Uchaguzi Wa Viongozi Wa CCM Wateka Anga la Siasa za Tanzania, CHADEMA yashikwa Mateka

Uchaguzi Wa Viongozi Wa CCM Wateka Anga la Siasa za Tanzania, CHADEMA yashikwa Mateka

Tumaini kwa richmod, escrow, kagoda, radar ya ndege, EPA etc. Mikopo kila siku lakini maji na umeme unategemea kudra za mvua.
Kwani hujaona mh Rais wetu mpendwa mama Samia akizindua mitambo mikubwa ya kuchimba visima virefu vya maji vitakavyo saidia kuondoa tatizo la maji?
 
Nimeuliza hapo juu mkuu kuwa mamilioni ya Ruzuku kuanzia 2015-2020 yalikwenda wapi? Vipi kuhusu 2010-2015 pesa za Ruzuku zilikwenda wapi? Mbona hata rangi tu katika ofisi imekuwa shida kupaka na kuboresha? Vipi pesa za akina Sabodo? Vipi pesa za join the chain? Unafahamu zikikusanywa shilingi ngapi? Unafahamu zipo kwa Nani? Vipi pesa za michango ya wabunge wa chadema ya miaka husika? Zipo wapi?

Unajua kwa mwezi chadema ilikuwa inapokea ruzuku shilingi ngapi?. Ukijua chukua mapato na matumizi kwa mwezi ndio utaona ulivyo kilaza wa kudandia mambo Wala huyajui.
 
Ndugu zangu CCM imeonesha umwamba wake wa siasa za hapa Tanzania,imeonesha kuwa ndio chama kikubwa na chenye ushawishi hapa Tanzania, imeonesha namna CCM ilivyo na nguvu hapa nchini, Imeonesha misuli yake ya kisiasa, imeonesha namna kinavyokubalika na kupendwa na watanzania,imeonesha namna ambavyo Ni ngumu kuizuia CCM mlangoni.

Katika uchaguzi wa ndani ya CCM wa viongozi mbalimbali katika ngazi tofauti tofauti unaoendelea nchini kwote umekuwa Ni gumzo hapa nchini. Mijadala yote ya kisiasa katika vijiwe vyote,mitaa yote,vyombo vyote vya Habari,mitandao yote ya kijamii Ni juu ya CCM na uchaguzi, Ni juu ya Nani kapitishwa na Nani kakatwa na Nani apigiwe kura za Ndio na Nani awe na Subira.

Ni uchaguzi ambao umeviteka vyama vya upinzani hasa chadema na kujikuta Vimesimamisha shughuli zake zote za kisiasa na kujikita kufuatilia uchaguzi wa viongozi wa CCM, kwa kuwa hakuna habari inayovuma kwa Sasa Kama uchaguzi wa CCM, Chadema imegeuka na kuwa Tawi la kuwatambulisha wagombea wa CCm, chadema ndio wamekuwa Kama maafisa habari wa habari za CCM juu ya Nani kakatwa na sababu za kukatwa kwake, chadema kwa Sasa imejikita katika kufuatilia kwa kina kinachoendelea katika uchaguzi huu na kusahau shughuli zao za ndani ya chama Chao

Hii Ni kutokana na Nguvu waliyonayo na wanayokuwa nayo viongozi wa CCm, hii Ni kutambua ushawishi wa viongozi wa CCm katika masuala mbalimbali yanayogusa maisha ya watanzania,kwa kuwa Hawa ndio wafuatiliaji wa utekelezaji wa ilani ya CCM, Hawa viongozi wa CCm Ndio wenye wajibu wakufahamu ikiwa wananchi wanapata huduma na kuhudumiwa Kama ilivyo ahidiwa katika ilani kupitia uchaguzi mkuu,Hawa ndio wenye ofisi ambazo zimekuwa wazi muda wote na kimbilio kwa waliokata Tamaa au kuonewa au kudhulumiwa au kucheleweshewa haki au kupokonywa haki.

