweze kuendeshea mitambo na kuwapatia maji ya kutosha wananchi in short hapo kuna figisu figisu baina ya hao watoto wawili wa Mama Tanzania na hio inapelekea hali ya huduma za kusuasua umeme wa kugawa kwa vipimo na maji ya kupimiana kwa vipimo mwendo wa kubanwa tu

Hii inanikumbusha Movie moja ya 'Mada Max: Fury Road - The Future Belongs to The Mad' yule mshenzi kayafungia maji kwenye miamba watu wanaishi na kiu yeye anatanua tu pumbafu
 
Nani kama Mama!
Hivi kwanini Samia alimuondoa Engineer Luhemeja pale DAWASA,pamoja na upungufu alionao wa kibinadamu ila jamaa alikuwa kichwa sana.
Sasa hivi eti ni Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu![emoji1787]
Hahahaha kaweka Watu wake
 
Mkuu Elli.
Juzi nimeriport mtaani kwetu tuna zaidi ya siku 7 (saba) hakuna maji, hali ni tete sana.
Sijajua DAWASCO wamekumbwa na nini! hali hii ikiendelea kunauwezekano mkubwa wa kulipuka kwa magonjwa ya tumbo (kuhara, kutapika, minyoo, na mengine mengi)
 
Subirini ziara ya Mako da pande hizo...

Wakishafabya maigizo yao na kura mtawapa kisha mtakuja kutulalamikia tena kuwa hampati maji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…