Uchambuzi: Uyahudi alizaa watoto wawili, mkubwa aliitwa Ukristo na mdogo akaitwa Uislam

Yacobo na yusuph sio ndugu bali ni mtu na mwanae, yaani yusuph ni mtoto wa yacobo wa kuzaa kabisa
 
[emoji85][emoji85][emoji89]
 
Mkuu hizi dini usizungumzie kwa chuki wala ubaguzi kumbuka zimeletwa na wamissionary na Waarabu walipokuja kuchukua malighafi Afrika mimi siwezi kumchukia au kumbagua mtu kwa Dini yake najua historia yake jinsi ilivyosambazwa...
 

Elimu bila ya malipo

 

Ongeza dawa hii

 
Tupe basi hizo fact tujue
 



Kwanza na kabla ya yote, lazima itambulike kuwa Yesu Kristo, mwana wa Mariamu, alikuwa ni wa mwisho katika orodha ya manabii wa Kiisraeli.


Aliishi kwa mujibu wa Torati, na sheria ya Musa, na aliwafundisha wafuasi zake wafanye hivyo hivyo.


Katika Mathayo 5:17- 18, Yesu ameeleza:


“Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua Torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kuitimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.”

Kwa bahati mbaya, kiasi cha miaka mitano baada ya kuisha kwa uchungaji wa Yesu, Rabbi kijana kwa jina la Sauli wa Tarsus, aliyedai kuwa amemuona Yesu katika maono, alianza kubadilisha njia ya Yesu.


Paulo (jina lake kwa Kirumi) alikuwa na heshima kubwa kwa falsafa ya Kirumi na alizungumza kwa ufahari kwa kuwa na uraia wa Roman.


Imani yake ilikuwa ni kuwa wasio-Wayahudi walioingia Ukristo wasibebeshwe mzigo wa Torati kwa hali yoyote ile.

Mtunzi wa Matendo 13:39 anamnukuu Paulo akisema,

“Na kwa yeye kila amwaminiye huhesabiwa haki katika mambo yale yote asiyoweza kuhesabiwa haki kwa Torati ya Musa.”

Kimsingi ilikuwa ni kwa kupitia juhudi za Paulo ndipo kanisa lilipoanza kufuata mkondo wa tabia za wasio-Wayahudi.

Paulo ameandika barua (nyaraka), nyingi za Agano Jipya zinazokubaliwa na kanisa zikiwa ni kama mafundisho rasmi ya kiitikadi na Kitabu kilichofunuliwa.

Nyaraka hizo hazikuilinda Injili ya Yesu wala hata kuiwakilisha; badala yake yamegeuza mafundisho ya Kristo kuwa ya falsafa ya Kihelleniki (Graeco-Roman).


Differences of the Ministries of Jesus and Paul
Jesus:Paul:
1. Preached the gospel of the kingdom1. Preached the gospel of the grace of God
2. Defined the “kingdom of heaven” as Israel’s prophetic earthly kingdom2. Defined the “kingdom of heaven” as the heavenly position of the body of Christ
3. Presented Himself as the Messiah and King of the Jews (Israel)3. Presented Jesus as the risen Lord, Head of the Church, the body of Christ
4. Preached repentance, water baptism, keeping the Law, forgiving others, and faith in who He was as necessary for salvation4. Preached faith alone in the death, burial, and resurrection of Christ as necessary for salvation
5. Had Jews as His audience (a couple exceptions)5. Had Gentiles as his primary audience
6. Operated under the Mosaic Law6. Operated under grace
 


Paulo mpinga kristo. Mwanzilishi halisi wa Ukristo!

- Imani ya Ukristo inapinga mafundisho ya Mungu katika Hosea 6:6,

"Maana nataka rehema, wala si sadaka; na kumjua Mungu kuliko sadaka za kuteketezwa."

