Uchaguzi wa karibuni kwenye mazingira kama yetu, ni huu wa juzi Zimbabwe.
Waangalizi mbali mbali mbali wakiwamo SADC, Carter Center na wengine, wamelazimika kuuita kwa majina yake. Yaani kwa ufupi, wameuona siyo uchaguzi bali ni wizi wa mchana kweupe.
Hapa chini ni sampuli za yale matokeo pendwa ya zile tume zetu za kizalendo kutokea vyama tawala kama yanavyoendelea kutolewa:
Hiyo CHADEMA ya huko (CCC) ndipo sasa watajua kumbe walikuwa hawajui.
"Kibaka ni kibaka tu."
Ajabu na kweli hiki chama cha upinzani, CCC kilikwenda kufanya nini kwenye uchaguzi wa namna hii? Kwa hiyo sasa ndiyo waanze kulalamika siyo? Kwamba walikuwa wamesahau nini?
Haya si ndiyo ya kwetu: CHADEMA, ACT na wore wenye kujinasibu kusaka ukombozi wa nchi hii? Watakayokuja kuyalalamikia 2024 na baadaye 2025?
"Hivi kweli hiyo itakuwa ni akili, au matope?"
Kwani hata haya 2020 hatukuyasikia?
"Au ni kuchagua kuwa kama mang'ombe tu?"
Enyi ndugu mnaojielekeza kwenye kushiriki uchaguzi mkuu 2024/25 bila shaka kwa msukumo wa njaa zenu binafsi, siyo siri kuwa mnaturudisha nyuma sana kwenye ukombozi wa nchi hii.
"Ama kwa hakika mkisikia tunawaita ni wasaliti bila kujali nyadhifa zenu au historia zenu, wala msishangae."
Si mkajiunge hata na kina Makhtoum kwenye biashara za bandari huko? Kama taabu yenu kumbe ni njaa za matumbo yenu na familia zenu tu?
Ifahamike hatuujui msimamo mwingine baina yetu, zaidi ya huu hapa:
Uchaguzi bila katiba mpya wa nini?