Uchambuzi: Huyu Amaleki anayezungumziwa na Askofu Gwajima ni nani?

Halafu wanachorus zao eti hawaumwi kiviilee! Sasa kama kama umechanja unaumwa na kuna vyuma havijachanja na haviumwi au navyo haviumwi kivileee. Yaani sound kibao
Mpaka ikupate au imuondoe ndugu yako ndo utapupia chanjo
 
Nakubaliana na wewe kwenye historia ya waameleki lakini wazo lako kuwa kwa Israeli kutaka kufanya siasa na Imani kuwa kitu kimoja waisraeli walikosea.

Hapo sio sawa. Israeli ni taifa aliloliunda Mungu kupita kwa Ibrahim, isaka yakobo mpaka Yesu. Nia ya Mungu ni kuwa taifa hili limwakilishe hapa duniani katika mpango wake wa kuifuta dhambi iliyotokea edeni(kwa hapa duniani). mambo ya taifa la Israeli yaliendeshwa kwa kupata uongozi wa Mungu kupitia manabii na wazee.

Walipokuww wakitii maelekezo ya Mungu mambo yalinyooka walipokwenda kinyume waliangushwa. Kwa mantiki hiyo kwa waisraeli (wa Kale na wa Sasa) pona Yao ilitokana na kumtii Mungu kama taifa. Hivyo habari ya hii ni siasa hii ni Imani kwa waisraeli yote ni Imani na yote ni siasa kwa maana kwamba survival Yao inategemea utii wao kwa Mungu.

Of course kwa hivi leo hiyo inayoitwa Israeli sio inayoishia kwa hiyo Imani. Hao ni watu waliomkataa Yesu na hivyo wamekuwa kama wapagani wengine.

Waisraeli wa Sasa ni wale wanaoishi sawa sawa na mapenzi ya Mungu bila kujali wanatoka nanjilinji au wanatoka pale tel Aviv
 
Nina shaka sana na wachungaji walioenda kinyume na Gwajiboy kwenye suala, nyeti sana kwa Gwajiboy, la kususia chanjo za COVID-19!
Wajikaze tu wasijetoka mashimoni!
NIMEKUELEWA SANA MTOA MADA! πŸ™πŸ™πŸ™
 
Du jamaa umechanganyikiwa!
 
Nawiwa kurudia tena kusoma vitabu vitano vya Musa nijifunze kitu katika mambo ya kiutawala, ahsante kwa bandiko Mimi nimeondoka na elimu nyingine kabisa ambayo sikuitarajia.

Ya Gwajima na CCM yake naomba niwaachie wahusika
Biblia ni tamu sana hasa katika vile vitabu vya agano la kale! Ukivisoma kwa umakini utagundua kwamba hakuna jipya chini ya jua!
 
Mimi nachukuwa a very short brief kutoka kwenye Bible kwamba Chuki ya Waamaleki kwa Wayahudi na majaribio yao ya mara kwa mara ya kuwaangamiza watu wa Mungu yalipelekea adhabu yao ya mwisho. Hatma yao inapaswa kuwa onyo kwa wote ambao watajaribu kupinga mpango wa Mungu au ambao watalaani kile ambacho Mungu amebariki. Kwa kisa cha Gwajima mjadala unaweza kuwa Mpana zaidi, Amaleki aweza kuwa uongozi mzima kiserikali au serikali, Amaleki yaweza kuwa wale anaona kuwa wanapingana na utawala, Ameleki yaweza kuwa wapinzani kisiasa nk
 
Amalek nahisi namjua ila siwezi kuweka hapa nisije kuambiwa mimi ni GAIDI na 'nilipanga kulipua bahari ya Hindi na ziwa Victoria'πŸ™
 

Mkuu Nimependa Ulivyomalizia
Ni yule mtibeli kutoka nyota ya tibeli yenye mbawa mbili irukayo huku na huku;
 
Asante sana ROBERT HERIEL . Ni kweli kwamba nchi yetu ilikuwa ikielekea kwenye nchi ya ahadi. Nchi ya SGR, nchi ya JNHPP, nchi ya barabara ya njia nane kutoka KIMARA hadi KIBAHA, nchi ya flyhovers, nchi ya shirika imara la ndege ATCL, nchi ya shirika imara la simu, TTCL, nchi ya mauzo sahihi ya madini yake na Vito vya thamani, nchi isiyokuwa na majangili, nchi isiyokuwa na mafisadi.
Lakini naona sasa tumerudi nchi ambayo serikali kuu inahangaika kujenga matundu ya vyoo ambayo yalishakasimiwa kwa halmashauri za vijiji, kata na wilaya.
 
Huwezi tenganisha Dini na Siasa Mkuu.

Ukishakuwa mtumishi wa Mungu automatically umejiingiza kwenye siasa

Kifo cha Yohana mbatizaji Kifo cha Yesu vyote vilikuwa vifo vya kisiasa; ni kweli kabisa mkuu huwezi kutenganisha dini na siasa
 


Nafikiri Gwajiboy anazungumzia hayo
 


Hiyo ni Kwa mujibu wa Biblia kitabu kilichoandikwa na Waandishi wa kiyahudi.

Ulitegemea upate simulizi ipi tofauti na hiyo kama wameandika waisrael wenyewe.

Ni Sawa na Gazeti la CCM unategemea wataandika Jambo gani tofauti na kujisifia wao wenyewe.
 

Mkuu nimekubali uchambuzi wako upo sawa
 
Leo nakupa heko [emoji109]umeichambua vizuri mada

Asante sana infact hata sikuwa naijua hio amalek ndio nini!?
 
Ugomvi huu hautamsaidia
Utamsaidia kwasababu kiwango cha ujinga ni kama kimeingezeka. Elimu mbovu inayotolewa huku watawala wakiona poa imezalisha vijana wa hovyo ambao bila shaka ni mwiba kwa watawala haohao. Hawajui kusoma wala kuelewa jambo ila wanajua kuandika utumbo, matusi na kulalamika tu mitandaoni. Hata ukitangaza kila mkulima atagaiwa trekta moja, still watanzania watalalamika tu.
 
You mean it's push gang vs soga gang ?? Waamalek vs waisrael ??!! I don't think so ! But time will tell !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…