-Pia inapinga mafundisho ya Yesu anaposema katika Mathayo 9:13,

"lakini kama mngalijua maana yake, nitakuwa na rehema wala si dhabihu"... tena Yesu alisema katika 12:7 "Lakini kama ikijulikana maana yake ni nini, nataka rehema, wala si dhabihu”

- ni Paulo aliyefikiri ufufuo (Matendo 17:18).

Paulo, ambaye hakuwahi kumwona Yesu, alikiri katika 2Timotheo 2:8, kwamba kulingana na yeye tu Yesu alifufuka na alikuwa wa kwanza kufundisha Mungu alikuwa na mwana, Mdo 9:20,

UKRISTO NI FUNDISHO LA PAULO NA SI YESU

- Marko 16:9, ilifutiliwa mbali kutoka kwenye biblia na manabii wengine wengi waliinuliwa hadi mbinguni k.m. Eliya (2Wafalme 2:11-12) pia Henoko katika Mwanzo 5:24 na kurudia katika Waebrania 11:5.

- ukombozi wa dhambi ulikubaliwa miaka minne baada ya Yesu kuondoka na inapingana na biblia katika vifungu vingi sana.. k.m. duet 24:16, yerimiah 31:30, Ezekieli 18:20, Mathayo 7:1-2, 1Wakorintho 3:8, Mathayo 19:4

hivyo sote tulizaliwa bila dhambi.

Paulo alikomesha sheria ya mosaic matendo 13:39.
 

PAULO AU YESU? IMANI AU MATENDO?

Hebu yazingatie Mahubiri ya Yesu aliyotoa juu ya Mlima wa Zaituni:

Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie. Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni. Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
Mathayo 5.17-20

Mnamo mahubiri ya Mlima wa Zaituni ndio yanapatikana mafunzo makubwa ya Yesu Kristo.

Tunaweza kusema kuwa humu, khasa, ndio umo Ukristo; yaani ikiwa tunaamini ya kuwa Yesu ndiye Katika kifungu cha maneno hayo tuliyoyanukulu ya Yesu tunaona ya kuwa ni muhali mtu kuingia katika ufalme wa mbinguni, yaani Peponi, mpaka haki ya mtu izidi ile ya waandishi na Mafarisayo.

Yaani wema uutendao uzidi ule wa wanazuoni wa Kiyahudi.

Ni nini hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo?

Ni kuifuata sharia ya Taurati neno kwa neno, na pia waliofunza manabii wengineo.

Ndio maana Yesu akasema:

"Msidhani ya kuwa nalikuja kutangua torati au manabii, sikuja kutangua, bali kutimiliza."

Kazi yake haikuwa kutengua sharia ya Taurati na kuleta kitu kingine cha kutengua au kugonganisha na mafunzo ya sharia ya Mwenyezi Mungu na Mitume wake, bali kaja yeye kutimiliza kwa kuwafunza Mayahudi umuhimu wa mambo ya kiroho katika sharia.

Kutii madhaahiri ya sharia tu na kuwacha undani wake, uchamngu, hakutoshi.

Mwenyezi Mungu atiiwe kwa dhaahiri na kwa siri.

Yesu alishikilia sana kufundisha na kutenda, aliposema:

"Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni."

Katika amri za Taurati ni kama hii iliyomo katika Biblia:

Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu. Msile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu.

Mambo ya Walawi 11.7-8

Kwa hiyo naliwaambia wana wa Israeli, Msile damu ya mnyama wa aina yo yote; kwa kuwa uhai wa wanyama wote ni katika hiyo damu yake; atakayeila awaye yote atakatiliwa mbali. Tena kila mtu atakeykula nyamafu, au nyama aliyeraruliwa na wanyama, kama ni mzalia, kama ni mgeni, atafua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni; ndipo atakapokuwa safi.
Walawi 17.14-15

Hizo ni amri ziliomo katika Taurati, sharia ya Mungu, ambayo Yesu amesema kama ilivyo katika Injili ya Mathayo kuwa mwenye kuivunja ndogo yao na akawafundisha watu hivyo basi ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni.

