Uchumi wa Kati: Waziri wa Viwanda, Kitila Mkumbo azindua tela la kubeba mizigo

Uchumi wa Kati: Waziri wa Viwanda, Kitila Mkumbo azindua tela la kubeba mizigo

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Mh Kitila Mkumbo amezindua tela bora lenye uwezo wa kubeba mizigo ya hadi tani 5 lilotengenezwa Nchini Tanzania .

Ubora wa tela hilo umethibishwa na Shirika la viwango nchini Tanzania TBS

FB_IMG_1625768848689.jpg


E51fXOiXIAAjbxi.jpg
E51fXOgXsAMbucL.jpg


==========

Nimesoma hii Habari ;
"Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo amezindua Tela la kubeba mizigo lililotengenezwa Tanzania na Kiwanda cha Kuzalisha vipuri na mashine (KMTC) kwa ushirikiano na Taasisi za NDC, CAMARTEC na TEMDO,lenye uwezo wa kubeba uzito wa tani 5 za mizigo."

Nilibaki najiuliza hivi bado sekta ya viwanda na biashara ipo serious?. Yaani waziri mzima anatengeneza headline ya kuzindua hilo Tela!. Bado tuko kulekule kwenye concept ya Tanzania ya Viwanda.

Hapo sasa anazindua nini?, ni kama innovation au invention imefanyika mpaka anakuja Waziri wa Viwana wa Tanzania nzima kuja kuzindua hiyo kitu.

Hata wenzetu walioendelea si ni aibu kwetu wakiona hizi habari. Hii ni atleast angekuja tu afisa biashara wa manispaa kuzindua (au ndo kuipiga promo bidhaa).

Nashauri dhana ya Viwanda na ubunifu ungekuja na creativity za ukweli ndipo waziri ama kiongozi mkubwa kabisa katika sekta kuja kumake headlines kama hizi.
 
Maswali Muhimu:

Je ni bora kuliko mengine yaliyopo sokomi?
Na Gharama yake ni ndogo kuliko mengine ?
Uhitaji je, hii ni efficient kuliko ubebaji mwingine ?

Kama majibu ni ndio basi ni vema....
 
Sio kituo cha uuzaji na mikopo kwa wakulima zana za kilimo kweli hapo??
 
Mh Kitila Mkumbo amezindua tela bora lenye uwezo wa kubeba mizigo ya hadi tani 5 lilotengenezwa Nchini Tanzania .

Ubora wa tela hilo umethibishwa na Shirika la viwango nchini Tanzania TBS

View attachment 1846239
Trailer hizo cha mtoto.
SIDO tupu, nikifikiri kitu cha maana, you are not serious, 5 TONS unapigia jaramba?
 
Back
Top Bottom