Uchaguzi Zimbabwe, upinzani Tanzania bado hatujifunzi?

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Uchaguzi wa karibuni kwenye mazingira kama yetu, ni huu wa juzi Zimbabwe.

Waangalizi mbali mbali mbali wakiwamo SADC, Carter Center na wengine, wamelazimika kuuita kwa majina yake. Yaani kwa ufupi, wameuona siyo uchaguzi bali ni wizi wa mchana kweupe.

Hapa chini ni sampuli za yale matokeo pendwa ya zile tume zetu za kizalendo kutokea vyama tawala kama yanavyoendelea kutolewa:

IMG_20230826_091329~2.jpg

IMG_20230826_091304~2.jpg

Hiyo CHADEMA ya huko (CCC) ndipo sasa watajua kumbe walikuwa hawajui.

"Kibaka ni kibaka tu."

Ajabu na kweli hiki chama cha upinzani, CCC kilikwenda kufanya nini kwenye uchaguzi wa namna hii? Kwa hiyo sasa ndiyo waanze kulalamika siyo? Kwamba walikuwa wamesahau nini?

Haya si ndiyo ya kwetu: CHADEMA, ACT na wore wenye kujinasibu kusaka ukombozi wa nchi hii? Watakayokuja kuyalalamikia 2024 na baadaye 2025?

"Hivi kweli hiyo itakuwa ni akili, au matope?"

Kwani hata haya 2020 hatukuyasikia?

"Au ni kuchagua kuwa kama mang'ombe tu?"

Enyi ndugu mnaojielekeza kwenye kushiriki uchaguzi mkuu 2024/25 bila shaka kwa msukumo wa njaa zenu binafsi, siyo siri kuwa mnaturudisha nyuma sana kwenye ukombozi wa nchi hii.

"Ama kwa hakika mkisikia tunawaita ni wasaliti bila kujali nyadhifa zenu au historia zenu, wala msishangae."

Si mkajiunge hata na kina Makhtoum kwenye biashara za bandari huko? Kama taabu yenu kumbe ni njaa za matumbo yenu na familia zenu tu?

Ifahamike hatuujui msimamo mwingine baina yetu, zaidi ya huu hapa:

Uchaguzi bila katiba mpya wa nini?
 
Nchi zetu hizi kuna wakati unaona afadhali warudi wazungu kututawala, kwasababu inavyoonekana sisi wenye matatizo tumeshindwa kabisa kutatua matatizo yetu, hii ni kama laana, bara zima hasa kusini mwa Jangwa la Sahara tunalalamika tu, chaguzi mbovu kila mahali.
 
Baadhi ya Wapinzani daima huwa wanajidanganya na makundi ya watu wanaohudhuria mikutano yao.Wasijue kuwa hata wanaohudhuria kwenye mikutano ya vyama Tawala ni hao hao.
CCM,kwa mfano,imejikita hadi ngazi ya mashina ambako viongozi wake wanaitwa mabalozi.Hao viongozi wanazengo huwatumia kama viongozi wao katika masuala mbalimbali ya kijamii.
Wakati wa uchaguzi viongozi hao huwa waratibu wa kampeni kwa ajili ya CCM kwenye mashina yao.
Wapinzani wanabaki na mikutano ya hadhara tu na wakiondoka hakuna mtu wa kuendeleza kampeni.Na kwenye vituo vingi tu Wapinzani,wakiwemo Chadema,huwa hawaweki mawakala.
 
Si mkubali uwepo wa katiba yenye tume huru kuthibitisha madai yenu? Kumbe hofu ya nini?
 
Baadhi ya Wapinzani daima huwa wanajidanganya na makundi ya watu wanaohudhuria mikutano yao.Wasijue kuwa hata wanaohudhuria kwenye mikutano ya vyama Tawala ni hao hao.
CCM,kwa mfano,imejikita hadi ngazi ya mashina ambako viongozi wake wanaitwa mabalozi.Hao viongozi wanazengo huwatumia kama viongozi wao katika masuala mbalimbali ya kijamii.
Wakati wa uchaguzi viongozi hao huwa waratibu wa kampeni kwa ajili ya CCM kwenye mashina yao.
Wapinzani wanabaki na mikutano ya hadhara tu na wakiondoka hakuna mtu wa kuendeleza kampeni.Na kwenye vituo vingi tu Wapinzani,wakiwemo Chadema,huwa hawaweki mawakala.
Sio kweli na wala usitake kupotosha. Sehemu nyingi CDM huweka mawakala na bado hutangazwa mgombea wa CCM. Kwa mfano uchaguzi wa 2020 mawakala wengi wa upinzani hasa wa CDM hawakuapishwa, na waliofanikiwa kuapishwa bado hawakuruhusiwa kuingia vituoni, au waliruhusiwa kuingia muda ukiwa umeenda huku kukiwa na mabox ya kura yaliyo na kura nyingi kuliko za watu waliojitokeza kupiga kura. Na kibaya zaidi hata fomu za matokeo zilikuwa sio za kweli. Na mawakala walilazimishwa kusaini fomu hizo fake ama wabambikiwe kesi.

Michezo hii ya kishenzi ilifanyika mbele ya mafisa wa tume ya uchaguzi, na kwa usimamizi wa vyombo vya dola. Ndio maana kila siku huwa nasema uchaguzi hapa nchini sio uchaguzi, bali ni maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Machafuko tu ama mapinduzi ya kijeshi ndio yatarejesha heshima ya box la kura.
 
Bila kuficha watu wengi wamechoshwa na Serikali iliyomadarakani, pia wamechoshwa na chaguzi za mazingaombwe, hvyo bas Katba mpya, NI muhimu mno kwa sasa
Sitegemei kupata katiba mpya ya kuweza kupambana na hali hii, huku katiba hiyo ikihodhiwa na CCM. Labda yatokee machafuko ama mapinduzi ya kijeshi ndio huu upuuzi utafikia mwisho.
 
Nchi zetu hizi kuna wakati unaona afadhali warudi wazungu kututawala, kwasababu inavyoonekana sisi wenye matatizo tumeshindwa kabisa kutatua matatizo yetu, hii ni kama laana, bara zima hasa kusini mwa Jangwa la Sahara tunalalamika tu, chaguzi mbovu kila mahali.
Naunga mkono hoja
 
Uchaguzi wa karibuni kwenye mazingira kama yetu, ni huu wa juzi Zimbabwe.

Waangalizi mbali mbali mbali wakiwamo SADC, Carter Center na wengine, wamelazimika kuuita kwa majina lake. Yaani kwa ufupi, wameuona siyo uchaguzi bali ni wizi wa mchana kweupe.

Hapa chini ni sampuli za yale matokeo pendwa ya zile tume zetu za kizalendo kutokea vyama tawala kama yanavyoendelea kutolewa:

View attachment 2729187

View attachment 2729188

Hiyo CHADEMA ya huko (CCC) ndipo Sasa watajua kumbe walikuwa hawajui.

Kibaka ni kibaka tu.

Ajabu na kweli hiki chama cha upinzani, CCC kilikwenda kufanya nini kwenye uchaguzi wa namna hii? Kwa hiyo sasa ndiyo waanze kulalamika siyo? Kwamba walikuwa wamesahau nini?

Haya si ndiyo ya kwetu CHADEMA, ACT na wenye kujinasibu kusaka ukombozi wa nchi hii watakayokuja kuyalalamikia 2024 na baadaye 2025?

Hivi kweli hiyo itakuwa ni akili, au matope?

Kwani hata haya 2020 hatukuyasikia?

View attachment 2729204

Au ni kuchagua kuwa kama mang'ombe tu?

Enyi ndugu mnaojielekeza kwenye kushiriki uchaguzi mkuu 2024/25 bila shaka kwa msukumo wa njaa zenu binafsi, siyo siri kuwa mnaturudisha nyuma sana kwenye ukombozi wa nchi hii.

Ama kwa hakika mkisikia tunawaita ni wasaliti bila kujali nyadhifa zenu au historia, wala msishangae.

Si mkajiunge hata na kina Makhtoum kwenye biashara za bandari huko kama taabu yenu kumbe ni njaa za matumbo yenu na familia zenu tu?

Ifahamike hatuujui msimamo mwingine baina yetu zaidi ya huu:

Uchaguzi bila katiba mpya wa nini?
Baadhi ya mataifa ya West Africa majenerali wameanza kuonyesha uzalendo.....!!
 
Sitegemei kupata katiba mpya ya kuweza kupambana na hali hii, huku katiba hiyo ikihodhiwa na CCM. Labda yatokee machafuko ama mapinduzi ya kijeshi ndio huu upuuzi utafikia mwisho.
Tupo kwenye dimbwi zito, ambalo linahitaji maamuzi mazito Sana, CCM hawawezi kukubali Katiba itakayotengeneza anguko lao.
 
Back
Top Bottom