Na kuvunja hayo khasa ndio Paulo kafundisha. Msikieni:

Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri; maana Dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo.

1 Wakorintho 10.25-26

Mnamwona Paulo anavyobomoa sharia ya Taurati waliyoifwata Manabii wote, hata Yesu na wanafunzi wake thenashara, ya kuwa kuna vyakula vilivyo halali na kuna vingine ni najisi, haramu kuliwa, kama nguruwe, vya kunyongwa na damu?

Yesu kafunza nini, na Paulo anafunza nini!

Katika waraka wake aliowapelekea Wagalatia Paulo anasema:

Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema, Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya imani. Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.

Wagalatia 5.4-6

Kwa kauli moja Paulo ameitengua sharia yote.

Yesu kasema nini juu ya Mlima wa Zaituni na Paulo anasema nini katika barua yake kwa Wagalatia?

Yesu alifuata sharia ya Mwenyezi Mungu na aliihishimu na akaahidi kuwa yeye hatoitengua kabisa, ila ataitimiza.

Paulo anaibeza sharia na kuiona kuwa ni laana.

Yesu akila kilicho halalishwa na Mungu, na alikiepuka kilicho harimishwa na Mungu.

Paulo anatwambia tule kila kiuzwacho sokoni bila ya kujali dhamiri yetu.

Yesu na Manabii wote tangu Nabii Ibrahim walitahiriwa kwa kufuata amri ya Mungu kama isemavyo Biblia:

Mungu akamwambia Ibrahimu, Nawe ulishike agano langu, wewe na uzao wako kwa vizazi vyao baada yako. Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa.
Mwanzo 17.9-10

Paulo mjuaji, anasema kumpinga Mungu:

Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya.
Wagalatia 6.15

Katika barua yake aliyowapelekea Warumi ndio kabisa Paulo anaiangamiza sharia ya Mungu na kufanya vitendo kuwa havina maana yo yote.

Chenye maana peke yake ni imani tu.

Basi, twaona ya kuwa wanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria.
Warumi 3.28

Kwa Paulo kuamini kuwa Yesu kafa msalabani na damu yake kuwa ni fidia kwa dhambi zetu ndio kwenye maana, sio kufuata sharia wala vitendo.

Kwake yeye ile Taurati, ambayo Yesu mwenyewe hakuja kuitengua bali kaja makusudi kuitimiza, ni kifungo na pingamizi. Anawaambia Warumi:

Bali sasa tumefunguliwa katika torati, tumeifia hali ile iliyotupinga, ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya roho, si katika hali ya zamani, ya andiko.

Warumi 7.6

Paulo anaiona Taurati ni kifungo, pingamizi, bali ni laana.

Hayo sio maoni ya Yesu ambaye amesema:

"Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka."

Je, kwa kuingia Paulo katika umoja wa Kikristo ndio tusema mbingu na nchi zimeondoka?

Au kwa kutundikwa Yesu msalabani (ikiwa kweli katundikwa) ndio tuseme mbingu na nchi zimeondoka?

Mbona watu wameyasahau upesi maneno ya Yesu mwenyewe, na kuyasikiliza ya Paulo?

Kwa sababu yanakubaliana na matamanio yao?

Mafunzo ya Paulo yalileta mzozano na ubishi mkubwa tangu pale mwanzo katika historia ya Kanisa baina ya kikundi chake cha Wakristo waliomfuata kutoka upagani, na wale Wakristo wa asli ya Kiyahudi.

Wao walipinga moja kwa moja ile shauri ya kwenda kupelekewa mafunzo ya Ukristo mataifa waliokuwa hawakutahiriwa, wala hawaikubali sharia ya Taurati.

Baadhi ya wanafunzi wa Yesu walikuwa hawakubali hata kula nao wale "wasiotahiriwa".

