Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi


Nawaonea huruma kama watakubali kuchukua hisani ya vitu hivyo na kutoa kura zao. Kilio kitafuata baadaye. Maana duniani hakuna cha bure. Ukilataka cha bure mwisho wake utalipa tu.................tena kwa nguvu.
 

Wanaweza kuwa matajiri wakubwa lakini sina hakika kama Fisadi RA anatoka Kanda ya Ziwa. Pamoja na hayo Mtanzania wa leo anajua uchafu ambao wamekuwa wakiufanya na wanaendelea kuufanya. Vilevile sina hakika kuwa hata wale watanzania wenye maisha duni wanaweza kuuza haki yako kupitia kwa hao FISADIZ. Alama za nyakati ziko wazi na zinasomeka hata kwa yule aliyepitia GUMBALU.
 

- Strong analysis na ni karibu na ukweli wenyewe, heshima ikufikie mkuu.

William.
 
Uchaguzi Busanda Mafisadi ndani ya CCM wanatumaliza- Malecela
majira, Tuesday, 19 May 2009 17:07

WAKATI kampeni za Uchaguzi Mdogo Jimbo la Busanda wilayani Geita zikielekea ukingoni, Makamu Mwenyekiti msataafu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Bw. John Malecela amelalamika kuwa chama chake kinahujumiwa na mafisadi kwa kushirikiana na baadhi ya wabunge na makada wake.

Kada huyo mkongwe,alikiri kuwepo upinzani ndani na nje
ya CCM na kubainisha kuwa baadhi ya wanaCCM wenzao, wakiwemo wabunge na makada wa chama hicho, wanataka washindwe uchaguzi huo na wamekuwa wakitumia vyombo vya habari kukidhoofisha chama hicho.

"Baadhi ya mafisadi waliopo ndani ya chama ndio wanaoeneza
propaganda kwenye vyombo vya habari ili CCM ishindwe, lakini uongo haubadiliki kuwa ukweli na kila siku utabaki kuwa uongo, na ukweli utabaki kuwa ukweli"
alisema, Bw.Malecela wakati kizungumza na waandishi wa habari jana katika kijiji cha Nyarugusu.
 

Ni Kweli Hawakuweka Mgombea lakini Hawakumuunga Mkono Mgombea wa CHADEMA na wala hawakuilaani NCCR-Mageuzi kwa Kusimamisha Mgombea so acha Kuzusha Mkuu. Siungi Mkono Suala la Kuunga Mkono acha Vyama vijijenge vyenyewe vyenye Nguvu vitabakia dhaifu vitakufa. This is the survival of the Fittest Mkuu.

Ni Udhaifu na Unafiki Mkubwa kuungana na Wanafiki.
 
hata siku moja hawawezi kupelekwa busanda,
we unafikiri ccm ni wapumbavu kias hicho?!

Hawawezi kuthubutu hata kwa chembe kuwapeleka hawa jamaa. Kwanza itakuwa fujo maana sidhani jamaa kama watawaacha wapite mitaani. Pili hawa jamaa kwenye jamii si watu wazuri wanajulikana kwa matendo yao hivyo hawakubaliki. Tatu inawezekana CCM imeamua kuachia Busanda kwa wapinzani.
 
Miaka michache nyuma CCM walikuwa hawapati taabu za namna hii.
Watu waamini kuwa TANZANIA BILA YA CCM INAWEZEKANA.
 

Bora kukaa na mjinga kuliko kibaraka, usitupe mbachao kwa msaala upitao,
Chemchemi si kemi, mvivu ndiye mvunja moyo,
nikipata vocha, jioni nitakupigia.
..... .......... ....... ...........
 
Wadau, kwa kweli mimi nachoshwa kabisa na hii CCM! Ndiyo! Kinachofanyika katika uchaguzi mdogo wa Busanda ni uharibifu wa Demokrasia na bila aibu wala kujali CCM wanatuingiza kwenye gharama kubwa sana.

Matukio na Kampeni za Uchaguzi huo yanaonyesha kuwa uchaguzi huo umeshakuwa batili maana CCM wanatumia mbinu zote chafu kushinda uchaguzi huo baada ya kuona kuwa kampeni halali na za kistaarabu hazitawawezesha kushinda uchaguzi huo.

MFANO:

Moja; Imeripotiwa kuwa mgombea wa CCM ametumia lugha ya Kisukuma (ukabila) kwenye kampeni zake na hii ni kinyume cha sheria za Uchaguzi.

