Uchaguzi ujao utakuwa mwepesi sana kwa CCM tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe hapa nchini

Uchaguzi ujao utakuwa mwepesi sana kwa CCM tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe hapa nchini

Tindo rafiki yangu naomba nikwambie kuwa hakuna wa kuleta machafuko nchii hii Wala kuingia Barabarani kuipinga serikali hii shupavu ya CCM,Kama huamini maneno yangu Basi anzisha wewe hayo maandamano na uwe mstari wa mbele, au kamuulize lisu kilichomkuta 2020 ambapo Hadi wewe ulimsaliti kwa kukataa kuingia Barabarani na kubaki umejificha chumbani kwako
Wewe ulishaamua kujitoa akili, endelea kuwa chawa tuu labda kuna siku watakukumbuka
 
Sera na ajenda zinazogusa maisha ya watu pamoja dira na muelekeo unaoeleweka wa CCM ndio vinavyoibeba CCM miaka yote

Ni kweli, ndio maana vyombo vya dola vimekuwa msaada mkubwa wa CCM kukaa madarakani muda wote hata bila ridhaa ya umma.
 
Wewe ulishaamua kujitoa akili, endelea kuwa chawa tuu labda kuna siku watakukumbuka
Mimi naeleza ukweli,labda niambie kwa akili yako Ni kundi gani linaloweza kuwaunga mkono CHADEMA kwa Sasa na kuwapigania kupata Kura? Huoni upinzani ulivyo dhaifu na legelege?
 
Ni kweli, ndio maana vyombo vya dola vimekuwa msaada mkubwa wa CCM kukaa madarakani muda wote hata bila ridhaa ya umma.
CCM IPO madarakani kwa ridhaa ya wananchi ndio maana inaungwa mkono katika Sera na ajenda zake,ndio maana imekuwa ikipigiwa Kura kila uchaguzi ,ndio maana imekuwa ikiendesha serikali kwa utulivu na Amani pasipo mavurugu
 
Ndugu zangu watanzania,

Uchaguzi ujao Ni uchaguzi ambao CCM inakwenda ikiwa na ushindi mkononi, uchaguzi ambao CCM inakwenda ikiwa na Matokeo ya ushindi wa kishindo, Hii Ni kutokana na kazi kubwa Sana iliyofanywa na serikali ya CCM chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Rais Samia katika utekelezaji wa ilani ya CCM.

CCM inakwenda katika uchaguzi huo ikiwa na uungwaji mkono na kibali na baraka kutoka makundi yote kutokana na utendaji kazi wa serikali yake uliyogusa makundi yote pasipo kumwacha mtu nyuma au kundi lolote lile,Inakwenda katika uchaguzi huo ikiwa imejibu maswali yote na kero zote kubwa kwa kuzipatia majibu ya kuridhisha.

CCM inakwenda katika uchaguzi huo ikiwa imejiwekea Rekodi mpya ya maendeleo katika secta zote kuanzia Elimu ambapo Sasa Ni bure Hadi kidato Cha sita, huku ikiwa imeongeza bajeti ya mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu kufikia biliioni 654 kiasi kilichopelekea wanafunzi wote wenye sifa kupata mikopo bila shida ya aina yoyote pamoja na kuongeza fedha za kujikimu kufikia elfu kumi kwa siku Jambo lililoibua shangwe kubwa Sana hapa nchini.

CCM inakwenda katika uchaguzi huo ikiwa imejihakikishia kura za Ndio kwa wakulima baada ya kuwafuta machozi na kuwaheshimisha kwa kukifanya kilimo ni biashara na hivyo kuwafanya kunufaika na jasho lao,huku mabillioni ya Ruzuku takribani billioni Mia moja hamsini yakiwa yametolewa na serikali ya CCM zilizo pelekea kushuka kwa Bei ya mbolea sokoni mfano mbolea ya DAP msimu uliopita ilikuwa inauzwa shillingi laki moja na 40 lakini msimu huu inapatikana kwa Elfu 70 tu.

