Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Gwalihenzi unachuki sana na uislamu na wala wewe sio wakwanza kuwa hivyo wameshapita mafirauni wakubwa kuliko wewe, wewe umesema huna dini uislamu unakuwashia nini?
Sheikh Farid, huna sababu za kutokwa na mapovu, hujakosea kabisa mimi siamini katika mungu wala dini zenu, lakini hilo halinizuii mimi kukemea mtu anapokuja na imani yake kutaka kuwakosesha amani na utangamano watu wengine. Mzee wako Mohamed Saidi anachochea chuki isiyo na maana kwa jina la uislam. Hiyo sio sahihi hata kidogo.
 
Mohamed, kipya ulicho kiandika katika ngano zako ni uislam wa wazee wako! hapo ndipo tunapishana na wewe. Wazee wako hawakupambana na wakoloni wakiwa wamejitenga kama waislam, walipambana na wakoloni wakiwa watanganyika na wakishirikiana na watanganyika wengine.
 

Inashangaza sana wewe unakuja na data na facts za kutosha halafu wao wanakuja na maneno matupu halafu wanataka kubishana.

Tatizo lao hakuna hata mmoja ambae anakuja na historia ya Tanganyika hawana wanachosubiri wewe uandike waanze kubisha bahati mbaya wanabisha bila ushahidi wowete.

Kinachotakiwa wewe ukiandika kitu kama ni uongo wao wanatakiwa waandike ukweli kukupinga lakini hawafanyi ivyo wanaishia kukuita mchochozi tu bila kuthibitisha.
 

Ami,

Nimesema Nyerere hakuasisi TANU Nyerere yu hai.
Sikuhofu kwa kuwa nilikuwa nasema ukweli.

Na nikamtaja Abdu Sykes na kueleza yote alofanya
hadi siku ile 7 Julai 1954 TANU ilipozaliwa.

Sikuwa naficha jina langu katika makala zangu kama
unavyoona hapa JF.

Huu ndiyo msimamo wangu siku zote.
Siogopi kusema kweli.
 
Ritz,

Ukisikia hana dini basi jua ni mpenzi wa Ukristo.
Nimekutana na wengi sampuli hiyo.

Mambo ya kizamani kabisa kujinasibu na ukafiri.

Anajiumiza bure nafsi yake huwezi kuwa na chuki na Waislam 2.1 billion,
 

Ritz,

Haya ndiyo ya akina Abdulrahman Babu.
Miaka mingi iliyopita nilikuwa na Babu Brixton.

Hiki ni kitongoji nje ya London.

Siku nzima tulishinda kule na kwangu ilikuwa
ndiyo mara ya kwanza nafahamiananae.

Nikamsihi sana aandike historia ya mapinduzi
ya Zanzibar.

Siku hizo nikiamini zile stori za Umma Party kuwa
ndio walopindua.

Miaka mingi baadae nikafika Kipumbwi kwa jicho
langu nikashuhudia kambi walikotoka Wamakonde
kwenda Zanzibar kupindua.

Ndiyo hawa ndugu zetu wameivaa historia ya Kivukoni
hadi ikawaganda na ngozi.

Leo imekuwa tabu kuivua.
 

Umesema kweli Gwalihenzi.

Ila ilipokuja kuandikwa historia ya uhuru...
Wazee wangu wakafutwa,

Akabakishwa Nyerere peke yake.
Hiki ndicho kilichoniudhi.
 

G,

Kusema kweli ndiyo uchochezi?
Mbons humlaumu Sivalon?

Au unataka nikuwekee hapa maneno
yake?
 
Umesema kweli Gwalihenzi.

Ila ilipokuja kuandikwa historia ya uhuru...
Wazee wangu wakafutwa,

Akabakishwa Nyerere peke yake.
Hiki ndicho kilichoniudhi.
Sema historia ya uhuru iliyoandikwa na CCM kivukoni! mbona waandishi wengine hawajafuta. Sasa wewe umekuja na histohisia zaidi badala ya historia na ndio maana huwa tunakushangaa kwa nini hukwenda kumhoji Nyerere mweenyewe alipokuwa hai ili kujilidhisha na simlizi za wazee wako. Au na wewe ulibeba chuki dhidi ya Nyerere? Haiingii akilini kabisa kumuacha mchezaji mkuu na ukawakumbatia watazamaji.
 
Ritz,

Ukisikia hana dini basi jua ni mpenzi wa Ukristo.
Nimekutana na wengi sampuli hiyo.

Mambo ya kizamani kabisa kujinasibu na ukafiri.
Hizo ni hisia zako binafsi wala hazinidhuru mimi. Kinacho nidhuru ni uchochezi wako wa kidini unaopelekea kuvunja amani yetu. Mimi ni ATHEIST kwahiyo mungu wako au mungu wa kikrsto hanihusu hata kidogo. Amani ya taifa letu inanihusu sana.
 
Hapana, adui yangu ni yule anayeutumia uislam wake au dini yake nyingine kwa nia ya kuwafarakanisha watanzania.

Wakati mwingine uwe unajisoma unachoandika dhidi ya Waislam, si wewe ndiyo uwa unakejeli kwa Waislam wana akili za madrasa. Madrasa na inauhusiano gani na historia ya Tanganyika.
 
Hizo ni hisia zako binafsi wala hazinidhuru mimi. Kinacho nidhuru ni uchochezi wako wa kidini unaopelekea kuvunja amani yetu. Mimi ni ATHEIST kwahiyo mungu wako au mungu wa kikrsto hanihusu hata kidogo. Amani ya taifa letu inanihusu sana.

Wewe unasema ni ATHEIST mtu ambaye anaamini kwamba hakuna Mungu, mkanamungu.

Sasa hiyo amani unayosema itatoka wapi bila Mungu.

Wewe ni ATHEIST halafu unaogopa Uislam kuwa unaleta uchochezi uoni kama unajichanganya.
 
Mnanipa Raha......Japo sina la kuchangia kwa sasa katika Uzi huu lakini ni jambo la Faraja kujua Historia iliyojificha...na hili ndilo tatizo la Tanzania kila kitu 'Usanii' Watu wabinafsi sana....!!!!!!??????
 
Hapana, adui yangu ni yule anayeutumia uislam wake au dini yake nyingine kwa nia ya kuwafarakanisha watanzania.

Kichekesho kingine ATHEIST anazihofia dini zingine zinaweza kuleta machafuko kupitia dini zao.
 
Wakati mwingine uwe unajisoma unachoandika dhidi ya Waislam, si wewe ndiyo uwa unakejeli kwa Waislam wana akili za madrasa. Madrasa na inauhusiano gani na historia ya Tanganyika.
Ritz, wacha kunizulia, ebu nionesha ni wapi nilipotoa kejeli hizo!
 
Hizo ni hisia zako binafsi wala hazinidhuru mimi. Kinacho nidhuru ni uchochezi wako wa kidini unaopelekea kuvunja amani yetu. Mimi ni ATHEIST kwahiyo mungu wako au mungu wa kikrsto hanihusu hata kidogo. Amani ya taifa letu inanihusu sana.

G,

Nakuwekea tena maneno ya Sivalon na unijibu Insha Allah:

The second book is by Dr John C. Sivalon, who in his expose, Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi 1985, [1] unmasks a conspiracy in the government to subvert Islam.

Sivalon revealed that the Catholic Church as far back as 1961 was worried by two prospects. First, was the unity between the Muslim madhheb (sect) of Sunni, Bohora, Ismailia and Ithnasheri in Tanganyika; and the second, was the transfer of the headquarters of the East African Muslim Welfare Society (EAMWS) from Mombasa to Dar es Salaam.

The Church was worried that the resources in the hands of rich Asian Muslim community in East Africa, coupled with the political power of African Muslims, particularly in Tanganyika, would endanger Christian interests in East Africa.

The Church therefore declared Islam as its enemy in the country and plotted to thwart its progress.[2]


[1] John C. Sivalon, Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi 1985, (Ndanda, 1992).
[2] Ibid. p 37.

Hapa sijaweka Bergen wala Njozi.

Kanisa limetahayari liko kimya wewe usie na dini ndiye unawajibia hii hamu kubwa sana ya kutaka kulijibia Kanisa inaletwa na nini?

Kwa nini huliulizi Kanisa ukweli wa haya yalosemwa?

Unalo?
 

Mzee Said hakuna hata mahali hata pamoja ambapo miye naleta viroja. Viroja ninavyoona ni vile vya kwako. Unazungumza kama unataka utambulike kwa utafiti ulioufanya. Baati mbaya sana wenzako wakikuuliza kuhusu "utafiti" huo unaruka. Unatoa madai tunakuuliza utujuze unakwepa; una kile ambacho naweza kukiita ni intellectual arrogance ya kuamini kuwa ulichosema wewe ni neno lisiloulizwa, lisilohojiwa, na lisilopingwa. Umejiaminishha kichwani mwako kuwa ulicohsema ni 'kweli' na kuwa ni kweli si kwa sababu ya ushahidi uliopo bali ni kwlei kwa sababu wewe umesema. Hivyo, watu hawahitaji kukuulizwa, hawahitaji kufafanuliwa, na hawahitaji kukusahihisha. Unaamini kuwa ukikubali kusahihishwa au kusahihisha histohisia yako au lugha unayotumia basi unajidhalilisha.

Mchango wako ni mkubwa sana katika kuelewa kwa kiasi harakati za Uhuru; kwa kweli miye nimekipenda kitabu chako (na nimekisoma) kwa sababu moja kubwa. Kinathibitisha kuwa Nyerere ndiye alikuwa kinara wa harakati za Uhuru. Mashujaa wengine wote ambao unawataja walimzunguka shujaa huyu.
 
Heshima sana DULLAH MSAVIVOR ,

Kwanza lazima nikupongeza kwa mafanikio yako ambayo yametokana na juhudi zako mwenyewe ni dhahiri jitihada zako zimekufikisha hapo ulipo.Kupitia andiko lako mwenyewe umedhihirisha NECTA hakuna uonevu wala mfumo kristo unaopigiwa upatu na watu wasiotaka kushughulisha akili zao haupo kabisa.Ukisoma vizuri hakuna wa kukuzuia,ukibangaiza utaishia kuwachora kina Messi na Zombie.....



 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…