Ubungo, Mabibo, Mburahati, Manzese hakuna maji siku zaidi ya tano sasa

Nafikir mambo mengine japo ccm inahusika lakin yako attached sana na utendaji na watemdaji wa serikali katika taass husika. Taasis ambazo ni za kiraia zisizobagua vyama, yan huko tuko mimi na wewe.
Watendaji ambao wakisimama madhabahu za kisiasa wanaitetea CCM kwa fahamu zao zote....

Serikali na CCM ni damu na kirusi
 
Serikali sikivu ya miccm inalifanyia kazi, mleta mada ukae kwa utulivu.
 
Nafikir mambo mengine japo ccm inahusika lakin yako attached sana na utendaji na watemdaji wa serikali katika taass husika. Taasis ambazo ni za kiraia zisizobagua vyama, yan huko tuko mimi na wewe.
Bila shaka umefahamishwa kuwa serikali, taasisi na watendaji wake wote wanatekeleza ilani ya CCM. Asiyetaka anaambiwa aachie ngazi. CCM ndiyo inayoisimamia serikali.

Ziara na mbwembwe za Makonda ni katika muktadha huo.
 
Inasikitisha sana jiji kama la Dar es salaam eti kuna shida ya maji wakati Mito yote na maporomoko yote yaliyoko kuu yanamwaga maji baharini.

tunashindwa kujenga reservour kubwa at low side maeneo fulani ya pwani na kutunza maji Kwa ajili ya backup ya mitaa ya Dar es salaam na maeneo yote yanayozunguka baadala ya kuachia maji yote yanayotiririka kutokea Moro na Maeneo ya Pwani kuelekea baharini.
 
Hili Jiji lina kero kubwa ya Maji.

Sijui mamlaka kama hata wanajali.

Ndiyo maana binafsi niliamua kuchimba Kisima changu, nikafunga pampu na kupandisha SimTank , hiyo kero ya Maji nimebaki kuisikia Kwa majirani tu.

Kwasasa nimebaki na Kero ya Umeme, Kuna jamaa nimempa kazi ya ku-design Solar Panels system za kuweza kuwasha taa/Tv/Friji/Mota ya Pampu/Feni n.k

Nikifanikiwa hili, hao Tanesco hawataona nalipia Luku zao ambazo zimebaki kama geresha tu.
 
Saaafi kabisa Ndugu yangu
 
Hakika Ndugu yangu, bahati mbaya Sana tunapozungumza mambo ya Msingi kama haya wapuuzi wachache wanaona ni SIASA
 
Saaafi kabisa Ndugu yangu
Uzuri wa DSM water table Iko juu, ukichimba kisima kama nyumba ni yako una uhakika wa kupata Maji sio kama Mikoani.

Kule Chunya unaweza kuchimba hata kisima cha mita 200 ukaishia kukosa Maji.

Kama hali ya Uduni wa huduma ikaendelea hivi, nahisi watakosa kura Hawa Chama Kongwe
 
Wananchi hawamini kwamba viongozi hawana mda nao.
 
CCM Oyeeeee kidumu chama Cha Majambazi
 
Mmh hapana aisee
Pamoja na mapungufu,lkn Kwa baadhi ya vitu km umeme nimemkumbuka
Angekuepo yule mkono wa Chuma kuna washenzi hapo TANESCO sasa hivi wangekua wanacheza nyuma ya Goli yaan wangeshaondolewa uwanjani kitambo sana tena wangelishwa na umeme kabisa (red card) hakuna kurudi uwanjani tena
 
Bila shaka umefahamishwa kuwa serikali, taasisi na watendaji wake wote wanatekeleza ilani ya CCM. Asiyetaka anaambiwa aachie ngazi. CCM ndiyo inayoisimamia serikali.

Ziara na mbwembwe za Makonda ni katika muktadha huo.
Yah nakubal ndio maana niksaema ccm is attached but ,bado kuna mambo ni uzembe na kutowajibika wa watenda kazi wa hizo taasis husika mkuu, tukubali tu.
 
Yah nakubal ndio maana niksaema ccm is attached but ,bado kuna mambo ni uzembe na kutowajibika wa watenda kazi wa hizo taasis husika mkuu, tukubali tu.
CCM wangekuwa wanategemea kura za wananchi kushinda na kushika madaraka ya serikali, usingeona huo uzembe na kutowajibika kwa hao watenda kazi kwa kiwango kikubwa hivi.

Mamlaka ya uteuzi, ajira na nidhamu serikalini ni factor kubwa sana katika utendaji wa waajiriwa na taasisi zake. Usipoliona hilo sina cha kuongeza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…