Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nilitarajia kura kuharibika 6-10 na imekuwa hivyo.
Kuharibika kura kwa hawa jamaa hakumaanishi kutokuwa na elimu ya uraia... HAPANA, kuna zaidi ya hivyo
Hommie sasa tumekwisha.....ngoja nikatulize stress kule kwa mama Big..:bowl:Anaapa sasa....kuwa mwaminifu kwa jamhuri ya Muungano wa tanzania (hivi ule uaminifu mwengine wanaapiaga wapi)
Sasa nimejua ukweli kuhusu bandiko hili la Dr Slaa jana.Mbona wapinzani wanatuangusha, wapo zaidi ya 80 lakini mbona Marando amepata 53? Du kweli Tanzania tuna safari ndefu kufikia mabadiliko ya kweli.
Originally Posted by Dr.W.Slaa![]()
![]()
Kanyagio,
Thanks. Napenda tu kusema kuwa kushirikiana ni maridhiano ya pande husika. Upande mmoja hata ungelitamani kiasi gani, mashirikiano hayatawezekana iwapo upande wa pili hautaki, au kama malengo na ajenda zinatofautiana. Wengi tunajadiliana, lakini kwa bahati mbaya details nyingi hamzifahamu, na hatua ambazo Chadema tumekwisha kuchukua kuwaomba wenzetu wakubali kushirikiana nao. Kwa Taarifa yenu, CUF imetuandikia barua kuiunga mkono Chadema kwa suala la Uspika. Taarifa zisizorasmi zinazotufikia sasa ni kuwa Wabunge wa CUF wamaelekezwa kutoka Zanzibar kuwa Wasiingue mkono Chadema. Yetu macho tutazame nini kitatokea katika upigaji kura wa Uspika. Hapo ndipo tutajua ukweli wote. Ni imani yangu kuwa CUF watashikilia msimamo wao ambao uko kwa Maandishi kuwa wataunga mkono mgombea wa Chadema wa Uspika. Maslahi ya Taifa letu ni makubwa zaidi kuliko maslahi ya vyama vyetu au yetu binafsi. Ni pale tutakapotambua ukweli huo na kuuweka kwenye matendo yetu, ushabiki wa vyama pekee hauwezi kupeleka Taifa hili mbele. Kama yanayosemwa ni kweli kuhusu ufisadi kubwa katika kumweka "Spika" kwa upande wa CCM, basi Taifa linazidi kuporomoka. Tusipende ushabiki zaidi, bali tufanye utafiti kwa kila jambo na tutajua ukweli umesimama wapi.
Jana usiku niliambiwa na impeccable source kwamba MAALIM SEIF SHARRIF HAMAD alitoa maelekezo maalum kwa wabunge wa CUF kumpigia kura mgombea wa CCM. Kwa hesabu hii ya kura naamini ndicho kilichotokea. Hii maana yake ni kwamba chama pekee cha upinzani kilichobaki ni CHADEMA. Tuungane tuijenge CHADEMA ili iwe mkombozi wa kweli wa Watanzania. To hell with CUF, to hell with HAMAD, the hyprocrite!
Kura 327 zinahesabiwa kwa saa moja. kulikuwa na nini?
Hapa nina hasira sana...
CHADEMA ina wabunge 56. Marando amepata kura 53. Whats going on? CCM wote, Wapinzani wengine wote na baadhi ya CHADEMA wameunga mkono mgombea wa CCM. This can tell what to expect in the next 5 years.
Jamani hawa jamaa wa CUF yaani wamegoma kabisa kumpa kura Marando?? Kweli nimeamini wao nao ni kama Lyatonga Mrema (watoto wa CCM kwa nyumba ndogo). Sasa wale washikaji wetu MAFISADI mambo lainiiii.
CCM kuna ushabiki wa ajabu sanaaa, ina maana hata Chenge angepitishwa na CC ya CCM wabunge wangempitisha kuwa Spika?
namuonea huruma huyo mama..! USILIE LAKINI...!
manake hachelewi kusema wananionea kwa sababu mm ni BINTI
Yaani hata ndani ya chadema wanatosana wenyewe kwa wenyewe!!!