Uchaguzi wa TLS 2024: Boniface Mwabukusi ashinda Urais, apata kura 1274
Kuna jamaa yangu ni wakili, jana tulikuwa pamoja ila leo ameniambia ameenda Dodoma, kuna deal ameipata ameenda kuifanya then anarudi kesho 🤔🤔

Nikamuuliza ni dili gani, akasema tu anaenda kwenye uchaguzi wa TLS. Kama una D mbili umeshaelewa vyema maana ya neno “DILI”
 
Wakuu,

UPDATE saa Saba Mchana: TLS waomba radhi kupitia ukurasa wao wa X baada ya kupost kuwa zoezi la upigaji kura limeisha wakati mawakili wakiwa wanasubiri karatasi za kupigia kura ziongezwe.

Kusoma zaidi kuhusu taarifa hii soma hapa: TLS waomba radhi kwa post yao waliyoweka mtandao wa X kuhusu zoezi la kupiga Uchaguzi wa Rais TLS kumalizika

======

UPDATE saa 12:17 PM: Ukurasa wa X wa TLS wamepost kuwa uchaguzi umeisha, lakini upande mwingine taarifa ni kuwa karatasi bado zinazubiriwa kuongezwa ili zoezi la kupiga kura liendelee kwa wale ambao bado hawajapiga kura.

Zaidi kuhusu taarifa hii soma hapa: Ukurasa wa TLS X umesema zoezi la kupiga kura limeisha, upande mwingine wanasema wanasubiri karatasi za kupiga kura ziongezwe, ukweli ni upi?

===

UPDATE majira ya saa tano asubuhi: Zoezi la kupiga kura limesimama baada ya karatasi kuisha, mawakili wanasubiri karatazi ziletwe ili zoezi liendelee.

Zaidi kuhusu hili soma hapa: Uchaguzi wa Rais TLS: Karatasi za kupigia kura zimeisha, mawakili wanasubiri karatasi nyingine ziletwe ili zoezi liendelee

====

Leo ndio leo, ni kivumbi na kijasho, hatma ya Urais TLS kugundulika leo.

Uchaguzi wa Rais wa TLS uliokuwa unasubiriwa kwa hamu, kufanyika leo Agosti 2, 2024. Je nani ataibuka mshindi kati ya wagombea hawa sita?


Kama ulikosa mdahalo wa wagombea hawa pita hapa Mdahalo wa Wagombea Urais Chama cha Mawakili Tanzania Bara (TLS) mwaka 2024

1. Capt. Ibrahim Mbiu Bendera
2. Paul Revocatus Kaunda
3. Sweetbert Mkuba
4. Boniface Mwabukusi
5. Emmanuel Agustino Muga
6. Revocutus Lubigili Kibwe

Kwa kufatilia kwangu naona upinzani mkubwa upo kati ya
Sweetbert Mkuba na Boniface Mwabukusi.

Je, unadhani mshindi atatoka kati ya hawa wawili au tutapata mshangao wa kufunga mwaka kwa asiyetarajiwa kabisa kuibuka mshindi?

Usikae mbali na uzi huu kupata updates zote za yanayoendelea kwenye uchaguzi huu.
Hatutaki chawa na kunguni wa system
 
Back
Top Bottom