UCHAGUZI CHADEMA: Hotuba ya leo, kisiasa Heche amemucha mbali sana Lissu

Tatizo la Heche ni kubeti tu,

akiacha hiyo anaweza kua kitu pale chadema huko mbeleni 🐒
 
Hitimisho lako ndio salama ya CCM hilo ndilo kubwa lililokuleta.
 

Inaelekea hujamuelewa Heche kasema kwa njakati hizi nchi inamtaka Lissu na wengj wanaona hayo. Hii nchi inataka kwa sasa wakunja ngumi
 
Pumba 2pu
 
Wewe ndo kasongoyeye mwenyewe wengine wanaigiza tu
 
Nakubaliana na wewe kwa 💯; busara ya kiuongozi naona Lissu bado hana; sioni kama anaweza kuunganisha team, yeye pamoja na Wenje naona kama wana fanana sana. Hehe ni habari nyingine; kwangu mimi ili kuziondoa tofauti au nyufa zilizo tokea Chadema kupitia Lissu na Mbowe, better wote wasichaguliwe; kwa mtazamo wangu, Heche is/was the right candidate on that post. Walau makundi yote 2, team Mbowe na Lissu wote watakua wamepoteza. Kwasasa sioni team Mbowe kama inaweza kufanya kazi na Lissu; chukulia maoni ya kina Ntobi, Yerico Nyerere; wale wanaweza kuendelea kua Chadema kweli? Sidhani. Team Lissu as well, endapo Lissu atashindwa, hivi wakikaa kikaoni na Mbowe, wanaweza kuaminiana hawa tena? I don't think so.
 
Lisu hafai kuwa mwenyekiti chadema, Kaonyesha asivyojua siasa, anabwabwaja bila staha bila kufanya tafakari ya anachoongea, na hajui nafasi aliyonayo na wajibu wake.

Tangu awe makamu mwenyekiti hata hajui kafanya nini, zaidi ya kujiita makamu mwenyekiti.

Nashangazwa na,wanaoona anafaa kuwa mwenyekiti wakati hata umakamu mwenyekiti haelewi majukumu ya nafasi hiyo, sijui wanapata wapi hisia kwamba anaweza kuwa mwenyekiti.

Ukiwauliza kafanya nini tangu awe makamu mwenyekiti, wao hawafahamu, na hata yeye hafahamu.

Anadhani kuitwa mwenyekiti ndio sifa za mwenyekiti chadema, bila kujua majukumu ya nafasi ya mwenyekiti.

Anao uwezo kwenye taaluma yake ya sheria, lakini hajitambui kwenye siasa.

Pia huwa sielewi inakuwaje kila analosikia vijiweni bila ushahidi wa kina, anaita press anaongea, unakuwaje mwanasheria huwezi kukusanya ushahidi na kujua upi ni ukweli na zipi porojo za vijiweni, au lipi linaongelewa wapi na lipi haliongelewi wapi?

Hata akishindwa kwenye nafasi ya mwenyekiti taifa chadema, uongozi ndani ya chama asipewe kwasababu hajui miiko ya uongozi, awe tu mwanachama mtiifu, au ahame aende huko aendako, au aanzishe chama tumuangalie atakavyo kilea hadi kikuwe.
 
Wanaomtaka Lissu wanamhitaji kwa kitu kimoja tu: kuanzisha mapambano; kuwasha moto (confrontation) dhidi ya CCM aka dola. Basi. Na kama mwanaharakati amethibitisha sifa hiyo pasi na shaka. Msimamo wake kwenye harakati hauhojiki. Amejitoa mhanga sana na ni wazi kuwa mahasimu wake hawajafanikiwa “kumfikisha bei” - tangu miaka ya 1990 (mwishoni).

LAKINI pia inaonekana wazi kabisa Lissu hana karama ya kujenga na kuongoza taasisi (institutional management), kazi inayodai sana uelewa, uvumilivu, subira na kuwa tayari kuelimisha na kuweka maelewano kati ya makada, watendaji, wafuasi na mashabiki wenye uelewa, karama na uwezo tofauti tofauti kuhusu malengo na sera za chama. It’s all boring to him. Ana haraka ya kufanikisha kile anachotaka bila kusumbuka kuhusu aina ya watu anaokuwa nao.

Ni kama Fidel Castro alivyoshindwa kuenenda na camarade Ernesto Che Guevara mara baada ya ukombozi wa Cuba. Castro alikuwa anawaza namna bora ya kuongoza nchi yake na wananchi wenzake kwa ufanisi. Che Guevara alikuwa anaona fursa ya kuwasha moto wa mapinduzi ndani ya Cuba yenyewe na America ya Kusini yote (kufagia takataka zote za mabeberu na kusimika himaya imara za kikomunisti).

Kungekuwa na namna ya kuwapa nafasi hawa wote wenye hizi karama muhimu tofauti tofauti - kwa nyakati sahihi, CHADEMA Ingekuwa katika nafasi bora kabisa kama chama cha kisiasa nchini. Hasa ikieleweka kuwa CCM sasa si chama cha siasa tena bali ni mamlaka kamili ya dola. Na vyama vingine (ukiondoa ACT to some extent) kiasi kikubwa ni mifano (dummies) tu.
 
Kosa kubwa alilofanya Heche ni kujifungamanisha na Lissu waziwazi. Yeye angegombea umakamu kama mgombea huru na kufanya kazi na atakayeshinda ikiwa ni Lissu maana yake kazi yake itakuwa rahisi naana wana mtizamo mmoja wa approach kuhusu hoja zilizo mbele yao kama chama; akishinda Mbowe angekuwa na kazi ya kumshawishi Mwenyekiti Akubaliane na mtizamo wake ( ambao ndiyo mtizamo wa Lissu) kuhusu hoja zilizo mbele ya chama.

Pia hii ingemuandaa kugombea uenyekiti hapo baadae.

Katika chama haiwezekani wote muwe na mtazamo mmoja kuhusu jambo lolote hivyo tofauti ya mitazamo sio usaliti.

Heche kwa kusisitiza Mbowe akae pembeni amejiweka within striking range ya Mbowe.

Nb: haya ni maoni yangu tu.
 
Wanaojiita team Lisu hawaelewi tofauti ya mwanaharakati na kiongozi.
Kwasasa wanafuata mwanaharakati, wanamponda kiongozi aliye walea, aliyefahamu kujenga taasisi kwa kufahamu hivyo vitu viwili na akavitenganisha, ndio maana juzi aliposema yeye ndiye the last line of defense hawakumuelewa.
 
Master legendary mnyika hajapoa bali yeye ni kiongozi mwanasiasa na sio kiongozi mwanaharakati kama slaa kwahiyo hupo kitendaji zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…