LGE2024 Uchambuzi ziara ya muenezi Paul Makonda, serikali ya CCM 2024 kukosa kura?

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
January 2024

TATHMINI YA ZIGO ZITO ALILOTWISHWA MUENEZI PAUL MAKONDA KURUDISHA IMANI KWA RAIA

Ziara ndefu ya Paul Makonda ambaye ni katibu uenezi, itikadi na mafunzo wa CCM imeibua na kuweka wazi jinsi chama hiki kongwe dola kimeshindwa kuweka mifumo ya utawala bora. '


View: https://m.youtube.com/watch?v=PIP2WWD5wlsKundi la burudani la CCM TOT Plus wakipasha moto jukwaa ktk ziara ya muenezi Paul Makonda

Ziara hiyo ya muenezi wa CCM imeanzia mkoa wa Dar ikaenda Pwani na kuingia Tanga, kisha Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Singida, Tabora, Shinyanga kuelekea kanda ya Ziwa .

Baadhi ya watanzania ambao bado walikuwa wanadhani matatizo yao yanawakumba wao wachache, wamegundua kumbe wapo kwa mamia wenye matatizo kama yao.

Wananchi wamejionea wenyewe kuwa wametukana na wenzao waliobeba bahasha za kaki zenye nyaraka zao ambazo zinabeba haki zao za kila aina walizotegemea mifumo ya serikali ya CCM ingetatua lakini haijawezekana na hivyo wote kuelekeza matumaini yao kwa mtu mmoja Paul Makonda atafanya miujiza.

Picha: Katibu muenezi Paul Makonda akijaribu kutatua matatizo kwa kuongea na simu.

Miujiza ambayo kwa uhakika haiwezi kutokea kwa kuwa mfumo rasmi wa utawala bora, utendaji kazi, kuwajali watu na rasilimali za kuwezesha serikali ifanye kazi haipo.


Na udhaifu huo wa CCM umeonekana hadi kwa wanaosemekana ni viongozi wa kuchaguliwa yaani wabunge wa 2020.

Picha: Hon. Emmanuel Adamson Adamson, Mwakasaka, Mbunge (CCM) wa Jimbo, Tabora Mjini

Wananchi wa Tabora mjini wamemuambia wazi Makonda kuwa mbunge wao Hon. Emmanuel Adamson Mwakasaka, Mbunge wa Jimbo, Tabora Mjini haishi tena Tabora wala hawamuoni jimboni, ametoweka na kuwaacha kama mayatima.

Mbunge mwingine wa CCM ya 2020 wa jimbo la Same magharibi Kilimanjaro Hon. Dr. David Mathayo David naye amekataliwa wazi na watu wengi waliojitokeza waliovaa mashati ya kijani na mayowe kutanda katika mkutano Same magharibi kuwa hawamtaki.

Dr. David Mathayo David mbunge (CCM) Same Magharibi

Wananchi wengi wa kawaida sasa kweli ni wanyonge kwa kuwa wana hati za umiliki ardhi lakini haki hiyo imeporwa. Wengine wana hukumu za Mabaraza ya Ardhi au Mahakama lakini wanazungushwa kupata haki ya kurudishiwa ardhi zilizoporwa.


Wengi wamejaribu kufika ofisi wa wakuu wa wilaya ambao waliteuliwa kwa kigezo cha waligombea kuomba ubunge na kushindwa kura za wajumbe wa CCM, hivyo kupewa uDED na uDC kama kukiimarisha chama kongwe dola ngazi ya wilaya na majimbo.

Lakini hao maDC na maDED na ma RAS makada wa CCM wameonesha kushindwa kutumikia vyeo hivyo vyenye mamlaka ya maamuzi ngazi hizo za wilaya na halmashauri.


Imebidi muenezi Paul Makonda jeshi la mtu mmoja kuanza kuwapigia simu mawaziri waliopo Dodoma na Dar es Salaam ili kujaribu kuwapoza wananchi wenye kero kibao zilizoshindikana ngazi za maeneo yao.

Ni jambo la kushangaza kuwa wananchi wanaweza kumuamini waziri mgeni aliye mbali na maeneo yake ataweza kupata ufumbuzi wa kero zinazowasumbua badala ya kuwepo mifumo bora ya utawala bora kuanzia chini kwenda juu.

Je swali kuu ziara ya katibu muenezi itikadi na mafunzo yeye pekee yake kama Paul Makonda bila mifumo thabiti ya utawala katika ngazi serikali za mitaa na serikali ndiyo inaweza kuipa CCM kupata ushindi wa kishindo 2024 na 2025?


Swali jingine imani hii kwa CCM iliyobaki kiduchu huko kote anapopita Paul Makonda mwezi January 2024 inaweza kuendelea kubaki katika mioyo ya raia.

Au baada ya wananchi wenyewe kubaini na kuona wazi kwa mamia yao wameshindwa kusaidiwa, mbali walijitahidi kunyoosha vidole kama wanafunzi ktk darasa la wazi au kuonesha bahasha za hati zao, mabango ya kero wamebaini jinsi uozo wa kimfumo wa serikali ya CCM ulivyo mkubwa kumzidi Paul Makonda na hivyo mzigo umemshinda msukuma.

Na hivyo kuna uwezekano sasa kuamua kuingia katika maandamano ya amani kudai haki zao mbalimbali?
 
Mkapa, kikwete, Magufuli na sasa Samia wote wameshindwa kutatua Huduma za Umeme hata kwa asilimia 60.

Ccm ni chama kizee
 
Mkapa, kikwete, Magufuli na sasa Samia wote wameshindwa kutatua Huduma za Umeme hata kwa asilimia 60.

