UCHAGUZI CHADEMA: Hotuba ya leo, kisiasa Heche amemucha mbali sana Lissu

Master Legendary

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
576
Reaction score
876
Nimesikiliza Hotuba ya Heche leo akitangaza kugombea Umakamu Mwenyekiti CHADEMA, nimegundua kisiasa Heche ni Mkubwa sana kuliko Lissu ingawa kiharakati Lissu kamuacha mbali sana Heche.

Heche katambua nguvu ya Mbowe ndani ya CHADEMA, hotuba yake imekwepa sana kumshambulia Mbowe Binafsi na imetambua Mchango wa Mbowe kwenye Chama na kumjenga yeye Heche,hii kisiasa imemkwepesha Heche na Chuki kutoka kwa wapiga Kura wa kundi la Mbowe ambao lazima tukubali bado ni wengi ndani ya CHADEMA.Hii kisiasa itamnufaisha sana Heche na kwa watu wenye akili wanamuona Heche ni Asset kubwa sana ya Uongozi ndani ya CHADEMA.

NIkiri nampenda Lissu uwezo wake wa kuongea,akili yake kubwa,Misimamo yake,na naheshimu gharama alizolipa katika kupigania mabadiliko ila nikiri wazi katika hizi Siasa za kugombea Uenyekiti wa CHADEMA binafsi kwa upande wangu zimenifanya nimshushe kidogo, na nikiri wazi kuwa baada ya kumfuatilia nimeona bado Mbowe anastahili kuongoza CHADEMA sitafafanua zaidi ila wanaoona kama mimi watakuwa wamenielewa.

Kwangu mimi naona Mbowe abaki Mwenyekiti,Heche aingie Umakamu,Lissu ateuliwe Mjumbe Kamati Kuu na abaki Mgombea Urais,Godbless Lema ateuliwe Mjumbe Kamati Kuu,Mnyika abaki Katibu Mkuu na Halima Mdee ateuliwe Naibu Katibu Mkuu amsaidie Mnyika kwasababu kapooza Sana simuelewi, mambo ya Usaliti yawekwe pembeni kidogo.

Lissu awekwe chini ya Heche kwa muda afundishwe Siasa na Uongozi wa kitimu akijiandaa kumrithi Mbowe, ikionekana anaendeleza mambo yake basi Heche aandaliwe kumrithi Mbowe.

Ni mtazamo tu masela msijenge Chuki, nakaribisha Povu.
 
Lisu na Heche wote wanagombea kila mtu kwa nafasi yake, wacha wagombee wajumbe wataamua.
 
We sema ni Lissu tu uenyekiti, habari za kusubiri hadi hapo baadae mbowe atoke ndio lissu aje, hiyo waachie akina heche na mnyika
 
Niliwahi kushauri hili jambo
Chadema inaenda kuwa imara Sasa

 
Iko poa hii!. Vinginevyo piga Lisu chini, piga Mbowe chini, uchaguzi uhairishwe na Heche aandaliwe kuwa Mwenyekiti.
 
CCM wote wanataka FAM abaki kuwa mwenyekiti, Kwanini?
 
Heche ameonyesha baba yake wa siasa ni nani,na tabia aliyo nayo ni ya ustaarabu maana Lisu yeye anashambulia mtu mazima,kana kwamba hicho Chama alikita hivyo hivyo na anajiaona ana utendaji uliotukuka ndani ya chama.Ni bora Heche angepewa huo Uenyekiti kabisa kama ingewezekana.
 
Angalau Heche kajaribu kuzungumzia maisha ya wananchi hawa wengine huwa siwaelewagi wanamuwakilisha nani.
 
Moja ya bandiko bora 2025.
Lissu nilimpigia kura 2020,lakini nilikuja kugundua very late hana subra ana mihemko kupita kiasi.

Heche wamwandae kuchukua mikoba 2030.
 
Hapo mwisho ndo uneharibu yaani msaliti mbowe aendelee kushirikiana na ccm kuihujumu chadema na kupiga pesa za mama abdul
 
Lisu kuongea ukweli sio kumshambulia mbowe Acha ujinga km rangi ni nyekundu itamkwe nyekundu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…