Wao walikuwa wanajua vyema kuwa Yesu aliwakataza wasend kuwahubiria mataifa mengine isipokuwa Mayahudi tu, kwani ni wao ndio walikuwa wanaamini Mungu Mmoja na wao ndio wakiifuata sharia ya Mungu.
Mwishowe ulifanywa mkutano na yakawapo baadhi ya masikilizano kuwa yafaa kuhubiriwa Ukristo kwa mataifa yasiokuwa ya Kiyahudi, na wao wasilazimishwe kubeba mizigo mizito katika dini kama vile wenye asli ya Kiyahudi.

Walitumwa Paulo na Barnaba kuwaendea hao mataifa, nao ni Wazungu wa Kirumi na Kigiriki, na wakachukua barua iliomalizikia maneno haya muhimu:

Kwa maana ilimpendeza Roho Mtakatifu na sisi, tusiwatwike mzigo ila hayo yaliyo lazima, yaani, mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama zilizosongolewa na uasherati. Mkijizuia na hayo mtafanya vema. Wasalamu.

Matendo 15.28-29

Nyama zilizosongolewa, yaani nyama za kunyonga, zisiochinjwa.

Yazingatieni haya si maamrisho ya Yesu, lakini ni masikilizano baina akina Paulo na wanafunzi wake Yesu,(kwa ridhaa ya Roho Mtakatifu) baada ya kuwa Yesu mwenyewe hayupo tena.

Ikiwa hayo ndiyo waliokubaliana ilikuwaje Paulo tena kuwaandikia Wakorintho: "Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni bila ya kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri"? Lakini Paulo ni Paulo.

Inaendelea
 

Mtakatifu Paulo anadai kuwa yeye aliteuliwa makhsusi kuwa ni mtume wa Yesu katika ufunuo (Wahyi), na kuwa bado yeye anaendelea kupata amri moja kwa moja kutokana na mwenyewe Bwana Yesu, ijapokuwa amri hizo na mafunzo hayo yanapingana kabisa na yale waliyoyapata wale wanafunzi wake Yesu waliokuwa naye mwenyewe alipokuwa hai.

Yeye Paulo hakupata kuonana na Yesu, bali yeye alikuwa ni mpinzani mkubwa wa Ukristo na akawa ni sababu ya kuteswa na kuuwawa Wakristo kadhaa wa kadhaa, mmoja wao ni Mtakatifu Stefano, shahidi wa mwanzo katika Wakristo.

Paulo alikuwa na asili ya Kiyahudi, na dini yake rasmi ilikuwa ya Kiyahudi.

Kwa kuwa alizaliwa nje ya Palastina katika mamlaka ya Kirumi alikuwa na uraia kamili wa Kirumi, na huko alipata fursa ya kusoma ilimu na falsafa za Kiyunani.

Mazingara yake yote ya Kigiriki na Kirumi yalikuwa ya kikafiri, kipagani.

Kwani Magiriki na Warumi walikuwa washirikina wenye kuamini chungu ya miungu, kama ilivyokuwa ada ya karibu mataifa yote ya wakati ule isipokuwa Mayahudi.

Yalipozuka mafunzo ya Yesu Kristo, ambayo kwa asili yake hayakuwa ila ni kuendeleza ile ile imani ya Kiyahudi ya Mungu Mmoja na kufuata sharia ya Taurati na kuongeza uchamungu, na ikawa mafunzo hayo yanaendelea juu ya kupingwa, Paulo aliona anaweza kuipa nguvu hiyo dini au kwa hakika madhehebu mpya kwa kuwatia wale Warumi na Magiriki kwa kuchanganya imani zao na falsafa zao pamoja na imani ya Kiyahudi.

Mayahudi wanaamini Mungu Mmoja, ndio.

Ukristo unaamini Mungu Mmoja.

Magiriki na Warumi wanaamini miungu mingi, si chini ya watatu, ndio na Ukristo nao unaamini hivyo.

Jee, si pana mgongano hapo?

La, katika Ukristo imani ni ya Mungu Mmoja katika Utatu Mtakatifu: Mungu Mmoja, mwenye nafsi tatu, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.