Ccm ni chama kizee
Nakueleza ivi kwasasa hata uyo sijui Waziri wa Nishati Dottohakuna anachofanya.umeme unakatika kwa saa 24 hapa mjini namaanisha kinondoni na sinza iyo huko mikoani ni balaa.umeme unakatwa saa moja asubuh unarudishwa saa sita usiku and then saa nane usiku unakata na huwezi jua utarudi saa ngapi...yaan umeme imekua ni anasa ivi unajiuliza tuna serikali kweli???halafu wanatembea na msafara mkubwa doing dramas nchi nzima yaan you look at them unajiuliza do they have ata akili kidogo tu???kwamba tuko zama za uhalisia na utandawazi hii jamii inaelewa kila kitu usipoteze muda kuwadanganya??wanajua umeme ni haki yao sio anasa na kwamb hii serikali inazembea ndo mana hawapti umeme...
 
Hicho cheo cha serikali kisiasa cha naibu waziri mkuu ni kiini macho cha kuwafumba kundi flani la watu wasipoge kelele kwa awamu hii. Cheo cha mwenezi huy ni kigezo kile kile.
 
Huwa sipati majibu kwa nini huyu mtu hayupo jela. Ina maana hata mahakama zooooooote duniani hakuna namna?! Kwani wanasheria na viongozi wa Chadema wanaona hili ni poa tu au mimi ndio sielewi mweh.
 
Huwa sipati majibu kwa nini huyu mtu hayupo jela. Ina maana hata mahakama zooooooote duniani hakuna namna?! Kwani wanasheria na viongozi wa Chadema wanaona hili ni poa tu au mimi ndio sielewi mweh.
Apelekwe jela ya wapi?
 
Au baada ya wananchi wenyewe kubaini na kuona wazi kwa mamia yao wameshindwa kusaidiwa, mbali walijitahidi kunyoosha vidole kama wanafunzi ktk darasa la wazi au kuonesha bahasha za hati zao, mabango ya kero wamebaini jinsi uozo wa kimfumo wa serikali ya CCM ulivyo mkubwa kumzidi Paul Makonda na hivyo mzigo umemshinda msukuma.[emoji419][emoji375]


Sent using Jamii Forums mobile app
 
ZIARA YA MAKONDA :
KILIO CHA CCM KUWA INAJALI WANYONGE NA INAONGOZA AJENDA YA UMOJA WA KITAIFA

UMOJA WA KITAIFA 4Rs , Ni Kauli Mbiu Ya Kutafutia Uungwaji Mkono Kuelekea 2024 na 2025 Kwa Nia Safi au Ni Ngazi Ya Kutumiwa Kusalia Madarakani Kwa Hila

“National unity” is a bromide often trumpeted by politicians

HOTUBA YA MSOMI AYN RAND KUHUSU KAULI ZA UMOJA NA KUUJALI UMMA WAKATI WA KUELEKEA UCHAGUZI

Anachofanya muenezi Paul Makonda kilipata kuonywa ni ulaghai na msomi wa sayansi ya siasa maarufu Bi. Ayn Rand ambaye aliwatahadharisha wapiga kura kuwa makini na ziara zenye propaganda kujenga umoja wa kitaifa zisizo na mashiko

View: https://m.youtube.com/watch?v=o8IT4uaTlmgVideo speech / Excerpt / text below:
 
Wengine wana hukumu za Mabaraza ya Ardhi au Mahakama lakini wanazungushwa kupata haki ya kurudishiwa ardhi zilizoporwa.

28 January 2024
Shinyanga, Tanzania

MAKONDA ALIA KWA UCHUNGU - AKATISHA HOTUBA- MAMA AMTAJA TAJIRI ANAYEDAIWA KUMTEKA MUMEWE TANGU 2021


View: https://m.youtube.com/watch?v=tTsPLJRAKUE
baada ya kusikiliza maelezo ya mazingira mtu mwenye ardhi alivyotekwa, maelezo ya mkuu wa mkoa, ushahidi wa RPC kuhusu jalada kuwa ofisi ya NPS. Katibu uenezi ashikwa na simanzi huku akiishiwa nguvu jinsi mfumo wa jinai haki na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa inavyochukulia kwa wepesi kutekwa, kupotea .....
 
Mkapa, kikwete, Magufuli na sasa Samia wote wameshindwa kutatua Huduma za Umeme hata kwa asilimia 60.

Ccm ni chama kizee
Nyie tafuteni njia ya kuinua chama chenu kisiasa acheni kupitia mgongo wa Mwenezi wetu...Anafanya siasa na Raia wameonyesha bado Imani Yao ipo CCM.

Kuacha siasa tuje kwenye serikali, kwakweli viongozi lazima wawajibidhwe bila hivi amesha amesha hii itaondoa Imani ya wananchi Kwa chama chetu pendwa ambacho mpaka sasa hakina mpinzani
 
28 January 2024
Shinyanga mashahidi wanaogopa kutokea mahakamani,



View: https://m.youtube.com/watch?v=j85YDPfvJ0kRushwa nje nje kesi zinafutwa mashahidi hakuna, matatizo makubwa nchi hii .... Polisi inashutumiwa kupora fedha milioni 19 za mama, wamemtia kilema cha mguu na jeshi linajiburuza ... waziri mkuu Kassim Majaliwa alitoa maagizo uchunguzi wa kina kuhusu kesi hii lakini bado jeshi la Polisi ....
 
Mwenezi anaeneza porojo tu hakuna kitu chochote Tangible atafanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…