Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Status
Not open for further replies.

Kada Mpinzani

Umenilazimisha kurudi kidogo, ingawa nilishaaga kuwahi mkutano na wananchi wengine.

Mtanganyika

Nashukuru kwa maoni yako, mengi ya uliyoyasema na ya kukubali- na nisehemu ya mambo ambayo tulishaanza kuyatekeleza toka 2006; jambo moja ambayo watanzania wanapaswa wafahamu- CHADEMA ya mwaka 2010, haitakuwa kama CHADEMA ya mwaka 2010 kuanzia kwenye organization(grassroot) mpaka policy positioning. Kuna mengi yatafanyika 2008 na 2009, mwaka 2006 ulikuwa mwaka wa mabadiliko ya katiba yetu; mwaka 2007 ulikuwa mwaka wa ku-position hoja za kitaifa za kisiasa na ku pilot program za ujenzi wa chama katika baadhi ya maeneo. Mwaka 2008 ni mwaka wa Ujenzi wa oganizesheni ya chama na pia ni mwaka wa kudai uwanja sawa wa kisiasa. Tutawajulisha thrust and theme ya mwaka 2009 wakati ukikaribia

Kada Mpinzani:

Samahani kama neno heshima limekukwaza, I meant to offence- najua kwa mujibu wa ubinadamu na katiba yetu kila mtu ni mheshimiwa. Nilimaanisha tu Crediantials za Kimesera na Nangoro, Kimesera anakubalika zaidi na ni senior. Kumbuka, inasemakana Kimesera na Mmasai wa kwanza kupata degree upande wa Tanzania, lakini pia kwa muda mrefu amekuwa ni Mwenyekiti wa Wamasai. Sijui kwa sasa. Nilikuwa nasoma kitabu cha Historia ya Sokoine, nikashangaa kumkuta Kimesera kama MC wa tukio lile na baadaye mlezi wa karibu wa familia. Huyu ni mtu ambaye kutofautiana kwake na serikali ya Mwalimu kulitokana na mtizamo wake kuhusu sera za kiuchumi kama ilivyokuwa kwa Mtei. Haya ndiyo mambo yanayofanya nimheshimu na kutamka wazi kwamba kwa crediantials hizi, kumweka yeye kulikuwa to our advantage kuliko mgombea mpya kijana hasa kwa kuwa by elections campaign ni 21 days only- ukiingiza new brand katika jimbo ambayo illeteracy ni 23% tu, athari zake ni nyingi.

Kuhusu Ubungo- sitaki ubishani hapa kuwa nilishinda au sikushinda; nataka utafakari:

Hii ndio hoja ya msingi katika kesi ambayo serikali inaihofia katika malalamiko yangu kuhusu uchaguzi wa Ubungo----------

"Kwa hali iliyodhihirisha wazi kuwa matokeo yalipikwa, waliopiga kura za Ubunge walikuwa 185,684 wakati waliopiga kura za Rais walikuwa 152,525 na hivyo kufanya tofauti ya kura za Ubunge na urais kufikia 33,159. Katika hali ya kawaida na katika uchaguzi uliofanyika kwa wakati mmoja ilikuwa ni vigumu kwa tofauti kubwa ya kura kiasi hiki. Na hata kama wananchi wangekuwa hawapendi kupiga kura za rais kwa kuwa mpiga kura alikuwa akipewa karatasi zote tatu kura hizi zilipaswa kuwepo katika kura zilizoharibika kitu ambacho hakikutokea."

