Master Legendary
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 576
- 876
Nimesikiliza Hotuba ya Heche leo akitangaza kugombea Umakamu Mwenyekiti CHADEMA, nimegundua kisiasa Heche ni Mkubwa sana kuliko Lissu ingawa kiharakati Lissu kamuacha mbali sana Heche.
Heche katambua nguvu ya Mbowe ndani ya CHADEMA, hotuba yake imekwepa sana kumshambulia Mbowe Binafsi na imetambua Mchango wa Mbowe kwenye Chama na kumjenga yeye Heche,hii kisiasa imemkwepesha Heche na Chuki kutoka kwa wapiga Kura wa kundi la Mbowe ambao lazima tukubali bado ni wengi ndani ya CHADEMA.Hii kisiasa itamnufaisha sana Heche na kwa watu wenye akili wanamuona Heche ni Asset kubwa sana ya Uongozi ndani ya CHADEMA.
NIkiri nampenda Lissu uwezo wake wa kuongea,akili yake kubwa,Misimamo yake,na naheshimu gharama alizolipa katika kupigania mabadiliko ila nikiri wazi katika hizi Siasa za kugombea Uenyekiti wa CHADEMA binafsi kwa upande wangu zimenifanya nimshushe kidogo, na nikiri wazi kuwa baada ya kumfuatilia nimeona bado Mbowe anastahili kuongoza CHADEMA sitafafanua zaidi ila wanaoona kama mimi watakuwa wamenielewa.
Kwangu mimi naona Mbowe abaki Mwenyekiti,Heche aingie Umakamu,Lissu ateuliwe Mjumbe Kamati Kuu na abaki Mgombea Urais,Godbless Lema ateuliwe Mjumbe Kamati Kuu,Mnyika abaki Katibu Mkuu na Halima Mdee ateuliwe Naibu Katibu Mkuu amsaidie Mnyika kwasababu kapooza Sana simuelewi, mambo ya Usaliti yawekwe pembeni kidogo.
Lissu awekwe chini ya Heche kwa muda afundishwe Siasa na Uongozi wa kitimu akijiandaa kumrithi Mbowe, ikionekana anaendeleza mambo yake basi Heche aandaliwe kumrithi Mbowe.
Ni mtazamo tu masela msijenge Chuki, nakaribisha Povu.