Mapagani wa Kigiriki na Kirumi wakiamini mungu aliyekufa, akafufuka na akapaa mbinguni.

Hilo si kitu wanaweza kuendelea na imani hiyo katika Ukristo.

Wazungu magovi hawataki kutahiriwa.

Hapana kitu, kutahiriwa si kitu wala kutotahiriwa.

Hoja ipatikane tahara ya roho.

Wazungu wamezoea kula kila kitu, nguruwe, damu, kilichochinjwa na kisichochinjwa.

Hilo si tatizo, mtaendelea vivyo hivyo, kwani dhambi ni kitokacho mdomoni, sio kiingiacho.

Kuleni kila kiuzwacho sokoni.

Hapana halali wala haramu.

Huo ndio Ukristo mpya wa Paulo, na hiyo ndio Thiolojia yake ambayo, inasikitisha Wakristo wameifuata, wakayaacha mafunzo mepesi na yaliyonyooka ya mwenyewe Yesu Kristo.

Hayo ni maji makuu, letu sisi ni kuangalia yaliyomo ndani ya Biblia Takatifu.

Tuiache iseme.

Habari za kugeuka Paulo akaacha kumpinga Yesu, na badala yake akawa mfuasi wake zinasimuliwa pahala patatu katika Matendo ya Mitume katika Agano Jipya la Biblia.

Na katika zote mara tatu kisa hicho kinakhitalifiana katika mambo muhimu.

Kwanza tunasoma katika Sura ya 9 mstari wa 3 mpaka wa 7:

Hata (Paulo) alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni.

Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, (yaani Paulo) mbona waniudhi?

Akasema, U nani wewe, Bwana?

Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe.

Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda. Na wale waliosafiri pamoja naye wakasimama kimya, wakiisikia sauti, wasione mtu.
Matendo 9.3-7

Katika maelezo hayo hapo ni mwandikaji anasimulia. Yapo mambo mane lazima tuyazingatie vizuri katika maelezo hayo:

Mwangaza ambao Paulo ulimwangaza. Haikusemwa kuwa wengine waliuona mwangaza ule au la, lakini waliisikia sauti.

Ni Paulo ambaye "akaanguka chini."

Yeye na wale watu waliokuwa pamoja naye waliisikia sauti, lakini hawakumwona mtu.

Sauti ya Yesu ilimuamuru "aingie mjini, naye ataambiwa yampasayo kutenda." Hapo hakuambiwa nini la kutenda.
Katika Biblia hiyo hiyo, katika kitabu hicho hicho cha Matendo ya Mitume, sura 22, mstari wa 6 mpaka wa 10 ipo ncha ya pili ya hadithi kusimulia tukio lile lile.

Msimulizi hapa ni Paulo mwenyewe:

Ikawa nilipokuwa nikisafiri, nikikaribia Dameski, wakati wa adhuhuri, ghafula nuru kuu ilitoka mbinguni, ikanimulikia pande zote. Nikaanguka nchi (yaani chini), nikasikia sauti ikiniambia, Sauli, Sauli, mbona unaniudhi? Nikajibu, Wewe u nani, Bwana? Akaniambia, Mimi ni Yesu Mnazareti, ambaye wewe unaniudhi. Na wale waliokuwa pamoja nami waliiona ile nuru, lakini hawakuisikia ile sauti ya yule aliyesema nami. Nikasema, Nifanye nini, Bwana? Bwana akaniambia, Simama, uingie Dameski, na huko utaambiwa habari za mambo yote yaliyoamriwa uyafanye.
Matendo 22.6-10

Ncha hii yakubaliana na ile ya mwanzo katika mambo haya:

Aliyeanguka chini ni Paulo na sio wale waliokuwa pamoja naye.

Aliloambiwa Paulo ni kuingia mjini na huko ndiko atakoambiwa nini la kulifanya.

Ncha hii lakini inakosana na ile ya kwanza kuwa ya kwanza yasema ya kuwa wale waliokuwa naye "wakasimama kimya, wakisikia sauti, lakini haikusema kuwa waliona nuru.

