Haya wale wafia dini
Habari na Khamis Amani, Zanzibar -- BAADA ya mahakama ya mkoa Vuga kumwachilia huru mwalimu wa madrasat Qadiria iliyopo Amani wilaya ya Mjini Unguja, aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kumlawiti mwanafunzi wake wa kiume wa miaka 11, hatimaye mahakama kuu ya Zanzibar imemfunga jela miaka 15.
Uamuzi huo wa mahakama umekuja kufuatia rufaa iliyowasilishwa mahakamani hapo na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), kupinga hukumu iliyotolewa na mahakama ya Mkoa.
Mahakama hiyo, chini ya Jaji Abdulhakim Ameir Issa imelazimika kutoa adhabu hiyo baada ya kuridhika na sababu za rufaa zilizowasilishwa na DPP, ambazo zilidai kuwa Mahakama ya Mkoa wa Vuga imekosea kisheria katika utoaji wa hukumu. Hivyo, baada ya kusikiliza kwa kina hoja za pande mbili hizo juu ya rufaa hiyo pamoja na kuangalia vielelezo vya ushahidi vilivyotolewa katika mahakama ya mkoa wakati wa usikilizwaji wa kesi ya msingi, Jaji Abdulhakim alisema:
Mahakama inatengua uamuzi wa mahakama ya mkoa kwa sababu ilikosea kisheria katika utoaji wake wa hukumu, hivyo mahakama hii inaamuru kutumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka 15, haki ya rufaa ipo wazi kwa upande ambao haukuridhika na uamuzi huu
Pamoja na adhabu hiyo, Jaji Abdulhakim alimtaka Ustaadh huyo kulipa fidia ya shilingi 500,000 kwa mtoto huyo aliyemfanyia kitendo hicho.
Soma zaidi habari hii kwenye: ZanziNews blog
Haya kisa hicho kwa upande wa Shilingi!