Mama yangu nakumbuka wakati nipo shule ya msingi,alikua ananihusia mara kwa mara,Dullah hakikisha unaisoma vema na kujitahid kuihifadhi na kuilewa vyema Qur an kwani ndio msingi wa maisha yako na chakula cha ubongo wako,hata siku moja usizembee kwenda madrasa kujifunza,huku akiwa ananisimamia katika masomo yangu ya shule ya msingi kimasikini katika hizi ST KANUMBA,,shule zetu hizi walalahoi,,
Alikua ananiambia jitahid pia huko shule kuzingatia masomo kwani ukishindwa hapo mimi sina uwezo wa kukupeleka Private school,na alikua ananiambia Dawa ya hiyo hali yako ni kupiga shule na kuchimba maradufu ya wenzako,niliyafanyia kazi kweli kweli,nakumbuka Mtihani wa kumaliza Darasa la saba,hesabu nilipiga 50/50,lugha nikapiga 48/50,Maarifa ya jamii nikapiga 46/50 na nikachaguliwa kwenda Mzumbe high school(Special schoool),,
Kazi sasa ilikua mara baada ya kufika mzumbe high school enzi hizo kile chuo kikuu cha mzumbe kikitambuliwa kwa jina la IDM-MZUMBE,,
Bahati pale mzumbe high school kuna msikit uliojengwa karibu na shule na upo maeneo ya shule,nilishangazwa sana kipindi tunafika pale,ile ni shule ya serikali lakini idadi ya waislam ilikua ni ya kuhesabika,katika wanafunzi tulioripoti form one kwa idadi ya 105 waislam tulikua hatufiki hata 20,na ukiangalia kwa undani hata hao wakristo tulioripoti nao si kwamba walikua imara kias cha kusema walistahiki sana kuwepo pale,
Tulichokawa tunafanya sisi ni kuvaa vipedo kama wanavosema na kupiga kitabu kwa kwenda mbele,tuliwaprove wrong hasa katika National results,tukaambiana jaman mnajua hawa siku zote wanatusemanga ya kwamba sisi si chochote si lolote,kwaiyo tunawathibitishie,
National results zikija ni mwendo wa Div one tuh za single digit,div1 point 7,point 8,poit 9 na vipedo vyetu,
Hadi kuna kipindi wakristo wakaanza zengwe ya kwamba ooooh waislam wanashinda sana msikitini,hawafanyi kazi za shule,hawaudhurii roll call etc,mkuu wa shule Mzee R.J Mwasha akawaambia as long as hao jamaa wananipa matokeo mazuri mimi sion umuhim wa allegations zenu,ikawa kila mwaka ukifika tunaambukizana ile hali na hadi leo tumeuacha utamaduni huo katika shule kama ile,,
Sio kweli kwamba waislam hawazingatii shule,yapo mengi sana watu tunafanyiwa na tumefanyiwa,tunazungumza tunazungumza kwa mantiki ya kukemea na kujenga tanzania bora kwa kizazi kijacho,sasa kama watu hawataki ukweli usemwe ni juu yao..
Ukweli utasemwa tuh..