UBUNGO: Rais Magufuli afungua daraja la juu la Kijazi (Kijazi Interchange)

UBUNGO: Rais Magufuli afungua daraja la juu la Kijazi (Kijazi Interchange)

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Rais Magufuli leo anaanza ziara ya siku tatu mkoani Dar es Salaam ambapo atafungua miradi mbalimbali.

Kituo kikuu kipya cha mabasi ya mikoani Mbezi ni moja ya miradi itakayofunguliwa leo.

===

MATUKIO MBALIMBALI YALIYOJIRI:

Rais Magufuli amewasili Ubungo tayari kabisa kufungua barabara za juu.

Barabara imeshafunguliwa rasmi na kupewa jina la Daraja la Juu la Kijazi.

Injinia Godfrey Kasekenya, Naibu waziri wa ujenzi: Nashukuru kukubali mwaliko wetu wa kuwa mgeni Rasmi. Umekubali kutenga muda wako kuja kujumuika nasi katika shughuli hii. Jukumu langu ni kukukaribisha kufungua rasmi barabara hizi zilizokamilika kujengwa.

HOTUBA YA RAIS MAGUFULI
RAIS MAGUFULI: Napenda nichukue nafasi hii kuwashukuru wananchi wote mliojitokeza hapa, napenda niwashukuru sana kwa kura nyingi nilizozipata na kuniwezesha mimi kuwa Rais wenu, asanteni sana.

Wana Dar es Salaam na watanzania kwa ujumla katika kipindi cha miaka 60 tangu tupate uhuru mwaka 61 wanafahamu shida zilizukuwa hapa Ubungo. Wanafahamu hali halisi waliyokuwa wanaipata wakiwa hapa Ubungo, Ubungo hapa palikuwa ni pa shida.

Wapo watu walipoteza maisha yao hapa na mimi namkumbuka kwenye mwaka 2015 wakati tunafanya kampeni, Staff sajenti mmoja ambae alikuwa muongoza pikipiki alifia hapa kwenye mataa, Mungu aziweke roho za marehemu waliotangulia kwa amani.

Kwa wazaramu hapa palikuwa panaitwa 'Black spot', nina uhakika wapo watu walipoteza maisha yao hapa kwa kuchelewa kufika Muhimbili au kwenye hospitali wakati wangeweza kutibiwa, wapo watu waliochelewa hata safari zao za haraka wakiwa wanaenda Airport, wapo watu waliopoteza wachumba zao kwa kuchelewa kwenda kufunga ndoa kwa sababu ya junction ya Ubungo na inawezekana zipo ndoa zilizoachika kwa sababu watu walichelewa kufika nyumbani kwasababu ya matatizo ya hapa Ubungo.

Ndiyo maana nasimama hapa ndugu zangu kuungana na nyinyi nikisema leo ni siku ya furaha, ni siku ya furaha kwa kila mmoja wetu.

Tungeweza kulijenga wenyewe lakini kupanga ni kuchagua, ukiwa unaaminika kwenye mikopo, ukiwa wanajua kwamba wakikukopesha utalipa, ukiwa ni tajiri na matajiri wengi wanakopa na sisi matajiri wa Tanzania tuliamua kwenda kukopa benki ya Dunia kwasababu tutakaporudisha ule mkopo lazima turudishe na interest kwahiyo waliamini watarudisha huo mkopo pamoja na interest.

Na haya nataka kusema bila kumung'unya maneno, hii ni ahadi ya chama cha mapinduzi kwamba tutajenga daraja pale Ubungo na kama tulivyoahidi mwaka huu tutajenga madaraja karibu kumi kwa Dar es Salaam ya kupunguza misongamano na kutoa ajali.

Kijazi interchange.jpg

Dar es Salaam nadhani inazidi hata baadhi ya mitaa ya Ulaya, sijaenda Ulaya siku nyingi lakini naona sasahivi Ulaya iko Dar es Salaam na mimi nataka kuwahakikishia wa Dar es Salaam, ninajua makao makuu sasa niko Dodoma lakini Dar es Salaam sitaiacha, nitahakikisha tunatengeneza barabara, hata hizi barabara za mitaa.

Katika miaka mitano iliyopita tumefanya mageuzi makubwa katika mitaa yenu. Tumetumia zaidi ya trilioni 1 kufanya mabadiliko makubwa katika mitaa ya Dar es Salaam. Leo nenda mpaka Mbagala, nenda hata ndani uchochoroni utakutana na lami, ukienda Sinza utakuta kuna barabara nne, hapa tunatandika barabara nane, wengine walisema ni pana mno, hiyo ndiyo Dar es Salaam.

Magari yanayopita hapa kwa siku tumeeleza ni zaidi ya 68,839. Yakae yanasubiriana barabarani unaweza kuona changamoto iliyokuwa inapatikana, leo magari yanapishana na inawezekana watu wameshasahau kwamba hapa palikuwa na msongamano mkubwa.

Katika jiji la Dar es Salaam mtaona ma-flyover mengi yanatengenezwa, niliamua interchange hii tuiite jina la marehemu Kijazi na nafikiri wana Dar es Salaam mtakubaliana na mimi. Marehemu Kijazi amefanya kazi kubwa sana katika sekta ya barabara, alikuwa ni mtu ambae hana makuu, yeye ndie alikuwa mkurugenzi wa barabara nchini, baada ya kutoka yeye ndio akateuliwa Mfugale na baada ya Mfugale akaja Alhaji Iyombe ambae nae bahati nzuri akaja kuwa katibu mkuu na balozi Kijazi nae akawa Katibu mkuu.