Katika ncha hii ya pili twaambiwa: waliiona ile nuru, lakini hawakuisikia ile sauti.

Ncha ya tatu ya tukio hilo hilo muhimu kabisa katika historia ya Ukristo inaelezwa katika maneno yake mwenyewe Paulo vile vile kama inavyosimuliwa katika kitabu kile kile cha Matendo ya Mitume sura ya 26 mstari wa 12 mpaka wa 18:

Basi katika kazi hiyo nilipokuwa nikienda Dameski, mwenye mamlaka na maagizo ya wakuu wa makuhani; Ee Mfalme, ndipo wakati wa adhuhuri njiani naliona nuru inatoka mbinguni ipitayo mwangaza wa jua, ikinimulikia mimi, na wale waliofuatana nami pande zote. Tukaanguka nchi (chini) sote, nikasikia sauti ikisema nami kwa lugha ya kiebrania, Sauli! Sauli! mbona waniudhi? ni vigumu kwako kuupiga mateke mchokoo (ujiti wenye ncha wa kuchokolea). Nami nikasema,Wewe u nani, Bwana? Bwana akaniambia, Mimi ni Yesu, ambaye wewe unaniudhi. Lakini inuka, usimame kwa miguu yako, maana nimekutokea kwa sababu hii, nikuweke wewe uwe mtumishi na shahidi wa mambo haya uliyoyaona, na wa mambo ambayo katika hayo nitajidhihirisha kwako; nikikuokoa na watu wako, na watu wa Mataifa, ambao nakutuma kwao; uwafumbue macho yao, na kuwageuza waiache giza na kuielekea nuru, waziache na nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu; kisha wapate msamaha wa dhambi zao, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu mimi.
Matendo 26.12-18

Sasa hapa tunaona khitilafu kubwa na zile ncha za hadithi ziliomo katika sura ya 9 na sura ya 22 katika hicho hicho kitabu kimoja cha Matendo ya Mitume. Hebu tuchungue:

Kwa mujibu wa ncha hii si Paulo pekee aliyeona nuru - kama ilivyoelezwa pale mara ya kwanza - lakini wote waliokuwa naye waliona nuru, kama ilivyoelezwa mara ya pili.

Hapa Paulo anasema: Tukaanguka nchi sote. Haya yanapinga ncha ya kwanza na ya pili zilizosema kuwa ni Paulo tu peke yake ndiye aliyeanguka chini.

Katika masimulizi ya kwanza na ya pili ilisemwa wazi kuwa Paulo aliambiwa aingie mjini Demeski na huko ataambiwa habari za mambo yote yaliyoamriwa ayafanye.

Hii mara ya tatu mambo yote ameamuriwa hapo hapo kabla ya kuingia mjini, kinyume na ilivyosimuliwa mara ya kwanza na ilivyosimuliwa mara ya pili.

Tena hapo Paulo alimsikia Yesu anamuamrisha amri kinyume na alivyokuwa akiwafunza na kuwaamrisha wanafunzi wake siku zote katika uhai wake - anamuamrisha Paulo apeleke utume wa Yesu kwa mataifa mengine yasiyokuwa Mayahudi.

Kadhaalika kinyume na mafunzo ya Yesu katika uhai wake anamuamrisha afunze kuhesabiwa haki kwa imani na kufutiwa dhambi.

Inaendelea
 

Mafundisho yaliyotulia kabisa ya Yesu ni yale aliyohubiri juu ya Mlima wa Zaituni.

Na maoni yake yaliyo wazi na kauli ya kukata juu ya sharia na matendo, ni yaliyomo katika sura 5 ya Mathayo.

Akizungumzia juu ya wale wanaodai kuwa wao ni wafuasi wake, na kuwa ati wanafunza mafunzo yake, na huku kumbe wanayapotoa yale aliyoyafunza, Yesu anaambiwa kasema:

Si kila mtu aniambaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.
Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba.
Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.

