Mimi naona Maghufuli ajitambui kabisa.. kuwa anagombea uraisi kupitia chama tawala kilichoongoza nchi miula yote. na yeye akiwa ni kiongozi ngazi ya uwazir ktk miula mitatu.
Lakini ukitafakari sera za maghufuli ni kama vile ameamuwa kila mtu afe na mzigo wake.. sbb hotuba zake zote zinaingelea madhaifu yanayotendeka ndani ya serikali akigusia kila idara...
1. Kalamu sana kufa kwa viwanda... ila hiyo mikoa yote ambayo viwanda vimekufa,mingi inashikiliwa na ccm.. na ni serikali hihi ambayo imeuwa viwanda.. sasa hao wabunge wa ccm walikuwa wapi miaka yote kulipigia kelele bungeni.. je serikali awamu yote ilikuwa wapi??? waziri wa viwanda utaongea nini kwa watanzania
2. Elimu bure kuanzia la kwanza mpaka kidato cha nne - hivi kwautajiri tuliokuwanao wote... nilitegemea angesema mpaka kidato cha sita bure..na hii ilikuwa sera ya chadema japo chadema ilisema elimu itakuwa bure kwa ujumla. sasa hayo mabunge ya ccm yalikuwa wapi sikuzote kulipigia kelele swala la elimu kutolewa bure...au serikali kwa ujumla. waziri waelimu ambaye ni mbunge wa ccm,kazi unayo.
3. Afya - maghufuli anawatuumu manesi na madaktari kuchochea kuzorota kwa uduma ya afya tena kwa kuwatuumu ktk uwibaji wa dawa.ktk ili nilijuwa atakwenda kuongelea mzizi wa tatizo .. kulipwa kwa deni la msd, mishahara yao kuboreshwa.. kuliko kukaa na kuwatuumu.. hii inaonyesha wazi waziri wa afya hakuwa mtendasi mzuri.. mpaka anaruhusu wizi kutendeka au na yeye ni mwizi na uwenda hata ili deni la msd ni waziri katafuna pesa zetu kwa madawa ambayo yaliuzwa wanapojua wao.
Ni mengi sana yakuandika ila na malizia kwa kusema kweli nyani haoni kundule... ufisadi uliyofanyika ktk daraja la kigamboni hajagusia,nyumba zetu alizouza kwa bei ya kutupa na kujenga nyengine kwa ghala za juu,na uku watumishi wengi wakibakiwa bila makazi, amekaa kimya.
Maghufuli unaitaji wabunge wa CCM kuongoza nchi, badilisha hotuba zako.
Bye bye.