Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


WC,

Kila ulisomalo katika kitabu changu pamoja na hilo la katiba.
Kauli ya wazee wangu.

Narudia yote niliyoandika ni kauli toka kwa wazee wangu.

Hilo swali la katiba mimi halinishughulishi.

Ikiwa wewe unaona hilo ni jambo muhimu tafuta hizo katiba
na tuandikie utakayokuta humo ya manufaa.
 
Mzee Mohamed,
Ni lini utaitiwa angalau Udaktari wa Heshima kutoka vyuo hivi vinavyokuheshimu sana? Wanapewa watu wa hovyo kabisa hapa akina Mrema, Jakaya, Mengi, Mzindakaya, Nagu,...., halafu mtu muhimu kama wewe wanakuacha na maandishi yako wanayatumia na kukualika kila mara ukatoe mihadhara ya kisomi!
 

Mimi sialikwi nabembelezwa, kama ulikuwa hujui.

Unaongea pumba ambazo hazina tija kwenye huu mjadala. Wewe ni wakuwachwa tu kama ulivyo, huna la maana hata moja. Hivi una miaka mingapi weye? hivi wewe chuo gani umeshaalikwa? sidhani hata mtaani kwenu kukiwa kuna jambo kama unaalikwa kuongea seuse ya kuongea vyuoni.

Nakubaliana na Ritz alivyoku "describe".
 

Kuna wa hovyo zaidi ya dikteta? nae kishapewa.
 

Chako kimo? Hata Tanganyika library sijui kuna hata kijikaratasi chako mule wacha kitabu.

Uliingia kwenda kutafuta huko ulikoweka link ukatahayari.
 

N,

Ahsante sana kwa hiyo catalogue ya Library of Congress.

Hakika kitabu changu sasa hakipo katika catalogue.

Wala sitakwambia kuwa kilikuwapo maana tusiingie katika
mvutano mwingine.

Sasa na mimi nakupa ''title'' uiangalie kama ipo.

''Feats and Riot'' (1995) cha Jonathon Glassman.
Huyu ni mwalimu wa historia Northwestern University Chicago.

Kitabu chake kilikuwapo na sasa nimekitafuta hakipo.

Tunaweza Insha Allah kuendelea kuvitafuta na vitabu vingine
ambavyo mimi ninavyo katika maktaba yangu.

Hilo la ''facts'' mimi nishasema sina ugomvi na mtu si lazima
mtu aniamini.

Mimi Alhmdulilah lengo langu lilikuwa kuonyesha mchango wa
wazee wangu katika historia ya uhuru wa Tanganyika na
kwa kwa kweli nimefanikiwa pakubwa kuliko mategemeo yangu.

Tumo hapa JF wiki ya pili mnasikiza darsa yangu.
Dogo hilo?
 

Kwanini huzileti wewe ukamsuta kama kinachokuweka humu ni kusutana? wewe ndiye unaerusha tuhuma halafu unataka ushahidi aulete yeye? what a way of thinking.
 
Mzee Mohamed Said unaweza kutupatia historia fupi ya Mwl Cecil Motola
 
Last edited by a moderator:

Kipo kwa jina hilo hapo chini:

Feasts and riot : revelry, rebellion, and popular consciousness on the Swahili Coast, 1856-1888 / Jonathon Glassman.

Kuhusu suala zima la facts ni very simple facts are just facts, huwezi kuwa na facts zako, zangu na za atu tofauti katika kitu hicho hicho kimoja.

Mfano. Pg 126, kwenye kiabu chako kuhusu uchaguzi 1995.
"Nyerere as head of the powerful Christian lobby was campaigning for CCM candidate Mkapa. The Catholic Church supported Mkapa's campaign through Nyerere. In campaign tours up country Nyerere was hosted by the Catholic Church."
Utawezaje kuiita hiyo niliyo-highlight ni fact??????
 

M,

Sheikh Hassan bin Amir alifukuzwa nchi kwa shutuma za kutaka kupindua
serikali.

Halikadhalika wengi tu waliwekwa ndani kwa tuhuma hizo.

Kwa Dk. Mwanjisi lipi lilitangulia la ''kutoa mimba'' au ugomvi na Nyerere?
Kafungwa katoroka jela kakimbilia Kenya na asirudishwe Tanzania...

Kassanga Tumbo alikimbilia Mombasa na alirejeshwa.
Lakini haya yeshapita.
 
