Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Siku ya leo, Baraza la Taifa la Mitihani Nchini Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne na kufuta utaratibu wa muda mrefu wa kutoa orodha na mtiririko wa ubora wa shule kulingana na kiwango cha ufaulu na pia limefuta utaratibu wa kutangaza wanafunzi bora wa mitihani hiyo. NECTA imetoa sababu kuu mbili za wao kufanya hivyo, ambazo ni;
-Kutangaza shule bora ni kutangaza biashara kwa shule hizo.
-Hakuna usawa baina ya shule moja na nyingine katika mazingira ya utoaji elimu hivyo hawapaswi kushindanishwa.
Kwa kuwa JF ni Kisima cha maarifa na uchambuzi huru, Mimi binafsi hapa hapa nitazipinga hoja zote hizo mbili kwa kuchambua kwa kina hoja kwa hoja.
1. Hoja ya kutangaza biashara
Kwanza kabisa hoja hii imekaa kiupande mmoja, ni hoja ya kibaguzi kwa 100% na kuumiza wasiohusika kwa 100%. It is a double standard decision. Sababu za kibiashara zimewalenga wamiliki wa shule binafsi (zimewabagua) na hapo hapo zinazinyima fursa shule za serikali pasipo sababu (zime wahukumu pasipo kuhusika).
Pili ni hoja ya nusu nusu mno, kwa kuwa NECTA hiyo hiyo ndio imekuwa ikitoa hadharani matokeo yote ya shule moja moja yenye kuakisi ubora wa shule husika, hata kama NECTA haitaweka mtiririko rasmi wa ubora bado mtu yoyote makini (hata asiye makini) anaweza kuchambua na kuonyesha zipi ni shule kumi bora zaidi kulingana na mtiririko wa kimatokeo ulivyo.
Na katika hili, mtu au taasisi tofauti (vikiwemo vyombo vya habari) vinaweza kuja na uchambuzi wenye kukinzana na kuzaa upotoshaji. Kifupi tu, NECTA imejivua jukumu lake na sasa inakwenda kuruhusu mtu au taasisi yoyote kujitangazia ubora wake kimatokeo, hata kama ni kwa upotoshaji. Na tutegemee matangazo ya kibiashara (yenye chembechembe za upotoshaji) kwa kwa kutumia matokeo ya NECTA yakichipuka na kuongezeka maradufu. Mwisho katika hili, NECTA haipaswi kukwepa kuteketeleza majukumu yake, kisa tu inaogopa kivuli cha kuonekana inatangazia biashara shule bora. Vipi kama shule hizo 10 bora ningekuwa ni shule za serikali tu?
2. Hoja ya mazingira yasiyolingana katika utoaji elimu hapa nchini
Nadhani huenda hii ni hoja ya kipumbavu kupita maelezo kuwahi kutolewa na NECTA. Kwanza kabisa kuweka hoja sawa, sote yanapaswa kufahamu kuwa, NECTA haiwajibiki popote katika kutengeneza, kuboresha au kuyapima mazingira ya utoaji elimu hapa Tanzania, hivyo hawapaswi kuyasemea chochote mazingira hayo maana sio jukumu lao.
Pili NECTA wanawajibika kuandaa, kusimamia, kusahihisha na kutoa matokeo ya mitihani. Kama NECTA wanaona na kuamini kuwa mazingira ya utoaji elimu hapa Tanzania hayako sawa baina shule na shule na yanaathiri matokeo yao, ni kwanini waandae mitihani mmoja kwa wote au usahihishaji na utoaji wa alama za ufaulu uwe sawa?
Kwanini suala la utofauti wa mazingira baina ya shule moja na nyingine liwe ni hoja wakati wa kutangaza ubora wa shule tu, lakini isiwe ni hoja ya msingi wakati wa kutunga mitihani, kusahihisha na kuweka alama za ufaulu?