Haya ni baadhi ya mambo mengine ya yaliyomo kwenye kesi/mashtaka ya ubungo ambayo nilifungua mwaka 2006:

Kimsingi, hujuma za kimfumo na kimkakati za chama tawala ndiyo hasa vilivyofanya uchaguzi kutokuwa huru na haki. Kabla ya uchaguzi wajumbe wa nyumba kumi waliandikisha kadi za wapiga kura kwa lengo la kuwakosesha kupiga kura wale walioelekea kupigia kura upinzani na pia kuweza kuwapa rushwa wengine ili kupigia CCM.Wananchi wengi walizuiwa kupiga kura licha ya kuwa na kadi kutokana na ama majina yao kutoonekana kwenye orodha au kuwa tofauti na kwenye daftari. Kulikuwa na kampeni za vitisho kwa wapiga kura hususani katika kata za vijijini. Wananchi wengi walihongwa kukipigia kura chama tawala – hii ni pamoja na wengi kujifanya hawajui kusoma na kuandika ingawa baadhi yao vitambulisho vyao vya kupigia kura vilionekana kuwa na saini. Kulikuwa na mapungufu kadhaa katika mpangilio na idadi ya vituo vya kupigia kura. Halikadhalika, kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa kanuni na sheria katika ujumlishaji wa kura za ubunge. Kwa kiasi kidogo mtandao hafifu wa chama katika maeneo machache na udhaifu wa baadhi ya mawakala navyo vilichangia kushindwa katika vituo vichache ambavyo visingeathiri matokeo kwa kiasi kikubwa kwa ujumla. Na mwisho matokeo ya ubunge jimbo la Ubungo yakatangazwa kwa shuruti bila kutangaza na kujumlisha kwa pamoja matokeo ya kituo hadi kituo hali iliyoashiria kuwa matokeo ya Ubunge yalikuwa na utata. Kutangaza huku kwa nguvu ilikuwa ni mkakati wa kutaka matokeo hayo yasihojiwe kama ilivyokuwa katika matokeo ya urais ambayo yalichelewa kutangazwa kutokana na kukutwa na mapungufu mengi.


Naomba usome with open heart, na uamue mwenyewe moyoni.

Ubarikiwe

JJ
 

asante sana tena sana mnyika kwa kuweka wazi, napenda sana watu wawazi kama wewe !
(1) nimependa hizo sifa za kimesera kama ulivyoanisha hapo juu, knowing that alikuwa mmasai wa kwanza kupata degree na meeengi uliyosema juu ya huyu mzee, inaonyesha kwamba mgombea wa ccm alikuwa anashindana na big candidate kutokana na sifa ulizommwagia, lakini still mgombea wa ccm managed kuibuka mshindi, dont you think kwamba mshindi wa kiteto ambae ni ccm anastahili pia kupongezwa kwa juhudi zake katika kampeni na hatimae kuibuka mshindi baada ya kugombea uongozi na mtu ambae alikuwa ALREADY ESTABLISHED katika hiyo jamii ?

suala la 2 ambalo ni watu sijui kutoandikishwa kupiga kura, je mlifuata hatua gani kabla ya uchaguzi knowing that kuna makosa ambayo yapo in the making ???? THIS IS WHAT I DONT UNDERSTAND, na please dont write the whooooole forum kutujulisha ishu ndogo kama hiyo ya swali nililouliza !
 

Kaka Mtanganyika

1. Hilo la 'to find which eye can get sour and punch it', ni sawa lakini kama nilivyoomba mwanzoni- CCM isilazimishe watu wakafikia siasa za kuchochea wananchi kuasi, hebu jiulize- kama siku ile viongozi wa CHADEMA Komba alipovamia jukwaa, wangeelekezwa apigwe- ingekuwaje? Palikuwa na FFU wengi katika eneo hilo, badala ya kumtoa Komba, walikuwa wanambembeleza, lakini kama CHADEMA wangemshusha kwa nguvu FFU wangegeuka na kuwapiga wanaCHADEMA kama wale polisi wengine walivyofanya kwa viongozi wetu. Hakika siku ile ya kutangazwa matokeo, ni Mbowe ndiye aliyeokoa jahazi- vijana walikuwa wameshaanza kujikusanya, na walikuwa wanaimmba kuwa 'tunataka kufanya kama Kenya"; na kwa kweli ameacha chuki ya vijana dhidi ya viongozi wa CHADEMA kwa kuwazuia kufanya walichotaka