Hawa ndio sauti kwa wasio na sauti na nguvu kwa wasio na nguvu, Hawa ndio unaoweza ukawakimbilia na kupokelewa kwa uharaka,Hawa ndio wanaoweza kumsikiliza mwananchi mnyonge yeyote mwenye shida, Hawa ndio wanaojuwa Hali za kimaisha za watanzania na kuishi nao, Hawa ndio Tumaini la wote,Hawa ndio wanaoweza kumuita kiongozi yeyote wa serikali atoe majibu kwa maswali ya wananchi,Hawa ndio wenye masikio sikivu na macho ya kutazama kila kitu

Hakika CCM itaendeleaa kuongoza nchi hii Daima Milele na Hakuna chama Wala mtu mwenye uwezo wa kuitikisa CCM hapa nchini ,hayupo na Wala hajazaliwa, Kama huamini Basi ondoka ndani ya CCM uone kama CCM itatikisika au kuteteleka. Hii ndio CCM chama kiongozi , Chama Cha Hayati Baba wa Taifa mwalimu Nyerere, Chama kinachoheshimika ndani na nje ya Tanzania,

Chama mkombozi wa nchi za kusini Mwa Afrika, chama kilichobeba matumaini ya watanzania, chama kinachokubalika na kuaminika na makundi yote ya watanzania,chama chenye dira na muelekeo unaoeleweka, chama kilicho na misimamo na misingi madhubuti , chama kinachotanguliza maslahi ya Taifa mbele. Ni chama kilicho katika mikono salama ya Mwenyekiti wake Shupavu,Mzalendo na Hodari mh Mama Samia Suluhu Hassan.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu: 0742-676627

Kwahiyo habari za panya road zilizovyoteka vyombo vya habari maana yake hao panya road walikuwa ni bora?
 
Ndio tatizo kubwa la vimbwenelehi, kwa vile vimejiunga JF juzi kwa special assignment basi vinaona havionekani na kutambulika basi vinaweka namba za simu!
Aweke na picha yake hata mke na watoto kama anao ili ccm wawaandikishe kama Next of KinView attachment 2420959

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Weka na profile yako mkuu
 
Kwahiyo habari za panya road zilizovyoteka vyombo vya habari maana yake hao panya road walikuwa ni bora?
Achana na Habari za panya road, hao walishasambaratishwa mtandao wao na kufikishwa katika vyombo vya sheria
 
Unajua kwa mwezi chadema ilikuwa inapokea ruzuku shilingi ngapi?. Ukijua chukua mapato na matumizi kwa mwezi ndio utaona ulivyo kilaza wa kudandia mambo Wala huyajui.
Kama mlishindwa kubalansi vitu hivyo ili mpate akiba ya kujenga hata ofisi he nchi mngeiweza?
 
Kwani hujaona mh Rais wetu mpendwa mama Samia akizindua mitambo mikubwa ya kuchimba visima virefu vya maji vitakavyo saidia kuondoa tatizo la maji?

Magufuli alikuwa anahubiri kuwa amesambaza maji asilimia 75% ya nchi,tukawa tunasema ule ni utapeli. We hapa unaongelea magari ya kuchimba maji! Bado unaamini kuna wajinga wa hivyo? Hayo magari ni utapeli kama utapeli mwingine, hapo walipo wanaomba mvua zinyeshe ziwaondoe kwenye hiyo dhahama. Machafuko tu ndio yataondoa hiki chama kinachong'ang'ania madaraka huku hakina uwezo.
 
Achana na Habari za panya road, hao walishasambaratishwa mtandao wao na kufikishwa katika vyombo vya sheria

CCM ina tofauti gani na panya road, au kutamba na maVX ya kodi za wanaume ndio unawaona ni tofauti na panya road?
 
