Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Status
Not open for further replies.
Kazi kwelikweli . . . . bado safari ndefu. I wish alilowahi kusema Nyerere lingetekelezeka . . . . Alipenda kuona Tanzania ikiwa na vyama vikubwa vya siasa kuleta upinzani wa kweli.

Somebody need to bring the opposition together to bring serious opposition.
 
wapinzani bado si wanasiasa tunataka tuwape darasa la kuwa waangalizi ili wajifunze siasa na wapunguze haya maneno ya kifedhuli

Hao wanasiasa wanaoijua siasa wamewafanyia nini Watanzania kama siyo kuwaongezea ugumu wa maisha wakati wenyewe wakiendelea kuwa matajiri wa kupindukia!?
 
Tunawapongeza CCM, maana hii ndio namna nzuri ya kujenga demokrasia! Aliyeshinda apongezwe na ambaye kura hazikutosha afanye mipango ili kwenye uchaguzi unaofuata kura zitoshe...

Kwa maana nyingine, mimi napenda hiki kiswahili cha JK kinapunguza munkari sana... badala ya kushindwa tuseme (kura hazijatosha)

Mimi nina swali; Je wapinzani wangeungana CCM bado ingeshinda? Maana hii ndio imekuwa weekness ya upinzani kwa muda sasa?
 
Nakubaliana na wewe Kamanda na moja ya mikakati mibovu ni kwa Chadema ku hijjack the whole campaign na kuwa ya Ki-chadema zaidi badala ya umoja wa wapinzani.

Niliwahi kuta hadharisha kuhusu hili mwanzoni mwa thread hii, tumeshuhudia ubinafsi mkubwa wa wanachadema na matokeo yake ule ushirikiano wa vyama umekuwa hauna maana yeyote.

Kabla hamjaanza na ule utaratibu wenu wa kawaida wa kudai mmeibiwa kura, vitisho, sumu nk kwanza safisheni nyumba yenu ni chafu mno.

..ccm na chadema wote ni watanzania,hawatofautiani sana.

..tafauti waliyonayo ni kuwa ccm ni babu,chadema mjukuu[mmoja mzoefu wa muda mrefu,mwingine ndio anajifunza]
 
Chadema wanapaswa kuondokana na upuuzi wa kudhani kuwaonyesha wananchi 'helikopta' ndio mvuto mkubwa wananchi wawape kura. If anything, this in itself should be reason enough to vote against them.

Nakubaliana na mawazo ya Mkjj. Kila uchaguzi unategemea umejipanga vipi, na ni mikakati ipi umeiweka kufanikisha azma yako ya uchaguzi. Je, unawajua vizuri wapiga kura wako? Unayajua vizuri mahitaji yao?

Huwezi kwenda tu kuomba kura kwa kelele za jukwaani. Mgombea wa Chadema alishagalagazwa mara kadhaa katika jimbo hilo hilo. Je, kabla ya kumteua tena kugombea mara nyingine, walijiuliza ni sababu zipi zilizokuwa zinamfanya ashindwe; na kama walizijua, ni yapi waliyokuwa wameyafanya safari hii ili aweze kukubalika zaidi!

Chadema, kama chama inawabidi pia wakae chini ili wajitazame upya. Their top leadership may not be inspiring enough to the wananchi.
 
Kiteto: Chadema ni kilio

2008-02-25 17:10:50
Na Simon Mhina, Kiteto

Simanzi imewakumba wanachama na mashabiki wa chama cha upinzani cha CHADEMA wilayani hapa, baada ya kibao kugeuka ghafla na matokeo ya uchaguzi kuonyesha mgombea wa ubunge wa chama hicho, Bwana Victor Kimeseara, amepigwa bao na yule wa CCM, Bwana Benedict Nangoro.

Kwa mujibu wa matokeo hayo yaliyopatikana kutoka katika maeneo tofauti jimboni humo, hadi kufikia asubuhi ya leo, mgombea wa CCM alikuwa akipeta kwa kuzoa kura zinazotajwa kufikia 14,000, dhidi ya kura 13,000 za mgombea wa CHADEMA.

Taarifa hizo zilizothibitishwa na baadhi ya viongozi wa CHADEMA zimedai kuwa, matokeo hayo ni ya kata zote isipokuwa moja ya Krash, ambayo iko mpakani mwa wilaya hiyo na Handeni.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, kiongozi mmoja wa CHADEMA amesema hata kama watazoa kura nyingi katika kata hiyo ya Krash, bado hawataweza tena kumpiku mgombea wa CCM, kutokana na ukweli kuwa kura zilizopo hazifiki 1,000.