CCM inakwenda katika uchaguzi huo ikiwa inaungwa mkono na wafanyabiashara wote hapa nchini baada ya kuwa mazingira ya biashara yameboreshwa kwa kuweka Sera nzuri na kuwa na maafikiano mazuri na yenye Afya na tija katika ukadiriaji wa Kodi ,Sasa biashara zinafunguliwa kila Kona ya nchi hii badala ya kufungwa,Sasa TRA na maafisa wake wanatenda haki na kuwatendea haki wafanyabiashara na hivyo kujenga Hali ya kuaminiana katika ulipaji wa Kodi,Hali iliyopelekea kupanda kwa mapato kufikia Trioni mbili kwa Mwezi.

Ni uchaguzi utakao kuwa mwepesi Sana kwa CCM kupita na kuweza kushinda,inakwenda kuzoa Kura kwa kishindo Sana katika nafasi zote,Ni historia mpya inakwenda kuandika hapa nchini katika uchaguzi huo.

Kazi Iendeleee mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu

0742-676627
Lucas huko unakoelekea siko kuzuri hata kidogo. Si ajabu utaishia kuja kuwa, kama siyo mganga wa kienyeji "sangoma"basi itakuwa ni nabii wa uongo, ama la vyote viwili, na kuendelea kupiga ramli na ubashiri wa hovyo kama huu ili uanze kuuwalia pesa wajinga wenzako.
 
😆😆😆 Mimi naeleza ukweli maana siasa Ni sayansi na CCM imefanya na kutumia sayansi kupata na kujihakikishia ushindi uchaguzi ujao kwa kujibu kero na maswali ya wananchi,kwa kutatua kero na kuwapelekea maendeleo yanayogusa maisha yao
 
Msilete vikwazo kwenye tume huru tuuyamini maneno yako
 
Kama 2020 haukuwa mwepesi, msitegemee wepesi
 
HATA UCHAGUZI WA 2020 MLISEMA NI RAHISI LAKINI MAGUFULI ulikuwa MGUMU KWAKE akaona BORA AUVUGE ILI ATEUE WABUNGE NA MADIWANI badala ya Wananchi
 
CCM IPO madarakani kwa ridhaa ya wananchi ndio maana inaungwa mkono katika Sera na ajenda zake,ndio maana imekuwa ikipigiwa Kura kila uchaguzi ,ndio maana imekuwa ikiendesha serikali kwa utulivu na Amani pasipo mavurugu

Ww endelea kusema ndio maana, ndio maana, ndio maana, siku watu wataingia mtaani akili itawakaa sawa kwani hamna mtoto wa kuwapigia kura mkae madarakani.
 
Ww endelea kusema ndio maana, ndio maana, ndio maana, siku watu wataingia mtaani akili itawakaa sawa kwani hamna mtoto wa kuwapigia kura mkae madarakani.
Kwanini ulijificha uvunguni wakati Lisu amesema uandamane? Si unaona namna watanzania walivyompuuza Lisu na Chadema yenu
 
HATA UCHAGUZI WA 2020 MLISEMA NI RAHISI LAKINI MAGUFULI ulikuwa MGUMU KWAKE akaona BORA AUVUGE ILI ATEUE WABUNGE NA MADIWANI badala ya Wananchi
Sera na ajenda Bora za CCM ndio Ngao ya ushindi wa CCm miaka na chaguzi zote
 
Kwanini ulijificha uvunguni wakati Lisu amesema uandamane? Si unaona namna watanzania walivyompuuza Lisu na Chadema yenu

Magufuli angekaa mbele kutuzuia ili tujue sio muoga, sisi hatuna silaha, tulitaka CCM mkae mbele maana nyie ndio wanasiasa wenzetu mtuzuie.
 
Back
Top Bottom