Uchaguzi 2020 Uchambuzi: Hotuba ya Tundu Lissu kutangaza nia ya Kugombea Urais - Juni 8, 2020

Uchaguzi 2020 Uchambuzi: Hotuba ya Tundu Lissu kutangaza nia ya Kugombea Urais - Juni 8, 2020

Uchaguzi ungekuwa wa HURU na HAKI mchuano ungekuwa mkali.

Tume ya uchaguzi - sisiemu
Mahakama - sisiemu
Vyombo vya dola - (wakuu wa mikoa/wilaya)makada wa sisiemu
Mkuu siku zote CCM huwa inashinda kihalali kabisa ndio mana uliona kura za rais zilipungua ingekua wanaweza kuiba wangekua wanashinda kwa asilimia 98 huko.

Evidence nyingine ni chadema kushinda madiwani wengi na wabunge wengi last time. Ila this time twende na magufuli mkuu amalizie kazi aliyoianza ametufikisha pazuri penye ukweli tusifie mkuu
 
Amani iwe nanyi Wadau.

kama wote mnavyojua leo ndo siku ile ambayo watanzania kwa pamoja wameweza kushuhudia hotuba ya kwanza kutoka kwa gwiji la upinzani, ndugu Tundu Antipas Lissu. Hotuba iliyokuwa imejaa utulivu, akili, busara na hekima iliyotukuka.

Kama kawaida CCM walipanga yao, kwanza walipanga vijana wao kushambulia kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo facebook na Youtube ili tu kujaribu kuonesha umma na dunia kuwa Lissu hakubaliki ila kiukweli Lissu kwa hotuba ya leo ameonesha kuwa amejiandaa vizuri na amejipanga vizuri kuwa Raisi wa Tanzania mwaka 2020...
Lissu anatikisa sana nafikiri CCM matumbo moto moto.
 
ITV na Azam ni local vimeogopa ila international kama BBC na VOA vimerusha kama kawaida
 
Wakuu upo usemi kwamba Mungu akupi vyote. Aghalabu Wazungumzaji wazuri huwa si watendaji wazuri.

Kwenye ujengaji hoja Lissu yupo vizuri sana lakini ikulu hayahitajiki maneno pekee bali matendo zaidi. Tumpime Lissu kwenye rekodi zake za utendaji na ndio kitu muhimu zaidi.

Unaweza ona Lissu anafaa kuwa Rais wa JMT kwa kuwa tu anajenga hoja vizuri lakini kumbe nafasi inayomfaa Lissu ni kuwa mshauri tu wa Rais.

Watu wengi waliovizuri mdomoni si watendaji wazuri.

Nawasilisha.
Kwa hiyo unaahauri tubaki mr misifa ambaye anajua mabavu na kulazimisha kupendwa?
 
Nashangaa sana watu waliotishwa na kahutuba ka lisu, mtoto halali na hela, mwacheni tu ajitutumue ila ukweli anaujua mwenyewe na habari zake tunazo
Siku kukiwa na tume ya uchaguzi tutaona mengi sana
 
Nimebet kuonesha msisitizo. Siyo kuwa simuungi mkono Lissu lahasha. Ila Itakuwa vigumu kushinda. Rejea vizuri hotuba ya Lissu UTANIELEWA.
Mimi kwenye Lisu kushinda au kushindwa, sijali! Maisha yako ni muhimu, acha viapo vya kijinga!
 
Kwa maono hayo Iko siku utaota mbawa. Mpe hongera!

Kuna ujanja wa aina fulani. Wanajua hawawezi kupata urais hivyo anasukumiwa mtu ambaye hawezi rudi Bungeni. Wale wenye uwezekano wa kurudi Bungeni, wanajaribu kuomba tena Ubunge. Lissu hapati kitu jimboni sasa naona anasukumiwa urais. Sawa lakini tunataka azungumzie matatizo ya nchi: elimu, uchumi, sayansi, afya, miundombinu, nk. siyo mambo ya risasi zake 30s.
Katika hotuba yake wewe umeona kazungumzia risasi zake ?
 
Kwa kura halali au zakusimamiwa na Polisi na Tume?
Thubutuuu. Lisu anaisaidia tu CCM KUWA USHINDI wake ulikuwa na upinzani mkali. Na hivyo kuonekana kuwa uchaguzi ulikuwa wa haki na kikatiba.