NCHI inaweza isiwe na katiba iliyoandikwa lakini sio CHAMA chochote kile hata hivi vya hiari lazima viwenayo. Na hakuna lisilo na manufaa ndani ya katiba. Hivi mtaongozana vipi? Mtachaguana vipi? Mtafanyaje vikao bila KATIBA?
Chimbuko na asili ya HISTORIA ya chama chochote kile ni KATIBA yake. Watu mkishakutana kwa madhumuni ya kuunda CHAMA ni lazima muanze na KATIBA. Usajili wenu ni lazima katiba iwepo. Uhalali wenu kukutana na kudai kitu chochote kile utatokana na katiba.
Anajitokeza mtu hapa anadai kuandika HISTORIA iliyosahaulika haigusi KATIBA. Anaandika UISLAM ambao haumo kwenye KATIBA! Aibu.
 

Ahsante kitabu nimekiona.

Kuwa Nyerere alikuwa mgeni wa Kanisa Katoliki mbona hilo dogo sana?
Hukuona mengine aliposema damu itamwagika?

Hii naomba uweke uzi mpya tujadili.
 
Kuna wa hovyo zaidi ya dikteta? nae kishapewa.
Yule alieachia madaraka kwa hiari yake? Huyo kapata nyingi tu sio moja. Kwa nini mzee wetu huyu anatutajia tu vyuo hivi halafu vyenyewe havionyeshi kumtambua?
 
Sema ugomvi na RAIS. Ugomvi na Mwalimu usingemfikisha hapo. Huyo Sheikh wako alirudishwa kwao. Hata akina Sykes wangejiingiza kwenye UDINI wangerudishwa kwao vilevile. Mwalimu hakuwa na mchezo na watu waliokuwa wakichezea KATIBA na SHERIA za NCHI. Hakujali DINI yako wala KABILA yako. Wala nafasi yako, hadhi yako katika jamii haikumsumbua Mwalimu.
 
Yule alieachia madaraka kwa hiari yake? Huyo kapata nyingi tu sio moja. Kwa nini mzee wetu huyu anatutajia tu vyuo hivi halafu vyenyewe havionyeshi kumtambua?

Kwa hiyari yake, kweli kabisa. Katuwacha kwenye tukiwa katika neema kubwa sana, barabara safi, chakula kingi, mafuta ya kumwaga, shule kibao, hospitali za kimataifa, elimu tuko juu katika afrika mashariki, uchumi tulikuwa tun reserve ya miaka 6 bot, katuwachia na BOT mpya nzuri, wizara ya mambo ya ndani mpya inang'aa.

Baada ya kututimizia hayo yote ndiyo akaamuwa kustaafu kwa hiyari yake.
 

Kumbe hawa waislam akina Ally (wakiwa mamluki) walikuwa wanamsaidia Mjerumani kwenye ukoloni wao wa kumkandamiza mtu mweusi? Je unasemaje kuhusu madai yako ya kuwa miaka hiyo, wakristo walikuwa wana-side na wakoloni, ila waislam walikuwa wanapinga ukoloni? Hapa umeonesha kuwa wazazi wa Sykes kumbe tayari walikuwa waislam wakati wakiwa mamluki... Of course, najua hii ume-reveal accidentally, you never intended to.
 
Kaacha madini yote ardhini, kaacha gas, kaacha wanyama wote mbugani, kaacha nchi imeenea misitu ya asili kila mahali, kaacha viwanda vingi vya umma, kaacha mabenki yote ya umma, kaacha kila kitu mikononi mwetu. Tukaanza kuvitafuna na kuvigombea kama mpira wa kona. Alijenga vyuo vikuu vya umma viwili, akajenga na vyuo vingine kama IDM, IFM, CBE, vyuo mifugo, waganga wasaidizi, walimu,....

Tutaanza kutafunana wenyewe hivi karibuni tu. Vuta subira.
 
Na kwa kukumbushia tu, ametuahidi atatuletea ushahidi mwingine kutoka kwa Chifu Mkwawa na akaahidi atatuletea historia ya Abushiri. Mpaka leo ana madeni kibao ya ahadi.

Naomba ajitokeze mtu ampe darsa la alama za unafik.

cc Yericko Nyerere

Alama za mnafiq tatu!

Moja wapo ni ile "akiweka ahadi hatimizi"

Prove us otherwise
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…