Uchaguzi mkuu kiti cha Rais 2025 (video): Unabii waweka wazi kuwa ni Samia S. Hassan (CCM) vs Bishop Josephat Gwajima (CHADEMA)...

Uchaguzi mkuu kiti cha Rais 2025 (video): Unabii waweka wazi kuwa ni Samia S. Hassan (CCM) vs Bishop Josephat Gwajima (CHADEMA)...

Labda CHADEMA tuwe tumerogwa! Gwajima?
Ondoa wazo la kurogwa..

Mungu akiamua iwe hivyo, basi itakuwa hivyo. Hakuna wa kupinga..

Na siku zote Mungu hujibu maombi ya watu wake ktk njia tofauti kabisa na tunavyodhani sisi kama asemavyo katika Neno lake;

‭Isaya 55:8-9 SUV‬

".....Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.."

Kwa Mungu yote yanawrzekana. Hata yule usiyemdhani na hujawahi kumweka katika akili na mawazo yako, anaweza kufanywa Rais wa nchi hii..!
 
Ume text-narrate vizuri sana..

Lakini huyu nabii hajaficha jina kwa herufi "J"

Amemtaja kwa uwazi kabisa kuwa ni Josephat Gwajima...
Nimetumia "J" Ili kupunguza mihemko.

Watu wengi wenye Roho wa Mungu, wamekwishaonyeshwa huyo ndiye ajaye.

Dunia inakwenda kupitia kipigo Cha miaka Saba, sasa Hadi 2030.

Tanzania, ndio Nchi Mungu ameiandaa Ili Ile INJILI ya ufalme sawasawa na Mathayo 24 ihubiriwe tokea hapa.

Inakwenda kurudisha dini Moja/ Kanisa la kwanza litarudi kuabudu J1.Wakristo, Na Hilo Kanisa ndilo litapambana na Mpinga kristo.

KITI hicho kikuu anataka akae Mungu mwenyewe Ili apambane na USHOGA, na Kila aina ya mifumo ovu ya kishetani iliyoko duniani.

Hayupo mwingine awezaye vita hiyo zaidi ya "J".

Kwa miaka 7 ijayo, Mungu akujaalie uhai, utaona mambo ambayo hayajawahi tokea Ulimwenguni, nadhani umeona mafuriko Dubai, uarabuni nk nk, Bado yaja.

Tusubiri.
 
Ninaposema chaguo la Mungu ni wakati wa sasa ,baada ya miaka 5 ni ishu nyingine anaweza asiwepo...Yote sawa.
Sio baada ya miaka mi5..

Huyu mama aliwekwa ktk kipindi hiki cha mpito ili tu ku - comply na takwa la kikatiba la kuwa VP atakuwa full president kama Rais aliyepo atafariki akiwa madarakani na kumalizia muda uliobaki..

Narudia tena kusema, huyu mama mwisho wake ni 2025. Hata kwa akili za kibinadamu tu ni kuwa huyu hawezi na amesha prove failures...
Kwa wakati uliopo ilipangwa ndio maana hata kifo cha Magufuli hakikutarajiwa ni mpango wa Mungu ambao upo nje ya uwezo wetu.
Yes, I agree. Nisome hapo juu☝🏻☝🏻☝🏻
Lolote linaweza kutokea ,humu ndani kuna jamaa aliandika utabiri wa Mwanamke haswa Samia kushika usukani ,hatuwezi kudharau hatujui lolote .
Na hili nakubaliana na wewe.
Hata Josephat Gwajima anaweza kuwa Rais wa Tanzania kupitia CHADEMA..
Mungu anaweza kufanya yote. Anaweza kugeuza lolote kuwa chochote...
 
NB:
Naomba moderators tafadhali ruhusuni mada hii ijadiliwe. Msiogope, haina madhara yoyote kwenu na JF kwa sbb hii ni kitu halisi na mtu aliyetoa unabii huu yupo na anaweza kuulizwa na kuthibitisha haya

==============================================

Ukiitazama na kuisikiliza hii video ya unabii huu toka kwa Mwl. Steven Jacob, toka Arusha, inafikirisha na kutafakarisha kiasi chake. Tazama na sikiliza👇🏻👇🏻👇
View attachment 2969906

Kwa ufupi sana kwa wale wasio na vifurushi:

1. Mama Samia Suluhu Hassan (Rais wa sasa wa JMT) amekataliwa na Mungu - Jehovah, hatakiwi kugombea kiti cha Urais mwaka 2025. Si chaguo la Mungu - Jehova kuiongoza Tanzania mwaka 2025 - 2030..