Kwani hujaona mh Rais wetu mpendwa mama Samia akizindua mitambo mikubwa ya kuchimba visima virefu vya maji vitakavyo saidia kuondoa tatizo la maji?

Be realistic. Chukua idadi ya hivyo visima na ugawanye na idadi ya watu wa Dar wasio na uunganishwaji wa maji. Halafu niambie kisima kimoja kinatosha watu wangapi?. Dar Ina idadi ya watu zaidi ya milioni tano lakini waliounganishiwa maji ni laki tano tu. 2022 bado unasifia visima?
 
Kama mlishindwa kubalansi vitu hivyo ili mpate akiba ya kujenga hata ofisi he nchi mngeiweza?

Nimekuuliza wewe mpayukaji . Kama hujui matumizi ya CHADEMA kwa mwezi na kiasi Cha Ruzuku wanachopewa kwa mwezi kaa kimya.
 
Nia ipi hiyo embu itaje, mbona magazetini hujawahi uliza maana yakuweka namba mwisho wa makala

Basi kaandike magazetini. Magazetini huwa Wana maeditor wanao hariri hizo taarifa. Ukiongea uongo Kama wako mahakamani kesi ya madai. Muulize nduugu musiba kilichomtokea.

Sasa kaandike huu ujinga kwenye gazeti Kama CHADEMA watakuacha salama.
 
Magufuli alikuwa anahubiri kuwa amesambaza maji asilimia 75% ya nchi,tukawa tunasema ule ni utapeli. We hapa unaongelea magari ya kuchimba maji! Bado unaamini kuna wajinga wa hivyo? Hayo magari ni utapeli kama utapeli mwingine, hapo walipo wanaomba mvua zinyeshe ziwaondoe kwenye hiyo dhahama. Machafuko tu ndio yataondoa hiki chama kinachong'ang'ania madaraka huku hakina uwezo.
Kila siku nakwambia kuwa hakuna wa kuleta machafuko nchi hii kwa kuwa serikali iliyopo madarakani Ni sikivu na inawajali watu wake ndio maana inaungwa mkono na mamillion ya watanzania. Katika Hilo hata wewe unafahamu namna watanzania wanavyoiunga mkono serikali yao ndio sababu walimgomea na kumpuuza Lisu alipowaambia waandamane ikiwepo wewe mwenyewe ambaye ulimgomea Lisu baada ya kutambua kuwa Ni mbabaishaji tu
 
Basi kaandike magazetini. Magazetini huwa Wana maeditor wanao hariri hizo taarifa. Ukiongea uongo Kama wako mahakamani kesi ya madai. Muulize nduugu musiba kilichomtokea.

Sasa kaandike huu ujinga kwenye gazeti Kama CHADEMA watakuacha salama.
Hapa pia Ni sehemu ya kupashana habari na inawafikia watu wengi tu ikiwepo wewe mwenyewe
 
Hii namba ya simu hapa chini ni ya nini?
Alishauriwa na wadau hapa hapa maana mwanzo alikua haweki sasa hivi kaweka mnamnanga tena, maisha ni magumu huko porini kwake alipo, mwenzio yupo mawindoni
 
Kila siku nakwambia kuwa hakuna wa kuleta machafuko nchi hii kwa kuwa serikali iliyopo madarakani Ni sikivu na inawajali watu wake ndio maana inaungwa mkono na mamillion ya watanzania. Katika Hilo hata wewe unafahamu namna watanzania wanavyoiunga mkono serikali yao ndio sababu walimgomea na kumpuuza Lisu alipowaambia waandamane ikiwepo wewe mwenyewe ambaye ulimgomea Lisu baada ya kutambua kuwa Ni mbabaishaji tu

Sikivu kwa huu mgao wa umeme na maji? Au hujui unaongea nini? Naona unadhani uoga kwa serikali ndio mapenzi ya wananchi kwa serikali ya majizi ya kura.
 
Back
Top Bottom