Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Status
Not open for further replies.
This human cruelty is unacceptable!! Hizi picha ifanyike jitihada waonyeshwe Bush akiwa na Kikwete hapo hapo Arusha. Ndiyo jamaa aelewe kuwa anadeal na msanii na siyo rafiki wa kweli kama alivyofagiliwa.

Watu hawawezi kusulubiwa wakiwa mikononi mwa polisi, unless something is seriously wrong with the system!!

Aluta continua...
 
Mzee Mwenzangu,

Wewe ninakuaminia kwa dataz, na ninataka kuamini hizi picha ni za kweli kutoka huko Kiteto, na kwamba chanzo cha hawa wananchi kupigwa ni kiu yao ya demokrasia kwa kusaidia chama chochote cha upinzani kushindana na CCM, na kwamba wamepigwa kwa shinikizo la CCM, basi Tanzania tutakuwa tumefika mbali sana na ccm wanahitaji kutoa maelezo mazito on this ishu,

Bado ninatafuta ukweli zaidi kabla ya kuzisukuma mbele hizi picha.
 
Mwnkjj una hakika hapo ni Kibaya (Kiteto)?
I refuse to believe...... may be Eldoret?
Lakini msimamo wa shupavu haubadilishwi kwa kupigwa.
Poleni mliokutwa na masahibu haya - tuko pamoja.
 
This human cruelty is unacceptable!! Hizi picha ifanyike jitihada waonyeshwe Bush akiwa na Kikwete hapo hapo Arusha. Ndiyo jamaa aelewe kuwa anadeal na msanii na siyo rafiki wa kweli kama alivyofagiliwa.

Watu hawawezi kusulubiwa wakiwa mikononi mwa polisi, unless something is seriously wrong with the system!!

Aluta continua...

mfwatiliaji,

Haya mambo Kichaka anayajua vizuri sana ila kwa sasa hii sio priority yake. Labda vyombo vya habari vinaweza kupewa hizi picha lakini Kichaka sasa hivi yeye yuko kwenye mission yake ya siri na mambo kama haya wala hatajali kabisaaaaa!
 
Jamani ni lini watanganyika watakuwa huru kwenye nchi yao?

Wakati mwingine huwa nafikiri hawa Polisi wanafanya haya sio kwa kutumwa na chama chochote bali kama njia ya kujikomba kwa viongozi wa chama Fulani, Je chama chenye kushika hatamu mliwatuma hawa polisi?

Kama hamjawatuma, je wanafanya kwa maslahi ya nani?

Wana kiteto poleni kwa yote yanayowakuta. Huu ni wasaa pekee wa kuwaondoa hawa wanyonyaji, mafisadi, wezi wa kura, wanyanyasaji, wabakaji wa demokrasia, wasanii, matapeli, wazushi, n.k

Wakati umefika wa kuwaondoa hawa mabaradhuli gumegume na kuweka wapenda maendeleo, demokrasia na ustawi wa jamii na chaguo pekee ni KIMESERA WA CHADEMA

PIGA KURA, Na Mchague KIMESERA

mungu awabariki Kiteto mungu awape siha njema walioumizwa
 
siwezi kuamini kwamba hii imetokea Tanzania. huu ndio mwaka wa ushirikiano na vyama vya upinzani kwa kutumia dola kuwanyamazisha. Serikali iunde tume kuchunguza suala hili, au mpaka kutokee vifo ndiyo tume inaundwa kama ile ya Zomba? nielewesheni. tusipoziba ufa tutajenga ukuta kama ule wa Kenya.
 
Mwnkjj una hakika hapo ni Kibaya (Kiteto)?
I refuse to believe...... may be Eldoret?
Lakini msimamo wa shupavu haubadilishwi kwa kupigwa.
Poleni mliokutwa na masahibu haya - tuko pamoja.

Hiyo ni bongo yenyewe kabisa ambayo watu wamepagawa na hawataki kuacha uchaguzi ufanyike kwa haki (maana hata wakipoteza hili jimbo moja itawapunguzia nini?).

Mambo mengine ni zaidi ya maeelezo ya kawaida ya kibinadamu.
 
Inasikitisha sana kuona kunakuwa na ukiukwaji wa haki za msingi za binadamu namna hiyo katika Tanzania "huru".
Mungu awajalie majeruhi wapone na waendelee na majukumu ya kuijenga nchi yetu.
 
Nini hasa kisa cha kupigwa kiasi icho may I be enlighten manake vipigo ni kama tuko Sobibo ya enzi za Hitler
 
Hawa jamaa walikuwa kwenye ofisi yao ya Chadema na kikundi chao cha kwaya/nyimbo wakifanya mazoezi (rehearsal) ndipo maPopo wakajitokeza na kuwataka wafuatane nao.. walikowapeleka ni mbingu tu wanajua kwani baada ya kutoka huko hali zao ndiyo hivyo.
 