``Tumeanguka... hicho ndicho ninachoweza kusema,`` amesema kiongozi mmoja wa CHADEMA wakati akizungumza na Alasiri leo asubuhi
.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bw. Zitto Kabwe, amekiri kushindwa kwa chama chake, lakini akatilia mashaka juu ya daftari la kudumu la wapiga kura.

Zitto ametilia mashaka daftari hilo kutokana na madai kuwa watu wengi hawakupata haki yao ya kupiga kura na hivyo kuhisi kuwa kuna hujuma imefanyika.

Hadi wakati tukienda mitamboni, matokeo rasmi ya uchaguizi huo yalikuwa bado hayajatangazwa.

Maeneo ya mengi ya mjini Kiteto yalikuwa kimya leo hii baada ya habari za kushindwa kwa mgombea wa CHADEMA kujulikana.

Matokeo ya vituo mbalimbali mjini Kiteto yameonyesha kuwa mgombea wa CHADEMA ndiye aliyeibuka kidedea baada ya kujizolea kura nyingi dhidi ya mpinzani wake.

Aidha, utulivu huo umeelezwa kuwa umechangiwa vilevile na taarifa zilizokuwa zikienezwa na baadhi ya makada wa CCM, waliokuwa wakizunguka kwenye majumba ya watu wao na kuwapa taarifa njema za ushindi, huku wakiwasihi kutulizana badala ya kushangilia mitaani, lengo ikiwa ni kuepuka kuzuka kwa fujo.

Katika hatua nyingine, imeelezwa kuwa kuharibika kwa helikopta ya CHADEMA katika siku ya mwisho ya kampeni, kumechangia kwa kiasi fulani, kushindwa kwa mgombea wao.
Jumamosi, helikopta iliyokuwa ikitumiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA.

Bw. Freeman Mbowe na mgombea wao, Victor Kimesera iliharibika mjini Dodoma na kuwafanya washindwe kuitumia katika kuwakusanya watu wao maeneo ya vijijini kama ilivyotazamiwa.

``Sio siri, lile dege lilikuwa likisaidia sana katika kuwakusanya watu mikutanoni na kuwaelezea sera za mgombea wa CHADEMA... nadhani waliwakosa baadhi ya watu pale lilipoharibika na matokeo yake CCM wakapata mwanya wa kutumia helikopta yao katika kuwawezesha kushinda,`` akasema mwananchi mmoja wa mjini Kiteto, aliyejitaja kwa jina la Alphonce Ernest.

SOURCE: Alasiri
 
Kazi kweli kweli. Hivi Tanzania utamaduni wa Opinion Polls vipi? Maana nilichokuwa nasikia kabla ya upigaji kura ni mchuano mkali kati ya CCM na Chadema. That was it.

Redet, are you sleeping? Najua baadhi ya wahusika wenu wapo humu humu.
 
Angalia namba kwenye KLH News.. halafu mchambue..

Kaka Mzee MwanaKijiji nimeona mkuu!!! lakini nakuona umenyong'onyea sana mzee wangu, pole mkuu, as if umefukuzwa uwaziri mkuu kwi kwi kwi, naona umeonja yale mtani wako aliyoyapata hivi karibuni!!!

Jifunze kupokea matokeo yote... Siamini leo hii unatuambia tuchambue sisi wenyewe... Wakati wewe ni mchambuzi wetu mahiri...

Pole mkuu!!! kama unapata kinywaji please go and take some bottles!!!
 
Ama kweli mwanakijiji leo kachanganyikiwa amefikia kutoa Thanks na lile jina lake la "mwafrika wa kike" ambapo mjadala huu halijachangia kitu. teh teh teh teh
 
Tunamsubiri Mtani wake "Mtu wa Pwani" Mh, "John Mnyika" kwa jina lingine "JJ" kuja na sababu za kura za (CHADEMA + SAU +TPP) kutotosha.

Haya ndio miongoni mwa hoja zake atakazoleta:-
1. Taftari la Kudumu
2. Kura zimeibiwa
3. Watu wengi walipoteza kadi za kura.
4. Muda wa kampeni ulikuwa mdogo
5. Helkopta yetu iliharibika siku za mwisho.
6. Msimamizi wa Uchaguzi alikuwa DED (ambaye huchaguliwa) na serikali ya CCM.