Mathayo 7.21-27

Hayo ni maneno aliyohitimishia Yesu mawaidha yake juu ya Mlima wa Zaituni.

Ni maneno yaliyokaa sawa, yawazi, hayana ubabaishi.

Ni nani hao "watendao maovu", hao wapumbavu, wasiofuata mafunzo ya Yesu wakayatenda, mafunzo ambayo msingi wake ni kutimiliza sharia na manabii, na kutenda mapenzi ya Mungu?

Ni nani hao wanaodai kufanya miujiza na kuponyesha watu kwa jina la Yesu, na kudai kuwa ni mitume wa Kristo, na huku wanapinga mafunzo yake, na kuwaambia watu kuwa wataokoka kwa imani tu kwamba Yesu kafa msalabini kwa ajili yao, bila ya haja ya vitendo?

Ni nani hao wanaolitumia jina la Yesu naye mwenyewe atawakataa?

Kama tuna akili basi yafaa tuitumie.

Tusiwe kama mtu mpumbavu ajengaye nyumba yake juu ya fungu la mchanga.

Tutaanguka, na anguko letu litakuwa kubwa.

Mafunzo ya Yesu Kristo si haba, lakini kwa ufupi wa maisha yake (aliwahi kuhubiri kiasi miaka miwili mitatu tu) na kutokuwa tayari ulimwengu kuchukua kweli yote, hakuweza kutimiza ujumbe wote wa Mwenyezi Mungu.

Ni hikima yake Mwenyezi Mungu kuwa kila nabii aliyemleta alikuwa anaongeza juu ya yale yaliyotangulia.

Ni kweli Yesu alisema kama ilivyo katika Mathayo 5.17-20 ambayo tumekwisha yataja kuwa yeye alikuja kutimiza Taurati na mafunzo ya Manabii, hakuja kutengua lo lote katika hayo.

Ulipokaribia wakati wake wa kuondoka aliungama kuwa mengi aliyo nayo hana nafasi ya kuyasema, lakini atakuja mwengine ambaye atauwongoza ulimwengu kwenye kweli yote, na ataufundisha ulimwengu mafunzo kamili juu ya dhambi na haki.
 
aiseee... umefikiria sana mkuu

Endelea kusoma ndugu, hayo ni maandiko na historia , sijatia langu , mwenye macho haambiwi tazama

Kazi kwako kumfuata Yesu au Paulo , na ukimfuata Yesu ndiyo yale yale mafundisho ya mitume wote Kuanzia Adam mpaka Muhammad SAW ambayo ni uislamu

Ukimfuata Paulo utakuwa umeangamia
 
Sio kweli

Muslims & Christians are ALL Monotheist

Ni Waamini wa Mungu Mmoja, hakuna POPOTE anayejiita Mkristo anaamini kuwa kuna Miungu (zaidi ya Mungu mmoja)

Yapasa watu waelewe:

Inawezekana kabisa kwa Mungu mmoja kuwa na nafsi 3 kwasababu yeye ni Mungu hashindwi kufanya hivyo

Hata katika Uumbaji both kwa Wakristo na Waislam Mungu alifanya uumbaji akiwa na nafsi zaidi ya moja

Sehemu nyingi alitumia maneno kama

Na
''Tumfanye Mtu kwa mfano wetu

''Tumekuumbeni
'' Tumekutumeni mfanye hivi na hivi

Kuanza na neno TU....inamaanisha hakuwa peke yake ilihali tunaamini ni Mungu Mmoja.
 
Leo umejitahidi kujibu kwa akili na ufahamu badala ya mihemko

Ni kweli kuna sehemu nyingine Mtume Paulo alikuwa anatamka

'' Ningependa mfanye hivi...

'' Ninashauri katika mambo ya roho mfanye hivi

'' Enyi mlioamini fanyeni hivi na vile

This means kuna mahali Paulo alikuwa anatoa mitazamo yake kwa kutumia akili na ufahamu wake na sio ya kiroho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…