2. Pamoja na kuwa ameshakataliwa, kitakachokuwa ni ajabu ni kuwa yeye na watu wake watalazimisha agombee. Na kwa mujibu wa unabii huu, ni kuwa atapitishwa kwa hila, atagombea lakini habari njema kwa wanamageuzi wote ni kuwa HATASHINDA UCHAGUZI HUO..!

3. Wakati huohuo ndani ya CCM yupo mtu ambaye Mungu keshamweka kuwa ndiye agombee na awe Rais ajaye wa Tanzania na jina lake katajwa kwa uwazi kabisa kuwa ni Bishop Josephat Gwajima. Ila wenzake ndani ya CCM watamkataa na hawatampa nafasi hiyo..

4. Kwa mujibu wa unabii huu, CHADEMA hawana mtu ambaye ana kibali cha Mungu - Yehova kugombea kiti cha u - Rais mwaka 2025 aliye ndani ya chama chao..

5. Na kwa kuwa Mungu tayari ameshampaka mafuta ya u - Rais wa nchi hii ndugu Josephat Gwajima, na kwa CCM watakuwa wamemkataa, basi Mungu atatengeneza mazingira ya kumtoa CCM na mara moja Freeman Mbowe au CHADEMA watampa nafasi ya ugombea u - Rais na CHADEMA kupitia kwa Ndugu Josephat Gwajima, watashinda na kuitawala nchi kwa mara ya kwanza..

6. Kwa Mama Samia Suluhu Hassan na CCM , unabii unasema, systematically Mungu ataachilia aibu iliyo kuu kwake na CCM itachinjwa kidogo kidogo mpaka ife kabisa..

============================================

MAONI YANGU

1. Pamoja na kuwa sisi wakristo Biblia - Neno la Mungu linatuonya kuwa;

‭1 Wathesalonike 5:20-22 SUV

".....msitweze unabii; jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema; jitengeni na ubaya wa kila namna.."

Lakini wakati huohuo Biblia hiyo hiyo inatuhadharisha kuwa ni lazima kila unabii (kila roho isemayo yatoka kwa Mungu) ipimwe katika vigezo vya Neno la Mungu (Biblia) kama ilivyoandikwa;

‭1 Yohana 4:1-2 SUV‬

"...Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu.."

Ukipimwa na ukaenda sambamba na Neno la Mungu, huo unabii au hiyo roho iliyoleta neno hilo itakuwa inatoka kwa Mungu na kwa hiyo hapaswi mtu kuubeza (kuutweza au kuudharau)..

2. Unabii wa huyu ndugu ni mzito sana. Unahusu hatima ya nchi na taifa letu na watu wa nchi hii kwa ujumla. Natoa wito kwa wajuzi wa maandiko (Neno la Mungu) waje hapa na kutoa uchambuzi usio - base katika hisia na maarifa ya kibinadamu bali ule unaozingatia Neno la Mungu (Biblia...)

3. Je, wewe unasemaje? Toa maoni yako...
Mafi yake
 
Nimetumia "J" Ili kupunguza mihemko.

Watu wengi wenye Roho wa Mungu, wamekwishaonyeshwa huyo ndiye ajaye.

Dunia inakwenda kupitia kipigo Cha miaka Saba, sasa Hadi 2030.

Tanzania, ndio Nchi Mungu ameiandaa Ili Ile INJILI ya ufalme sawasawa na Mathayo 24 ihubiriwe tokea hapa.

Inakwenda kurudisha dini Moja/ Kanisa la kwanza litarudi kuabudu J1.Wakristo, Na Hilo Kanisa ndilo litapambana na Mpinga kristo.

KITI hicho kikuu anataka akae Mungu mwenyewe Ili apambane na USHOGA, na Kila aina ya mifumo ovu ya kishetani iliyoko duniani.

Hayupo mwingine awezaye vita hiyo zaidi ya "J".

Kwa miaka 7 ijayo, Mungu akujaalie uhai, utaona mambo ambayo hayajawahi tokea Ulimwenguni, nadhani umeona mafuriko Dubai, uarabuni nk nk, Bado yaja.

Tusubiri.
Ofcoz, hata mimi natamani na nataka nchi hii iongozwe na Rais mcha Mungu..

Askofu Josephat Gwajima ni mtu sahihi. Na iwe hivyo, amina🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻..!!
 
Sio baada ya miaka mi5..

Huyu mama aliwekwa ktk kipindi hiki cha mpito ili tu ku - comply na takwa la kikatiba la kuwa VP atakuwa full president kama Rais aliyepo atafariki akiwa madarakani na kumalizia muda uliobaki..

Narudia tena kusema, huyu mama mwisho wake ni 2025. Hata kwa akili za kibinadamu tu ni kuwa huyu hawezi na amesha prove failures...

Yes, I agree. Nisome hapo juu☝🏻☝🏻☝🏻

Na hili nakubaliana na wewe.
Hata Josephat Gwajima anaweza kuwa Rais wa Tanzania kupitia CHADEMA..
Mungu anaweza kufanya yote. Anaweza kugeuza lolote kuwa chochote...
Kwa upande wako ila CCM ndio imefeli kwa ujumla ,save post yangu
 
Tunaomba CV yake.
Asijekuwa mwanamfumo maana mara chache Mungu amejihusisha na mambo vyama vingi.
Manabii washakaji wa Trump walifanya sana haya wakati wa uchaguzi.
Nabii Samwel aliyepeleka ujumbe Kwa Daudi kuwa atakuwa mfalme alikuwa mwana mfumo?

Hivi wewe hujui Cheo Cha Urais ni Cheo Cha Mungu Mwenyewe huruhusu watu kukikalia Ili kuongoza watu?

Usidanganywe kuwa Utawala wa Serikali za WANADAMU kuwa Mungu Huwa Hana mkono wake humo.

Open your eyes and see!!
 
Why iwe chadema???? Km kapakwa mafuta si aende chauma akagombee huko😀😀😀😀😀😀😀
 
Ofcoz, hata mimi natamani na nataka nchi hii iongozwe na Rais mcha Mungu..

Askofu Josephat Gwajima ni mtu sahihi. Na iwe hivyo, amina🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻..!!
In other words,

CCM wanaambiwa kuwa, wakimsimamisha Gwajima awe mgombea Urais,

Atashinda Kwa kishindo na kuinusuru CCM na kifo.

Lakini Kwakuwa wamekataa kutubu, acha wafe!!
 
Hicho alichoongea ka copy mahali and paste Toka mahali Fulani Lakini unabii wa ku copy and paste Bila kuangalia uli copy bilacl kujua uhalisia ukojevsi sahihi

Kifupi Kuna waganga wa kienyeji Wana vilinge vyao kwenye vikao vya vilinge vyao vya Uganga gizani wanamtaka Gwajima si kuwa ni chaguo la Mungu la hasha la Shetani kupitia baadhi ya wachawi wa nchi za kiafrika.Wanataka mchawi wao akamate nchi kuwa zamu Yao na waliyemwandaa ni Gwajima

Uzuri watu wa Mungu walishaliona Hilo mapena na kuwa halitafanikiwa .Nchi haviwezi kabidhiwa Kwa wachawi hii .Mama Samia Yuko vizuri na Hana tatizo na Kanisa ana mahusiano mazuri mno

Huyo Mwalimu aelewe Hilo kuwa Hadi vikao vya kichawi vilivyoamua Hilo watu minutes wanazo .Kifupi huo unaoitwa unabii wake haitakuwa
 
Sasa kwa kuwa anadai ni unabii wacha tuwe Wapole ila kikitokea ambacho ni tofauti na huo unabii tunaomba turuhusiwe kumporomoshea mitusi ya nguoni ndugu nabii
 
Nabii Samwel aliyepeleka ujumbe Kwa Daudi kuwa atakuwa mfalme alikuwa mwana mfumo?

Hivi wewe hujui Cheo Cha Urais ni Cheo Cha Mungu Mwenyewe huruhusu watu kukikalia Ili kuongoza watu?

Usidanganywe kuwa Utawala wa Serikali za WANADAMU kuwa Mungu Huwa Hana mkono wake humo.

Open your eyes and see!!
Hiyo kesi haina uhusiano. Samweli alienda direct kwenye matokeo na na kumsema muhusika ( Mfalme ajae).
Sio kupendekeza wagombea ufalme.

Serikali zote ziko chini ya Mungu ni kweli hata kama zinaingia kwa wizi maana yeye ndiye mmiliki wa pumzi za za wezi hao. Ila kesi ya siasa hizi za vyama vingi na mashindano hiyo kesi haipo kwenue biblia.
 
Ngoja tufanye kunukuu tu, kwa matumizi ya baadaye...

Nina swali, mbona Gwajima jimbo limemshinda? Ataweza nchi kweli!!!

5. Na kwa kuwa Mungu tayari ameshampaka mafuta ya u - Rais wa nchi hii ndugu Josephat Gwajima, na kwa CCM watakuwa wamemkataa, basi Mungu atatengeneza mazingira ya kumtoa CCM na mara moja Freeman Mbowe au CHADEMA watampa nafasi ya ugombea u - Rais na CHADEMA kupitia kwa Ndugu Josephat Gwajima, watashinda na kuitawala nchi kwa mara ya kwanza..
 
..mgombea mwenye tuhuma kwamba ni msagaji atashindaje uchaguzi?
 
Back
Top Bottom