Mfugale ameumisi ukatibu mkuu kwasababu hata umri sasahivi hawezi akateuliwa kuwa katibu mkuu lakini ni ukweli usiopingika kwamba balozi Kijazi alifanya kazi yake kwa uadilifu mkubwa.

Miradi hii yote hata ya Dar es Salaam, ya masoko, stendi na kadhalika, yeyendie alikuwa katibu mkuu kiongozi na yeye ndie alikuwa kiongozi katika MTC, Braza la makatibu wakuu wote, kwahiyo kwa njia moja au nyingine amechangia kwa kiasi kikubwa sana katika kufanikiwa miradi hii.

Ndio maana sikusubiri kwa mujibu wa sheria kumuacha waziri au wizara ya ujenzi watangaze jina la interchange hii, nikaona niwahi wahi ili niite interchange hii jina la kijazi kwasababu ninajua atakaekuja kulifuta hili jina ni Rais atakaekuja au mwingine nae nitamshangaa kwanini alifute jina la Kijazi.

Magufuli 2.jpg

Nategemea jiji la Dar es Slaam kulivunja na hii nawaambia hapa ili tutengeneze jiji la eneo fulani, tunaweza tukaifanya Ilala ndio ikawa jiji, itadepend na mamo yatakavyoenda lakini kuwa na madiwani ambao wanakaa hapa juu, wanachangiwa hela, hawana miradi ya maendeleo, wanakula posho na hawakuchaguliwa na watu, hili nitalikataza.

Kwahiyo ninalizungumza hapa, wale wanaojiandaa kuwa mameya wa jiji la Dar es Salaam na wanakaa hawana maeneo wajue hicho kimekwisha. Tunataka Manispaa moja katika jiji la Dar es Salaam ndio ipandishwe hadhi iwe jiji halafu nyingine ziwe manispaa, ni kama ilivyo katika majiji mengine.

Kwahiyo mjiandae kisaikolojia wale waliokuwa wanataka umeya wajiji la Dar es Salaam, meya atapatikana kutoka Ilala au kutoka manispaa mojawapo ya hapa, huu ndio ukweli na ukweli utabaki kuwa ukweli na draft nimeshaletewa na mheshimiwa Jaffo, nafikiri nikitoka huku nitakwenda kuisaini. Ili turahisishe mambo, bajeti ya jiji ambayo haipo, fedha zilikuwa zinapotea ndugu zangu waheshimiwa wabunge, jiji la Dar es Salaam litaendelea kuwepo lakini tutachukua eneo fulani nafikiri Ilala inafaa kuwa jiji, ndio katikati ya jiji la Dar es Salaam, wewe Ubungo utasubiri kwanza kwasababu hata barabara bado hazijatengenezwa tengenezwa lakini nafanya haya ndugu zangu kwa kuangalia matumizi mazuri ya fedha zetu.

Magufuli 3.jpg

Niwaombe madereva mlitunze daraja hili. Msimwage mwage Oil pale juu, wala lisigongwe gongwe. Kamwe msifungue boriti. Tulitunze lidumu. Hii ni mali ya Watanzania ni lazima itunzwe.

Niwaambie Makandarasi wasitafute visingizio vya kutomaliza kazi. Mara korona... Hawa wamemaliza mradi huu wakati wa korona. Niwaombe Watendaji wangu ukikuta Mkandarasi anachelewesha kazi na anasema kwa sababu ya korona, mfukuze kazi akakoronee huko.

Tuendelee kutimiza yale tuliyoyaahidi katika maeneo yetu mbalimbali, katika majimbo yetu tutembelee tujue kero zetu, tusiwe tunasubiri kero mpaka itoke kama ile shule, ni lazima sisi viongozi tujipange katika kutatua kero katika maeneo yetu.

Ninashukuru mkuu wa mkoa ulivamia pale na kuanza kushughulikia lakini ile shule ingekuwa mpaka leo haijajengwa, nilitaka nitoe Demo. Ningeanzia mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, mkurugenzi, sijui mwenyekiti wa council mpaka mwenyekiti wa kijiji kwasababu wananchi hawa waliotuchagua wanataka waone amatokeo wa yale tuliyoyaahidi, hata waziri.

Kwahiyo mkuu wa mkoa nakushukuru, malaika walikugusa ukawahi haraka haraka nikawa nakuangalia, nikasema Makunenge oyee kwa sababu mkuu wako wa wilaya alishaanza kulalamika hawa wanatumiwa, wanatumiwa wakati wanaeleza ukweli?
 
Safii ni ukamilikaji kwa ilani ya chama cha mapinduzi.
Tuoshe mikono na tuvae barakoa ukiona dalili usiache kwenda kituo cha afya usinde kwa mganga!
Waongoza msafara na mfunguzi wa hayo majengo hana barakoa!
 
Hoja itakua Corona na Vita vya kiuchumi, sio Wapinzani tena! Ikiisha Corona kumtia aibu sijui atahamia kwenye ajenda gani tena
Hivi wapinzani wako wapi! Mbona hatuwasikii tena? Hata kuitisha press conference zao walizozizoea hakuna!

Kwani, CCM imetekeleza yote waliyokuwa wanapinga? Kimya kimekua kingi - kumebaki na wapinzani wachache (vibarakoa) ndio wanasikika tu!
 
Back
Top Bottom