Kama kawaida ya polisi hawa wa bongo wanavyofanya nyakati za uchaguzi. Unaadhibiwa kwanza na kisha unaambiwa makosa yako.. mfano unaambiwa kuwa ulipiga mluzi karibu na ofisi ya serikali (ofisi ya katibu kata) kwa hiyo ulionyesha dharau kwa serikali.
 
Hawa jamaa walikuwa kwenye ofisi yao ya Chadema na kikundi chao cha kwaya/nyimbo wakifanya mazoezi (rehearsal) ndipo maPopo wakajitokeza na kuwataka wafuatane nao.. walikowapeleka ni mbingu tu wanajua kwani baada ya kutoka huko hali zao ndiyo hivyo.

Noma sana!
Inabidi hao maafande washitakiwe kwa utovu wa nidhamu uliopita maelezo.
 
siwezi kuamini kwamba hii imetokea Tanzania. huu ndio mwaka wa ushirikiano na vyama vya upinzani kwa kutumia dola kuwanyamazisha. Serikali iunde tume kuchunguza suala hili, au mpaka kutokee vifo ndiyo tume inaundwa kama ile ya Zomba? nielewesheni. tusipoziba ufa tutajenga ukuta kama ule wa Kenya.

Wao hawafikirii haya mkuu na hivi Kichaka amewapatia mabilioni basi ndio imetoka hivyo for now!
 
Hizi picha ni za kweli maana namuona Msafiri Mtemelwa ambaye anashati na kalamu yaonekana wa kwanza kabisa kashika Mguu . Inasemekana huenda akawa kavunjwa mguu kwa kipigo.Natudia inasemekana huenda akawa amevunja mguu si habari za uhakika . Habari toka Kiteto zinasema Zitto yuko Polisi anafuatilia kujua uhalali wa kundi la watu 30 wanaitwa Komandoo ambao kazi yao ni piga piga na kutishia wananchi mbele ya Msekwa na Polisi lakini hakuna wa kusema lolote .
 
Kweli kabisa Lunyungu,

Habari kutoka Kiteto zinasikitisha sana. Mambo mengi bado hayajafika polisi kuripotiwa au kwenye vyombo vya habari. Inabidi haya mambo yashikiwe bango hapa hadi kieleweke.

Hatutaki kupatiwa mauaji na vurugu zingine hapa east afrika. Tuliyopata miezi miwili iliyopita toka kwa Kibaki na wezi wenzake wa Kenya yanatosha kwa sasa.
 
Bila ya kujali hao watu wana makosa au hawana makosa, polisi hawana haki ya kupiga raia.

Inatakiwa kuchukua hatua ili polisi waliohusika wachukuliwe hatua.

Hata CCM wenyewe inabidi mujiepushe na ujinga kama hao. Kura zinapatikana kwa nguvu za hoja na wala sio hoja za manguvu.

Lini tutajifunza kuheshimiana na kulindana kama Watanzania hata kama tuna vyama tofauti au tuna imani tofauti?
 
Bush kaharibu move zote za kisiasa na labda zianze baada ya yeye kuondoka .Mbwembwe hizi zitahojiwa kama hawata deliver na hapa CCM wanajichimbia kaburi . Hivi ni kweli damu ya mtu haina thamani mbele ya mtu kuingia bungeni kwa nguvu ? CCM inafanya mamzuri na wanajiamini kwa nini kutumia nguvu nyingi za namna hii kama wanakubalika ?
 
Hili ni swali la dola milioni mia sita themanini!
 
Bila ya kujali hao watu wana makosa au hawana makosa, polisi hawana haki ya kupiga raia.

Inatakiwa kuchukua hatua ili polisi waliohusika wachukuliwe hatua.

Hata CCM wenyewe inabidi mujiepushe na ujinga kama hao. Kura zinapatikana kwa nguvu za hoja na wala sio hoja za manguvu.

Lini tutajifunza kuheshimiana na kulindana kama Watanzania hata kama tuna vyama tofauti au tuna imani tofauti?

Mtanzania,

hili ni somo ambalo litachukua miaka kueleweka au labda watu waseme imetosha kama jamaa wa kenya walivyofanya (GOD forbid).
 
Bila ya kujali hao watu wana makosa au hawana makosa, polisi hawana haki ya kupiga raia.

Inatakiwa kuchukua hatua ili polisi waliohusika wachukuliwe hatua.

Hata CCM wenyewe inabidi mujiepushe na ujinga kama hao. Kura zinapatikana kwa nguvu za hoja na wala sio hoja za manguvu.

Lini tutajifunza kuheshimiana na kulindana kama Watanzania hata kama tuna vyama tofauti au tuna imani tofauti?

Mtanzania majuzi nimeongea na kijana mmoja ni Mkwere wa huko Bwagamoyo .Akasema wewe mzee ukisema Serikali means CCM na CCM means Serikali .Sasa haya ndiyo majibu ya issue hii .
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom