Mkuu, unaongelea changamoto ya kusafirisha kama vile Kaskazini ni mikoa mipya inayohitaji kuanza michakato ya ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji wa umeme.
Mpaka sasa mikoa hii inatumia umeme wa Gridi ya taifa, kwahiyo hakuna hizo gharama za ujenzi, fidia wala muda kama ulivyotueleza hapa.
Nakubaliana na wewe kwenye point mbili ambazo ni unafuu wa umeme unaotoka Ethiopia kuliko tunaozalisha sisi, na pia suala la kuepuka gharama za upotevu unaotokana na conduction resistance.
Lakini tukirudi kwenye uhakisia, hatukustahili kununua umeme huu, badala yake tujenge powerstations hata kama ni kwa muda mrefu lakini tutakua na uhakika wa kutumia umeme wetu.
Serikali inatushika kwa kutaja hasara ya 32 B kwa kupoteza hizo 17 MW zinazopotea kwenye usafirishaji wa kuelekea kaskazini, lakini wasichotueleza kwamba hiyo ni hasara ya kimahesabu na sio hasara halisia. Ni sawa na mtu alieweka mkeka kwa gharama ya elfu 10 kubetia timu fulani ishinde apate Millioni 1, katikati ya mechi akaamua kusitisha ubashiri wake baada ya kusahwishiwa na laki 3 kwa kuhofia timu yake ingepoteza. Huyo mtu anaweza kusema amepata hasara ya laki 7 kwasababu asingesitisha angepata milioni, lakini kiuhalisia anakua kapata faida ya laki mbili na 90.
Hicho ndicho tunafanya sisi pia, tunaepusha kupoteza 17 MW ambazo zitabaki kama ziada tu kwenye gridi na badala yake tunaenda kununua 100 MW ambazo pamoja na kuwa za bei rahisi, lakini zitakua na gharama zaidi ya hiyo 32 B tunayopoteza. Kwa hesabu za mtaani tunakua tumepata hasara zaidi.
Nadhani uamuzi sahihi ulikua kujifunza teknolojia wanayotumia wao kufikisha umeme wao Namanga kwa gharama nafuu na sisi tuanze kujichanga kutengeneza miundombinu yetu ifikie ubora huo, ikiwemo kujenga hizo Substations za HVDC.