Mfwatiliaji
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 1,323
- 67
This human cruelty is unacceptable!! Hizi picha ifanyike jitihada waonyeshwe Bush akiwa na Kikwete hapo hapo Arusha. Ndiyo jamaa aelewe kuwa anadeal na msanii na siyo rafiki wa kweli kama alivyofagiliwa.
Watu hawawezi kusulubiwa wakiwa mikononi mwa polisi, unless something is seriously wrong with the system!!
Aluta continua...
Mwnkjj una hakika hapo ni Kibaya (Kiteto)?
I refuse to believe...... may be Eldoret?
Lakini msimamo wa shupavu haubadilishwi kwa kupigwa.
Poleni mliokutwa na masahibu haya - tuko pamoja.
Nini hasa kisa cha kupigwa kiasi icho may I be enlighten manake vipigo ni kama tuko Sobibo ya enzi za Hitler
Hawa jamaa walikuwa kwenye ofisi yao ya Chadema na kikundi chao cha kwaya/nyimbo wakifanya mazoezi (rehearsal) ndipo maPopo wakajitokeza na kuwataka wafuatane nao.. walikowapeleka ni mbingu tu wanajua kwani baada ya kutoka huko hali zao ndiyo hivyo.
siwezi kuamini kwamba hii imetokea Tanzania. huu ndio mwaka wa ushirikiano na vyama vya upinzani kwa kutumia dola kuwanyamazisha. Serikali iunde tume kuchunguza suala hili, au mpaka kutokee vifo ndiyo tume inaundwa kama ile ya Zomba? nielewesheni. tusipoziba ufa tutajenga ukuta kama ule wa Kenya.
Hizi picha ni za kweli maana namuona Msafiri Mtemelwa ambaye anashati na kalamu yaonekana wa kwanza kabisa kashika Mguu . Inasemekana huenda akawa kavunjwa mguu kwa kipigo.Natudia inasemekana huenda akawa amevunja mguu si habari za uhakika . Habari toka Kiteto zinasema Zitto yuko Polisi anafuatilia kujua uhalali wa kundi la watu 30 wanaitwa Komandoo ambao kazi yao ni piga piga na kutishia wananchi mbele ya Msekwa na Polisi lakini hakuna wa kusema lolote .
Bush kaharibu move zote za kisiasa na labda zianze baada ya yeye kuondoka .Mbwembwe hizi zitahojiwa kama hawata deliver na hapa CCM wanajichimbia kaburi . Hivi ni kweli damu ya mtu haina thamani mbele ya mtu kuingia bungeni kwa nguvu ? CCM inafanya mamzuri na wanajiamini kwa nini kutumia nguvu nyingi za namna hii kama wanakubalika ?
Bila ya kujali hao watu wana makosa au hawana makosa, polisi hawana haki ya kupiga raia.
Inatakiwa kuchukua hatua ili polisi waliohusika wachukuliwe hatua.
Hata CCM wenyewe inabidi mujiepushe na ujinga kama hao. Kura zinapatikana kwa nguvu za hoja na wala sio hoja za manguvu.
Lini tutajifunza kuheshimiana na kulindana kama Watanzania hata kama tuna vyama tofauti au tuna imani tofauti?
Bila ya kujali hao watu wana makosa au hawana makosa, polisi hawana haki ya kupiga raia.
Inatakiwa kuchukua hatua ili polisi waliohusika wachukuliwe hatua.
Hata CCM wenyewe inabidi mujiepushe na ujinga kama hao. Kura zinapatikana kwa nguvu za hoja na wala sio hoja za manguvu.
Lini tutajifunza kuheshimiana na kulindana kama Watanzania hata kama tuna vyama tofauti au tuna imani tofauti?