2. I had already taken hid of your call, I will go and get it.

3. I hope you meant trust, because if i restore the 'rust' in you, then there will be no hope for real change.

Halafu you guys are just looking at things- it seems we are all winning and wining- bado nguvu yenu ni ndogo ya kuhamasisha mabadiliko nchini tofauti na uwezo mlionao. Nafurahia sana nguvu yenu katika kupambana na ufisadi. Lakini katika masuala ya mabadiliko ya Katiba, Tume Huru ya Uchaguzi, Sheria, Kujenga oganizesheni ya vyama mbadala- bado mnakuwa kama wanatazamaji wengine tu, mnalalamika na kulaumu tu. As if sisi tuliupinzani ni kikundi fulani cha watu wachache waliozaliwa kuwa wapinzani tu. Hivi upinzani ni nani hasa? Mpaka hapo, watu kama wewe mtakapotoka nje ya box, na kutambua kwamba mpinzani wa kwanza ni wewe mwenyewe mwananchi usiyetaka hali iwe kama ilivyo sasa, tutaendelea kulalama tu milele. I am sorry if I am getting personal, but today I have to say it.

Kama ukiamua say- Nataka by 2009- Sheria X, iwe imebadilika na nitamia uwezo nilionao hata kama niko mbali- basi hayo yatatokea- instead of fire brigading tu. The management by crisis kind of!

Sisi CHADEMA tulishapanga, nini tunafanya lini- bahati mbaya uchaguzi wa Kiteto umekuja ghafla tu hapa kati kati, ndio maana mnadhani haya tunayesema sasa kwa sababu ya kushindwa Kiteto. Lakini rejea tamko la Mwenyekiti wa Taifa kwa wananchi katika mwaka mpya- tulishautangaza mwaka 2008 kuwa ni mwaka wa kudai Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi, na Tulishatangaza kuwa ni mwaka wa Uchaguzi ndani ya Chama- which means ni mwaka wa kusuka upya mtandao wa chama nchi nzima.

Yet you guys are just watching, yet you guys are just giving ushauri, ushauri, and ushauri. Its time for action guys, stop wining!

Get up, and stand up for your right- some people can be fooled for some time, but not all the people all the time( Robert Nesta Marley). The train is on the way...



JJ
 

Kada Mpinzani

katika hatua zote tulikuwa tunawasilisha Tume ya Uchaguzi malalamiko kama sheria inayoelekeza; lakini kada kama wewe unaijua tume yetu!

Mimi ndiye nilikuwa Kaimu Katibu Mkuu kipindi chote cha uchaguzi wakati Dr Slaa na Zitto wako Kiteto- so I signed most of the letters, and I met with Tume also. We were doing it both ways, Msimamizi wa Uchaguzi Kiteto- viongozi wetu wa wilaya walikuwa wakiwasilisha, na taifani tulikuwa tunawasilisha tume makao makuu. At the same time, ili kuhakikisha marekebisho yanafanyika haraka. But the tume, just left things to flow as the way they have been explained in the tamko!

It is sad, but that is Tanzanian democracy- ni jukumu letu wewe na mimi kubadili hali hii, ama sivyo- ipo siku wananchi watachoka kulalamika, na watamweka madarakani kiongozi wanayemtaka- kwa nguvu ya umma!

We are not far from Kenya, I pray that we do not reach up there- kikombe hiki tunaweza kukiepuka, kama tukitaka. Lakini kwanza tuondoe arrogance, na kuwaona wapinzani kama ni watu wa kulalamika tu, na CCM ndio wenye hatimiliki ya utawala katika taifa letu.

JJ
 


John,
I have been following up maelezo yako mara kwa mara nashawishika kwamba huenda umeamua kuwa a full time politician kama vile akina Mzee Kingunge na wengine kama yeye.

Kwa mtazamo wangu mwanasiasa wa hulka kama yako hupenda kuongea mambo yale ambayo anapenda kuyasikia yeye na wale makada wengine wakubwa-wakubwa ili aweze kuaminika zaidi au aweze kulinda nafasi yake katika uongozi wa chama.