Kama atakuwa Rais wa JMT Mimi nitajiua kwa kula sumu siyo kwa jiwe ninalolijua Mimi.
 
Watanzania tunawajua, walizoea kuongea kwa uhuru na sio hii hofu waliyopandikiziwa hivi sasa. Watanzania wako kimya maana kundi la watu wasiojulikana linawateka na kuwatoa uhai.

Chaguzi zinanajisiwa kimachomacho, na kuishia kupata viongozi waliopo madarakani bila ridhaa yao. Usidhani hao wananchi hawaoni yote hayo hata kama hawaongei kwa hofu ya kutekwa, na kuhujumiwa shughuli zao.

Haya manyanyaso na kutawala watu kwa shuruti yataisha tu. Hizo kinga mnazotafuta za kutaka kuwafanyia maovu, ushidhani hao watanzania hawaoni.
 
Kwa maono hayo Iko siku utaota mbawa. Mpe hongera!

Kuna ujanja wa aina fulani. Wanajua hawawezi kupata urais hivyo anasukumiwa mtu ambaye hawezi rudi Bungeni. Wale wenye uwezekano wa kurudi Bungeni, wanajaribu kuomba tena Ubunge. Lissu hapati kitu jimboni sasa naona anasukumiwa urais. Sawa lakini tunataka azungumzie matatizo ya nchi: elimu, uchumi, sayansi, afya, miundombinu, nk. siyo mambo ya risasi zake 30s.

Kaongea mengi kweli, ila hilo la risasi 16 ndio limekukera zaidi maana unajua ni kashfa itakayosumbua kwenye masikio ya wapiga kura. Hayo ya elimu, sayansi, afya nk yako kwenye ilani, leo alikuwa anazungumza kwa ujumla. Akipewa ridhaa na chama chake atanadi kwenye ilani. Usitake aongee kwa mujibu wa mtazamo wako na kile kitakachowafurahisha. Bado unadhani kuna watu watafanya siasa kwa utashi na mwenendo wa kiccm?

Leo naona mmeongezewa nguvu na jeshi la akiba, nadhani imeonekana nyie wenyewe mtachemsha. Pambaneni mkanushe kwa hoja alichokisema, na muweke ukweli.
 
Pamoja na kwamba Magufuli hafai Urais, Sikuwai kuona kama Lissu anafaa, though tunataka mbadala lakin, Wakipangwa wawili Ntamchagua tu Lisuu kama Nilivyomchagua Magufuli nikamuacha Lowassa,

Hawa wawili wakilinganishwa naona Lissu ana Unafuu kidogo angalau 25% ya sifa za urais anazo

Ufanano na utofauti wa Magufuli na Lissu kwenye ngazi ya juu ya uongozi wa nchi
Britannica uraisi ni taasisi sio maamuzi binafsi kama anavyofanya Jiwe kuvunja katiba kila mara. Ukiheshimu katiba na utawala wa sheria utaweza kuwa raisi manake yote unayotekeleza yanakuwa kwenye ilani ya chama husika!
 
Leo unahangaika kweli kweli haaaaa yaani hili ni bandiko la sita baada ya hotuba iliyojaa madini na vitamins za kutosha kutolewa kule Belgian
 
Hizo kelele unazopiga kuhusu huyo tundu ni humu mitandaoni tu,
ila mitaani kwenye maisha halisi ya watanzania ndio wanajua nani mtendaji na nani mlopokaji kuhusu utendaji serikalini

Huko mitaani si ndio kundi la watu wasiojulikana limetapakaa, yoyote asiyesujudia sifa za bandia anafanyiwa zengwe kwenye shughuli zake, anatekwa au kuuwawa? Hivi unadhani hawa wa huku mitandaoni hawakai mitaani?

Huku ndio pekee watu wanaweza kuongea ukweli, ambao huko mtaani ni kutaka kukutana na mabalaa. Hiki sio kizazi cha kuisujudia ccm tena hata ifanye nini. Ndio maana unaona, uhayawani, ushenzi na ukatili wa wazi kwenye chaguzi zetu, ili ccm ikae madarakani.

Huo uhayawani kwenye chaguzi utakuwa na mwisho wake, subiri tu utaona mziki wake. Hizo kinga za kutoshitakiwa ili mfanyie ukatili watanzania zitagota tu.
 
Back
Top Bottom