Lakini ni muhimu, tuache kufanya mambo kwa crisis kama serikali ya CCM, tuone basi strategy wandugu...
Ukifuatilia kwa makini sana viongozi wengi wa Upinzani ni wana CCM, yaani wanaisaidia sana CCM kujirekebisha eventually inaendelea kuonekana inabadilika na wakati... tena kwa sasa hivi ni vibaya zaidi maana wana mwenyekiti ambaye anaangalia upepo unavuma vipi.
 
Watu hapa tutatafuta wachawi wee,lakini ukweli ni kuwa wananchi wa Tanzania ni fools(people lacking good sense and good judgement) They deserve what they are getting because they choose to have that.
Wako tayari kutoandamana kuishinikiza serikali kuwachukulia hatua Maafisadi lakini wako tayari kwenda kuandamana kumpokea Lowassa. Tanzanians are cheap like a bunch of groundnuts.We are easly bought therefore we are cheaply treated.

Yaani hapa Nyangumi nakubaliana nawe 100%. Ngoja niendelee kufuatilia kampeni za Seneta wetu Barack Obama. Ukiendelea kufuatilia Siasa za Bongo kichwa kitakuuma tu kutokana na Watanzania wengi kuwa bado kwenye usingizi mzito wa uzembe.
 
2008-02-25 17:10:50
Na Simon Mhina, Kiteto

Simanzi imewakumba wanachama na mashabiki wa chama cha upinzani cha CHADEMA wilayani hapa, baada ya kibao kugeuka ghafla na matokeo ya uchaguzi kuonyesha mgombea wa ubunge wa chama hicho, Bwana Victor Kimeseara, amepigwa bao na yule wa CCM, Bwana Benedict Nangoro.

Kwa mujibu wa matokeo hayo yaliyopatikana kutoka katika maeneo tofauti jimboni humo, hadi kufikia asubuhi ya leo, mgombea wa CCM alikuwa akipeta kwa kuzoa kura zinazotajwa kufikia 14,000, dhidi ya kura 13,000 za mgombea wa CHADEMA.

Taarifa hizo zilizothibitishwa na baadhi ya viongozi wa CHADEMA zimedai kuwa, matokeo hayo ni ya kata zote isipokuwa moja ya Krash, ambayo iko mpakani mwa wilaya hiyo na Handeni.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, kiongozi mmoja wa CHADEMA amesema hata kama watazoa kura nyingi katika kata hiyo ya Krash, bado hawataweza tena kumpiku mgombea wa CCM, kutokana na ukweli kuwa kura zilizopo hazifiki 1,000.

``Tumeanguka... hicho ndicho ninachoweza kusema,`` amesema kiongozi mmoja wa CHADEMA wakati akizungumza na Alasiri leo asubuhi.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bw. Zitto Kabwe, amekiri kushindwa kwa chama chake, lakini akatilia mashaka juu ya daftari la kudumu la wapiga kura.

Zitto ametilia mashaka daftari hilo kutokana na madai kuwa watu wengi hawakupata haki yao ya kupiga kura na hivyo kuhisi kuwa kuna hujuma imefanyika.

Hadi wakati tukienda mitamboni, matokeo rasmi ya uchaguizi huo yalikuwa bado hayajatangazwa.

Maeneo ya mengi ya mjini Kiteto yalikuwa kimya leo hii baada ya habari za kushindwa kwa mgombea wa CHADEMA kujulikana.

Matokeo ya vituo mbalimbali mjini Kiteto yameonyesha kuwa mgombea wa CHADEMA ndiye aliyeibuka kidedea baada ya kujizolea kura nyingi dhidi ya mpinzani wake.

Aidha, utulivu huo umeelezwa kuwa umechangiwa vilevile na taarifa zilizokuwa zikienezwa na baadhi ya makada wa CCM, waliokuwa wakizunguka kwenye majumba ya watu wao na kuwapa taarifa njema za ushindi, huku wakiwasihi kutulizana badala ya kushangilia mitaani, lengo ikiwa ni kuepuka kuzuka kwa fujo.

Katika hatua nyingine, imeelezwa kuwa kuharibika kwa helikopta ya CHADEMA katika siku ya mwisho ya kampeni, kumechangia kwa kiasi fulani, kushindwa kwa mgombea wao.
Jumamosi, helikopta iliyokuwa ikitumiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA.

Bw. Freeman Mbowe na mgombea wao, Victor Kimesera iliharibika mjini Dodoma na kuwafanya washindwe kuitumia katika kuwakusanya watu wao maeneo ya vijijini kama ilivyotazamiwa.