Ninachotaka kufahamu kutoka kwako (ili niweze kujua kama wewe hasa ni mwanasiasa mpya au ni walewale) ni kama ifutavyo, je katika harakati za chaguzi mbalimbali kuanzia kuanzia ule uchaguzi mkuu uliopita na hadi uchaguzi mdogo wa jimbo la Kiteto, ni makosa gani ambayo unadhani chama chako kimefanya?

Je, wewe binafsi unayafamu matatizo na vipaumbele vya wananchi wa Kiteto? (Kama uliyafahamu, ni lini uliyafahamu na mlichukua hatua gani kabla ya kufariki kwa Mbunge aliyepita)

Je, unakubali Chadema inahitaji reforms ili kiwe chama chetu sisi wananchi kama vile kilivyo CCM, na sio chama cha kibwanyenye kama kilivyo sasa?

(NB: Mimi sio mwanachama wa chama chochote cha siasa)
 
JM, Tanzania hakuna sheria ya kurun as independent, ndio maana CHADEMA wana watu wengi supporter from outside. Swala ni mmoja tuu, jee kwa nini tunapiga kelele outside of the Arena?

Ni kweli kumake changes we all need to join pamoja, and create strong correlation which will take CCM down. Lakini tatizo ni mmoja tuu, nalo ni policy za CHADEMA, mimi binafsi naamini ya kwamba CHADEMA ndio mpinzani pekee anaitaje CPR ili afufuke, waliobaki their dead.

Kusema kwamba JF hatulii katiba mpya ni wrong, wote humu tunafahamu katiba yetu ina wababysit CCM na kumpa more power Raisi. Lakini kwa kupiga mbiu hapa hatuwezi kubadili katiba, the only way ni kupata wabunge wengi bungeni ambao watapitisha mswada wa mabadiliko ya kikatiba then we will all become winners.

I have to agree ni kweli JF hatujapiga kelele kuhusu tume kikagaragosi ya Uchaguzi, ni kweli tume yetu ya uchaguzi ni Branch la serikali, something which is total wrong.

Mimi nadhni kuna umuhimu wa kikatiba kuwatambua independent candidate kama mimi. Tanzania mbado inawabana raia haki zao za msingi.

I know we need to take action, lakini I as independent i cant have any voice ni lazima nijiunge na chama, na kusema kweli majority ya vyama vinaongozwa kama duka la bibi na babu. That is what am against with it.

Nimependa mabishano haya, i see one thing on you, you have potential and momentum. You need more forces to join you and to gather we will push Tanzania forward.
 

I salute you!
 

I see more independent kama mimi. Labda Pundamilia utueleze why not CHADEMA, CUF au TLP?
 

Pundamilia

I have never planned to be a career politician- take this from me. Kuna miaka ambayo nimejipangia ya kufanya siasa. Maisha ni zaidi ya siasa. Naamini utumishi wangu katika miaka hiyo, utakuwa umetosha kuwapisha wengine ili nao watumikie. Kwa hiyo, kunifananisha na Kingunge aliyekuwa tuyari kusema uwongo kwa sababu tu ni Mwanasiasa ni kunitukana na kuharibu maana nzima ya siasa. Watu kama Kingunge ndio wanafanya siasa kuwa mchezo mchafu. Na kwa kweli, i stand for principle, and certain values I am brought up with. If I will be forced to compromise my values, just because of politics, then I will quit politics in the first place. Naomba uyanukuu haya maneno yangu, uyahifadhi na uyatumie kunihumu nikienda tofauti. Ni muumini mzuri wa maneno ya Mwalimu kwamba ili tuendelee tunahitaji watu, ardhi(ingawa suala la ardhi natofautiana naye kiasi), siasa safi na uongozi bora!

Maneno yako yananifanya niamue kutokujibu maswali yako kwa kina kwa kuwa naisoma dhamira yako katika maneno yako. Kitendo cha kutamka kwamba CCM ni chama cha watu na pia umenihukumu tayari kuhusu hulka yangu ya kisiasa.

