Mama hakuna system ya kanda kuwa juu/chini ya kanda nyingine. Ni kweli kanda tunazo ili kurahisisha uratibu na upangaji wa shughuli za maendeleo, lakini siyo kwa lengo la kanda moja kuwa juu au chini ya kanda nyingine.
Advantage waliyonayo kanda ya ziwa ni kuwa kanda iliyo densely populated, kwa hiyo wakihamasishwa vizuri kujiandikisha kupiga kura na wakajitokeza kupiga kura hapo ndipo sisi kanda zingine tunaujua mziki wao.
Btw, huu mtindo tuliouanzisha wa kuwasuta, kuwabagua, kuwatukana, kuwakebehi na kuwashetanisha, nadhani utawafanya wawe na umoja zaidi kiasi kwamba utafika wakati wafikirie kufanya maamuzi yao kwa kujihami, kitu ambacho madhara yake yatakuwa makubwa zaidi. Don't wake up a sleeping giant!