Mbili; meripotiwa kuwa CCM wamegawa zawadi kama vile kanga na Tshirts wakati wa Kampeni; hiyo ni rushwa na ni kinyume cha sheria za uchaguzi.

Tatu, imeripotiwa kuwa CCMwamewataka wananchi wa Busanda waiisogelee (wasihudhurie?) helkopta ya CHADEMA kwani yaweza kulipuka kama mabomu ya Mbagala (vitisho na kuzuia 'washamba' wa Busanda waihudhurie Kampeni za CHADEMS)! Hii pia ni kinyume cha sheria za uchaguzi.

Nnne; CCM (Serikali yake) imeripotiwa 'kumwaga' nguzo za Umeme ili kuwashawishi wananchi wa Busanda kuipigia kura CCM! What a shame! Hiyo pia ni rushwa na kinyume cha sheria za uchaguzi maana kuleta umeme wakati wa Kampeni za Uchaguzi ni kuwapa rushwa wana-Busanda ili waendelee kuipa kura CCM.

Sababu hizo nne zinatosha kabisa kuufanya uchaguzi huo kutokuwa halali na ikiwa CCM watashinda ni wazi kuwa wapinzania wataenda Mahakamani kupinga. Kwa kuwa kesi za uchaguzi zinachukua muda mrefu, hata kama Mahakama itakubali kuwa CCM hawakushinda kihalai basi kipindi cha Uchagiuzi Mkuu kitakuwa kimefika na haitawagharimu CCM chochote! Ikiwa CCM itashinda kwa faulo hizo ni wazi itakuwa vigumu kwa wapinzania kwenda Mahakamani kupinga ushindi huo maana muda uliopo ni mfupi na kwa kufanya hivyo itakuwa ni kuingia gharama za bure.

MAONI YANGU
CCM wasitufanye WaTZ wa leo ni walewale wa enzi zile! Hata tulipo nje ya Busanda tunasikia na kuona mchezo mchafu huo wa CCM na hilo latosha kuondoa credibilty ya CCM kwenye macho ya Watanzania wengi; hiyo itawagharimu sana CCM mwakani.

NAWASILISHA!
 
Tano: CCM imeripotiwa kukamatwa wakinunua shahada za kipigia kura na kupelekea Diwani wao pamoja balozi wa nyumba kumi kumi kukamatwa. Sita: Green Guards wa CCM wameripotiwa kuwapiga na hata kuwaumiza wafuasi wa CHADEMA. Tuendelee kukusanya takwimu kwa ajili ya Biharamulo na chaguzi zitakazofuata.
 
Kwani ni lini Mfa Maji aliacha Kutapatapa?

Pamoja na Zawadi hizo, sitegemei kama watashinda.

Hiyo ishu ya Magogo ya Umeme, acha yamwagwe...lakini KICHEKESHO kitakuwa kama wapinzani wakishinda, na magogo hayo YAKATELEKEZWA, hapo ndo wananchi wa Busanda wajue kuwa CCM ni wana-ZE'KOMEDI, na uchaguzi wa 2010 utakuwa MTAMU zaidi... !

Time will tell kaka, usiogope.
 
The Revolution for freedom in Tanzania will get a new name to be Developments Movements and CCM will be the opposition immediately after the RESULTS ARE OUT BY NEXT MONDAY DESPITE OF ALL THOSE DIRTY TACTICTS ALREADY deployed in BUsanda and known by WANANCHI
 
Hatulipi kodi zetu kuwapa ruzuku ilimtafute visingizio, nyie wapinzani acheni utoto na visingizio vyenu vya ajabu ajabu, hao mafisadi CCM kwani wanawashinda ninyi akili?mnajua wazi hizo ni kampeni na wala msitegemee CCM watawasifia kwa helkopta yenu bali wataiponda tu. Hizo nguzo na CHADEMA wametoa hoja nzuri tu kwa kusema mbona hazikuanza kuweka huko umeme unapotokea sasa wasiwasi wa nini? Ipo siku wananchi watawachoka hata ninyi hasa mnapokuwa mnalialia kila siku huku kazi zenu zinalala.
 
Hiyo ndo potilikis sasa jamani si lazima watu watumie kila mbinu ili kushinda?sioni ubaya wa kutumia kisukuma jimboni kwa wasukuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…