That said- Majibu kwa Maswali yako

1. Kosa la CHADEMA ni kuruhusu CCM kuiba uchaguzi- kwa kutoshinikiza kwa nguvu zote mapema sana mabadiliko ya mwenendo wetu wa uchaguzi. Lengo la 2008 tuliojiwekea ni mbali, shinikizo lingepaswa lianze kwa nguvu zote toka mwaka 2006. Pia uchaguzi wa ndani ya chama tulipaswa kuufanya toka mwaka 2007 ili kuwa na miaka mingi zaidi ya kuwaridhisha wakina Tomaso kabla ya mwaka 2010. Lakini kwa ujumla, mwelekeo tunaokwenda ni sahihi, na makosa hayo madogo, yanaweza kurekebishika 2008 mpaka 2010. Kosa lingine, ni kushindwa kuwafanya wananchi wachangie hizi harakati zetu kila mahali, kuna baadhi ya watu pamoja na kuwa wanapenda upinzani- lakini wanaona kuwa kama si wajibu wao kuufanya upinzani ushamiri. Wanaona kama ni wajibu wa viongozi wa upinzani wenyewe. Changamoto kwetu ni kufanya wote tuwe kwenye same page

2. Kuhusu Kiteto, mimi sio mkazi wa Kiteto- lakini jua kwamba CHADEMA tuna diwani kwenye kata ya mjini kabisa Kibaya, diwani wetu kule amewatumikia wananchi vizuri toka 2005 ndio maana tunakubalika. Kimesera wakati wote amekuwa mstari wa mbele kuwatetea wanaKiteto hata baada ya kushindwa ubunge. Rejea sakata la wakulima ambalo hata LHRC ilijitokeza kulifuatilia.

3. CHADEMA inahitaji reforms, hilo nakubali. We always strive to be better, and if we get there we will strive to be the best, ndio maana tumeshaanza reforms toka 2006. Soma thread ya CHADEMA must reform nimeeleza utekelezaji. Lakini sikubaliane tujireform kuwa kama CCM, umesema CHADEMA ni chama cha mabwanyeye na kwamba CCM ni chama cha watu- lakini ukweli ni kuwa CHADEMA ni chama cha demokrasia na maendeleo-utawala watu, lakini CCM ya leo si sawa na CCM ya Nyerere- CCM ya leo ni Chama Cha Mabwanyeye kama nitatumia neno lako mwenyewe

Karibu ujiunge na CHADEMA, tembelea www.chadema.net kwa maelezo zaidi

JJ
 

Ahsante kwa kunipa cheo cha utaalam.

Hayo ya hapo juu yana confirm usemi wangu kuhusu helikopta kuwa ni chombo kilichofikirika na chadema kuwa kinaweza kuleta ushindi wa kura.


Viongozi gani wa CHADEMA hao ambao bado ni system? Au ni mkakati mwingine wa kuwatia hofu wananchi wasiwaamini viongozi wao?-Wagawe uwatawale.
Wa kwanza Mbowe, anajulikana na amesha tajwa sana kuwa ni system, wengine siwajui nikipata data ntakufahamisha.


Whatever you did was not good enough, ndio maana mkashindwa na matokeo mkasaini kuwa ni sawa, au bado hamjasaini?


Hayo juu ndio yale niliyosema "tunangoja ushahidi", unakijuwa kisa cha tunangoja ushahidi? Kama hukijuwi ngoja nikudokeze kwa kifupi: Kuna mtu alikuwa kalala, kuna muhuni mmoja akaona nimepata mdondo, akamnyatia akamvua suruali, akamvua chupi, akamgeuza, akampaka mate, akambandika, akamaliza. baada ya hapo jamaa alielala akamkamata yule aliefanya na kumaliza, akamshitaki. Kufika mahakamani Hakimu akawa anamuuliza, wewe kavua suruali alikuwa umelala tu? jamaa akajibu hapana nilistuka lakini nilikuwa nangoja nione atafanya nini. Kakuvua chupi, kakugeuza, kakuingiza, yote ulikuwa unafanya nini na ulishastuka? Akajibu alikuwa anangoja apate ushahidi.

Nadhani umeelewa nimejaribu kukifanya hichi kiwe ashaakum. Ndio hayo? tulikuwa tunangoja ushahidi?


Mengine yote uliyosema ni irrelevant.
 


Kaka

Wewe ni kati ya wale mnaogopa vyama vya siasa kama ukoma!

1. Katiba na Sheria haviruhusu mgombea binafsi, lakini Mahakama ilishaelekeza kupitia hukumu ya Mtikila kwamba serikali ifanye mabadiliko. Binafsi naunga mkono uwepo wa mgombea binafsi, lakini naunga mkono pia uwepo wa vyama thabiti vya siasa. Kwa kuwa wewe ni independent, ombi langu kwako- Sukuma ajenda ya serikali kutekeleza maamuzi haya ya Mahakama. Sukuma pia Tanzania iwe na mfumo kamili wa mchanyato- uwakilishi wa uwioano(PR) na FPTP/Winner takes all.

2. Avoid generalization, si vyama vyote vya siasa ni sawa. Treat vyama case by case. Na wenye wajibu wa kutengeneza mfumo wa chama ni wanachama, sasa kama watu kama wewe wanaona kuwa na kadi ya chama cha upinzani ni kama kuwa na passport ya kikagaidi; je tutafika?

JJ
 

I think mfano ulitumia sio irrelevant na topic. So, please try to be more professional sababu, we have different people from defferent places visits here. So, i advise you not to use such of words, because at the end of the day tutaonekana kama bunch of thugs.
 

Tukubsli ukweli, kuwa haiwezekani kila siku kushindwa halafu tunangoja kutowa sababu. Zozote zile ziwazo.

Simply, kama kuna uonevu haina haja ya kufanya chochote ni kukataa kuingia kwenye mchakato wa kupiga kura mpaka hapo tutapoona kuwa sababu zitazojitokeza hazitojitokeza.
 

JM mimi sijasema upinzani ni UKOMA. Nimesema kama wewe ulivyo na values and credentials zako concern politics, that is the samething i have. I have my own rules and values kuhusu siasa. CHADEMA and I differ in policy and organization management chart. I declared that for years that i don't belive Hon. Mbowe is a good Organization leader. I dont agree with him in many things, i differ with him in policy and management issues.

I believe movement start from bottom goes up, i believe grassroot politics is the way. I do believe your house management will reflect your principle and values. From that perceptives then i see problems with CHADEMA, i want them first to clean inside and I believe many will join the forces and to gather will move Tanzania forward.
 

I believe the same thing. What i don't agree na wewe ni kutumia mfano wa matusi pale juu. I guess kuna mifano mingi zaidi unaweza kutumia, na mfano wa kumvua nguo sijui kumfanya nini doesn't prove your point, lather it shows your weakness toward creation of strong argumented points.
 

Ahsante kwa kunijuza hilo, mwenye kufahamu atafahamu nimesema nini na nimesema hayo kwa makusudi kabisa na sidhani kama hayo ni matusi kwani kwa kwetu Dar Es Salaam, husema "Ashaakum si matusi".
 
 
I see more independent kama mimi. Labda Pundamilia utueleze why not CHADEMA, CUF au TLP?

Nadhani nafasi hii ya kuwa free from Chama cha siasa ndiyo nzuri kwani hainizibi mdomo wa kuongea, sitapenda kuwa katika mifumo ya siasa za kunifanya niseme hatuna matatizo kwenye uongozi wetu il-hali kumeoza.
 
 
Mnyika

Naona unaingia kwenye tundu la sindano ambalo watu wamekutegea. Jitahidi kutokujibu na kutolea maelezo kila kitu.

kumbuka hapa kuna wenye nia njema na wasio na nia njema kwako na kwa chadema. Kwa hiyo watapenda kujua unafanya au mnafanya nini ili nao wabuni njia za kukinzana nanyi. Usimpe nafasi mshindani wako kujua una silaha gani na unataka kufanya nini.

nitamsg jioni.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…