``Sio siri, lile dege lilikuwa likisaidia sana katika kuwakusanya watu mikutanoni na kuwaelezea sera za mgombea wa CHADEMA... nadhani waliwakosa baadhi ya watu pale lilipoharibika na matokeo yake CCM wakapata mwanya wa kutumia helikopta yao katika kuwawezesha kushinda,`` akasema mwananchi mmoja wa mjini Kiteto, aliyejitaja kwa jina la Alphonce Ernest.
SOURCE: Alasiri
 
Yaani hapa Nyangumi nakubaliana nawe 100%. Ngoja niendelee kufuatilia kampeni za Seneta wetu Barack Obama. Ukiendelea kufuatilia Siasa za Bongo kichwa kitakuuma tu kutokana na Watanzania wengi kuwa bado kwenye usingizi mzito wa uzembe.

Sijui watakuja kumlaumu nani .Msekwa na Makamba walihama Jiji wakaishia huko ? Hivi ni kweli CCM wanaweza kutumia nguvu kubwa namna hii kwa jimbo moja tu ?
 
Unajua Mwanakiji Kuna Watu Tunao Humu Jf Lkn Akili Zao Zimeshikwa Na Mafisadi,sasa Nyie Mnaona Raha Gani Ccm Kushinda?halafu Miongoni Mwa Hao Wanaoshangilia Huo Ushindi Hata Kadi Ya Ccm Hana Sasa Si Aibu Hh,au Ndio Mnafikiri Wote Walio Hapa Jf Ni Wapinzani Wa Ccm?tuliowengi Si Wana Ccm Wala Wa Pinzani Wa Ccm,ss Tunataka Kuona Maendeleo Yanapatikana Huko Bongo.kwa Maana Nyingine Tunataka Habari Zinazowachomoa Mafisadi Katika Mashimo Yao .
 
Ama kweli mwanakijiji leo kachanganyikiwa amefikia kutoa Thanks na lile jina lake la "mwafrika wa kike" ambapo mjadala huu halijachangia kitu. teh teh teh teh

Unajua wapinzani hawana sera hichi kibano wakizoee mpaka siku ile watakapobadirika na sera zao.
watu hatuoni kwanini wapewe CHADEMA/CUF/NCCR ambao hawafahamiki namna ya uendeshaji wao.

Maana kimantiki wapinzani hawatofautiani na CCM sasa basi kwanini ufanye majaribio ???

Mie naona udhaifu wa wapinzani ni huu mtindo wao eti kuibua uozo wa mwazako na kuufanya SERA,kuibua uozo ni vyema lakini kuufanya ndio mgongo wa kupandia ni makosa makubwa ,hii naifananisha kama mtu yule anayemtaka mwanamke kwa gia za kumuambia maovu ya mwanaume aliyenaye.Mwanaumme aliyenaye anaweza akawa muovu sana lakini wewe kupitia mgongo huo ili ufanikishe adhima yako na kama mwanamke huyo ni makini hakika hutompata.

Wapinzani kama wapo tofauti na CCM hawakuhitaji kuruka na ndege angani kupoteza fedha nyingi kwa kutangaza sera za maneno ,bali sera zao zingejitangaza zenyewe kwa kufanya hivi-

Wapinzani nendeni huko kijijini mnakoruka na madege wakati tu wa uchaguzi kafanyeni harambee/tafuteni wadhamini wapelekeni huduma ya maji,umeme.

wapinzani nendeni huko mkahamasishe watu muwaelimishe jinsi ya kufanya kilimo cha kipande kidogo na kuvuna mavuno yenye tija.

wapinzani kahamasisheni huko vijijini kwa miharambee/wadhamini watu wapate muamko wa kilimo cha kutumia matrekta.

wapinzani hamasisheni wananchi/wadhamini kujengea vyuo vikuu vingi nchini ili wananchi wapate kuelimika.
Hakika mkijitahidi hata kwa nusu ya hayo mtapata kura nyingi za tsunami ambazo hata wezi wa kura wataona aibu yenyewe na mtazipata bila jitihada zozote za kuruka na ndege angani .

Mnavyofanya saizi hamna tofauti na CCM ndio maana hatuna sababu ya kuwapa kura.
 
kuna kitu ambacho hukielewi katika siasa. Tatizo la watanzania wengi wanachagua chama wala si sera. Sisemi kama wapinzani ni bora, au CCM ni bora zaidi bali ni jambo la kujiuliza huo ushindi wa CCM kiteto hutaleta maendeleo gani? Je naweza pata jibu (quantify jibu lako). Nafikiri kabla ya kushangilia huo ushindi basi vinjari wilaya ya kiteto, kisha kwa dhati kabisa usimame kushangilia huo ushindi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom