Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Gwalihenzi unachuki sana na uislamu na wala wewe sio wakwanza kuwa hivyo wameshapita mafirauni wakubwa kuliko wewe, wewe umesema huna dini uislamu unakuwashia nini?
Sheikh Farid, huna sababu za kutokwa na mapovu, hujakosea kabisa mimi siamini katika mungu wala dini zenu, lakini hilo halinizuii mimi kukemea mtu anapokuja na imani yake kutaka kuwakosesha amani na utangamano watu wengine. Mzee wako Mohamed Saidi anachochea chuki isiyo na maana kwa jina la uislam. Hiyo sio sahihi hata kidogo.
 
G,

Nyie hamuulizi kujua mnauliza kubisha.
Mie kama maswali nimejibu siku nyingi.

Mmefadhaika na kitabu changu kwa kuwa
kimekuleteeni mambo mapya.

Hizo post kutoka "Under the Shadow of
British Colonialism" kote nilikohadhir
kilichofatia ni kuombwa nizidi kueleza hiki
au kile.

Nyie mmepigwa na butwa.

Isizidi Mwanakijiji anasoma kisha chembelecho
Zomba anakuja na viroja na kutaka ati nimjibu.

Viroja vinajibika?
Mohamed, kipya ulicho kiandika katika ngano zako ni uislam wa wazee wako! hapo ndipo tunapishana na wewe. Wazee wako hawakupambana na wakoloni wakiwa wamejitenga kama waislam, walipambana na wakoloni wakiwa watanganyika na wakishirikiana na watanganyika wengine.
 
Inashangaza sana wewe unakuja na data na facts za kutosha halafu wao wanakuja na maneno matupu halafu wanataka kubishana.

Tatizo lao hakuna hata mmoja ambae anakuja na historia ya Tanganyika hawana wanachosubiri wewe uandike waanze kubisha bahati mbaya wanabisha bila ushahidi wowete.

Kinachotakiwa wewe ukiandika kitu kama ni uongo wao wanatakiwa waandike ukweli kukupinga lakini hawafanyi ivyo wanaishia kukuita mchochozi tu bila kuthibitisha.
 
Kuchosha kwako kuko hapa.Utetezi wako ni wa kibaguzi.Unataka Nyerere apewe haki yake ambayo hata hivyo hakunyimwa lakini haki za wapigania uhuru wengine huna habari nazo.
Uadui na uchoyo wa Nyerere kwa wapigania uhuru wengine na kwa waislamu wa kawaida ndio haki yake ambayo amepewa kikamilifu katika historia ya Mohammed Said.
Kwa upande wako mwenyewe ni mjanja sana katika mijadala kutokana na uzoefu wako wa muda mrefu.Lakini hujui kuwa kunguru mjanja hunaswa na tundu bovu.
Tabia yako ni kuwa vumbi likitimka hapa unajificha.Ukirudi hujibu chochote cha maana ulichoulizwa.Unazusha maswali ambayo huko nyuma yameshajibiwa.
Kama ni kutokutoa haki basi wewe unaongoza,na si hivyo tu bali wewe ni mtovu wa nidhamu kwa tafiti za kielimu.Mtu kama Mohammed Saidi aliyetumia miaka na kuwasilisha mahojioni halisi na wapigania uhuru wewe unaita ni simulizi.
Mzee Mwanakijiji huna heshima kabisa na kazi za kitafiti ambazo zimeshathaminiwa na mamlioni ya watu nje na ndani ya nchi.
Kwa kutoweza kuleta utetezi wa maana kupinga historia ya Mohammed Said huoni kwamba unajitukana mwenyewe?.
Fuata ushauri wa Barubaru iwapo umeishiwa au umechoka basi tulia usome tu michango ya wenzako.

Ami,

Nimesema Nyerere hakuasisi TANU Nyerere yu hai.
Sikuhofu kwa kuwa nilikuwa nasema ukweli.

Na nikamtaja Abdu Sykes na kueleza yote alofanya
hadi siku ile 7 Julai 1954 TANU ilipozaliwa.

Sikuwa naficha jina langu katika makala zangu kama
unavyoona hapa JF.

Huu ndiyo msimamo wangu siku zote.
Siogopi kusema kweli.
 
Ritz,

Ukisikia hana dini basi jua ni mpenzi wa Ukristo.
Nimekutana na wengi sampuli hiyo.

Mambo ya kizamani kabisa kujinasibu na ukafiri.

Anajiumiza bure nafsi yake huwezi kuwa na chuki na Waislam 2.1 billion,
 
Inashangaza sana wewe unakuja na data na facts za kutosha halafu wao wanakuja na maneno matupu halafu wanataka kubishana.

Tatizo lao hakuna hata mmoja ambae anakuja na historia ya Tanganyika hawana wanachosubiri wewe uandike waanze kubisha bahati mbaya wanabisha bili ushahidi.

Kinachotakiwa wewe ukiandika kitu kama ni uongo wao wanatakiwa waandike ukweli kukupinga lakini hawafanyi ivyo wanaishia kukuita mchochozi tu bila kuthibitisha.

Ritz,

Haya ndiyo ya akina Abdulrahman Babu.
Miaka mingi iliyopita nilikuwa na Babu Brixton.

Hiki ni kitongoji nje ya London.

Siku nzima tulishinda kule na kwangu ilikuwa
ndiyo mara ya kwanza nafahamiananae.

Nikamsihi sana aandike historia ya mapinduzi
ya Zanzibar.

Siku hizo nikiamini zile stori za Umma Party kuwa
ndio walopindua.

Miaka mingi baadae nikafika Kipumbwi kwa jicho
langu nikashuhudia kambi walikotoka Wamakonde
kwenda Zanzibar kupindua.

Ndiyo hawa ndugu zetu wameivaa historia ya Kivukoni
hadi ikawaganda na ngozi.

Leo imekuwa tabu kuivua.
 
Mohamed, kipya ulicho kiandika katika ngano zako ni uislam wa wazee wako! hapo ndipo tunapishana na wewe. Wazee wako hawakupambana na wakoloni wakiwa wamejitenga kama waislam, walipambana na wakoloni wakiwa watanganyika na wakishirikiana na watanganyika wengine.

Umesema kweli Gwalihenzi.

Ila ilipokuja kuandikwa historia ya uhuru...
Wazee wangu wakafutwa,

Akabakishwa Nyerere peke yake.
Hiki ndicho kilichoniudhi.
 
Sheikh Farid, huna sababu za kutokwa na mapovu, hujakosea kabisa mimi siamini katika mungu wala dini zenu, lakini hilo halinizuii mimi kukemea mtu anapokuja na imani yake kutaka kuwakosesha amani na utangamano watu wengine. Mzee wako Mohamed Saidi anachochea chuki isiyo na maana kwa jina la uislam. Hiyo sio sahihi hata kidogo.

G,

Kusema kweli ndiyo uchochezi?
Mbons humlaumu Sivalon?

Au unataka nikuwekee hapa maneno
yake?
 
Umesema kweli Gwalihenzi.

Ila ilipokuja kuandikwa historia ya uhuru...
Wazee wangu wakafutwa,

Akabakishwa Nyerere peke yake.
Hiki ndicho kilichoniudhi.
Sema historia ya uhuru iliyoandikwa na CCM kivukoni! mbona waandishi wengine hawajafuta. Sasa wewe umekuja na histohisia zaidi badala ya historia na ndio maana huwa tunakushangaa kwa nini hukwenda kumhoji Nyerere mweenyewe alipokuwa hai ili kujilidhisha na simlizi za wazee wako. Au na wewe ulibeba chuki dhidi ya Nyerere? Haiingii akilini kabisa kumuacha mchezaji mkuu na ukawakumbatia watazamaji.
 
Ritz,

Ukisikia hana dini basi jua ni mpenzi wa Ukristo.
Nimekutana na wengi sampuli hiyo.

Mambo ya kizamani kabisa kujinasibu na ukafiri.
Hizo ni hisia zako binafsi wala hazinidhuru mimi. Kinacho nidhuru ni uchochezi wako wa kidini unaopelekea kuvunja amani yetu. Mimi ni ATHEIST kwahiyo mungu wako au mungu wa kikrsto hanihusu hata kidogo. Amani ya taifa letu inanihusu sana.
 
Hapana, adui yangu ni yule anayeutumia uislam wake au dini yake nyingine kwa nia ya kuwafarakanisha watanzania.

Wakati mwingine uwe unajisoma unachoandika dhidi ya Waislam, si wewe ndiyo uwa unakejeli kwa Waislam wana akili za madrasa. Madrasa na inauhusiano gani na historia ya Tanganyika.
 
Wewe unasema ni ATHEIST mtu ambaye anaamini kwamba hakuna Mungu, mkanamungu.

Sasa hiyo amani unayosema itatoka wapi bila Mungu.

Wewe ni ATHEIST halafu unaogopa Uislam kuwa unaleta uchochezi uoni kama unajichanganya.
 
Mnanipa Raha......Japo sina la kuchangia kwa sasa katika Uzi huu lakini ni jambo la Faraja kujua Historia iliyojificha...na hili ndilo tatizo la Tanzania kila kitu 'Usanii' Watu wabinafsi sana....!!!!!!??????
 
Hapana, adui yangu ni yule anayeutumia uislam wake au dini yake nyingine kwa nia ya kuwafarakanisha watanzania.

Kichekesho kingine ATHEIST anazihofia dini zingine zinaweza kuleta machafuko kupitia dini zao.
 
Wakati mwingine uwe unajisoma unachoandika dhidi ya Waislam, si wewe ndiyo uwa unakejeli kwa Waislam wana akili za madrasa. Madrasa na inauhusiano gani na historia ya Tanganyika.
Ritz, wacha kunizulia, ebu nionesha ni wapi nilipotoa kejeli hizo!
 
Hizo ni hisia zako binafsi wala hazinidhuru mimi. Kinacho nidhuru ni uchochezi wako wa kidini unaopelekea kuvunja amani yetu. Mimi ni ATHEIST kwahiyo mungu wako au mungu wa kikrsto hanihusu hata kidogo. Amani ya taifa letu inanihusu sana.

G,

Nakuwekea tena maneno ya Sivalon na unijibu Insha Allah:

The second book is by Dr John C. Sivalon, who in his expose, Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi 1985, [1] unmasks a conspiracy in the government to subvert Islam.

Sivalon revealed that the Catholic Church as far back as 1961 was worried by two prospects. First, was the unity between the Muslim madhheb (sect) of Sunni, Bohora, Ismailia and Ithnasheri in Tanganyika; and the second, was the transfer of the headquarters of the East African Muslim Welfare Society (EAMWS) from Mombasa to Dar es Salaam.

The Church was worried that the resources in the hands of rich Asian Muslim community in East Africa, coupled with the political power of African Muslims, particularly in Tanganyika, would endanger Christian interests in East Africa.

The Church therefore declared Islam as its enemy in the country and plotted to thwart its progress.[2]

[1] John C. Sivalon, Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi 1985, (Ndanda, 1992).
[2] Ibid. p 37.

Hapa sijaweka Bergen wala Njozi.

Kanisa limetahayari liko kimya wewe usie na dini ndiye unawajibia hii hamu kubwa sana ya kutaka kulijibia Kanisa inaletwa na nini?

Kwa nini huliulizi Kanisa ukweli wa haya yalosemwa?

Unalo?
 
G,

Nyie hamuulizi kujua mnauliza kubisha.
Mie kama maswali nimejibu siku nyingi.

Mmefadhaika na kitabu changu kwa kuwa
kimekuleteeni mambo mapya.

Hizo post kutoka "Under the Shadow of
British Colonialism" kote nilikohadhir
kilichofatia ni kuombwa nizidi kueleza hiki
au kile.

Nyie mmepigwa na butwa.

Isizidi Mwanakijiji anasoma kisha chembelecho
Zomba anakuja na viroja na kutaka ati nimjibu.

Viroja vinajibika?

Mzee Said hakuna hata mahali hata pamoja ambapo miye naleta viroja. Viroja ninavyoona ni vile vya kwako. Unazungumza kama unataka utambulike kwa utafiti ulioufanya. Baati mbaya sana wenzako wakikuuliza kuhusu "utafiti" huo unaruka. Unatoa madai tunakuuliza utujuze unakwepa; una kile ambacho naweza kukiita ni intellectual arrogance ya kuamini kuwa ulichosema wewe ni neno lisiloulizwa, lisilohojiwa, na lisilopingwa. Umejiaminishha kichwani mwako kuwa ulicohsema ni 'kweli' na kuwa ni kweli si kwa sababu ya ushahidi uliopo bali ni kwlei kwa sababu wewe umesema. Hivyo, watu hawahitaji kukuulizwa, hawahitaji kufafanuliwa, na hawahitaji kukusahihisha. Unaamini kuwa ukikubali kusahihishwa au kusahihisha histohisia yako au lugha unayotumia basi unajidhalilisha.

Mchango wako ni mkubwa sana katika kuelewa kwa kiasi harakati za Uhuru; kwa kweli miye nimekipenda kitabu chako (na nimekisoma) kwa sababu moja kubwa. Kinathibitisha kuwa Nyerere ndiye alikuwa kinara wa harakati za Uhuru. Mashujaa wengine wote ambao unawataja walimzunguka shujaa huyu.
 
Heshima sana DULLAH MSAVIVOR ,

Kwanza lazima nikupongeza kwa mafanikio yako ambayo yametokana na juhudi zako mwenyewe ni dhahiri jitihada zako zimekufikisha hapo ulipo.Kupitia andiko lako mwenyewe umedhihirisha NECTA hakuna uonevu wala mfumo kristo unaopigiwa upatu na watu wasiotaka kushughulisha akili zao haupo kabisa.Ukisoma vizuri hakuna wa kukuzuia,ukibangaiza utaishia kuwachora kina Messi na Zombie.....

Mama yangu nakumbuka wakati nipo shule ya msingi,alikua ananihusia mara kwa mara,Dullah hakikisha unaisoma vema na kujitahid kuihifadhi na kuilewa vyema Qur an kwani ndio msingi wa maisha yako na chakula cha ubongo wako,hata siku moja usizembee kwenda madrasa kujifunza,huku akiwa ananisimamia katika masomo yangu ya shule ya msingi kimasikini katika hizi ST KANUMBA,,shule zetu hizi walalahoi,,

Alikua ananiambia jitahid pia huko shule kuzingatia masomo kwani ukishindwa hapo mimi sina uwezo wa kukupeleka Private school,na alikua ananiambia Dawa ya hiyo hali yako ni kupiga shule na kuchimba maradufu ya wenzako,niliyafanyia kazi kweli kweli,nakumbuka Mtihani wa kumaliza Darasa la saba,hesabu nilipiga 50/50,lugha nikapiga 48/50,Maarifa ya jamii nikapiga 46/50 na nikachaguliwa kwenda Mzumbe high school(Special schoool),,

Kazi sasa ilikua mara baada ya kufika mzumbe high school enzi hizo kile chuo kikuu cha mzumbe kikitambuliwa kwa jina la IDM-MZUMBE,,

Bahati pale mzumbe high school kuna msikit uliojengwa karibu na shule na upo maeneo ya shule,nilishangazwa sana kipindi tunafika pale,ile ni shule ya serikali lakini idadi ya waislam ilikua ni ya kuhesabika,katika wanafunzi tulioripoti form one kwa idadi ya 105 waislam tulikua hatufiki hata 20,na ukiangalia kwa undani hata hao wakristo tulioripoti nao si kwamba walikua imara kias cha kusema walistahiki sana kuwepo pale,

Tulichokawa tunafanya sisi ni kuvaa vipedo kama wanavosema na kupiga kitabu kwa kwenda mbele,tuliwaprove wrong hasa katika National results,tukaambiana jaman mnajua hawa siku zote wanatusemanga ya kwamba sisi si chochote si lolote,kwaiyo tunawathibitishie,

National results zikija ni mwendo wa Div one tuh za single digit,div1 point 7,point 8,poit 9 na vipedo vyetu,

Hadi kuna kipindi wakristo wakaanza zengwe ya kwamba ooooh waislam wanashinda sana msikitini,hawafanyi kazi za shule,hawaudhurii roll call etc,mkuu wa shule Mzee R.J Mwasha akawaambia as long as hao jamaa wananipa matokeo mazuri mimi sion umuhim wa allegations zenu,ikawa kila mwaka ukifika tunaambukizana ile hali na hadi leo tumeuacha utamaduni huo katika shule kama ile,,

Sio kweli kwamba waislam hawazingatii shule,yapo mengi sana watu tunafanyiwa na tumefanyiwa,tunazungumza tunazungumza kwa mantiki ya kukemea na kujenga tanzania bora kwa kizazi kijacho,sasa kama watu hawataki ukweli usemwe ni juu yao..

Ukweli utasemwa tuh..
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom