Inashangaza sana pale ambapo kupanda kwa bei za vitu kunahusishwa na kufungua nchi, mfano; mazao kuuzwa nje ya nchi kulilenga kuongeza pato kwa mkulima, lakini ajabu bei ya mbolea nayo inapanda kila siku, sasa hapa kuna haja gani ya kuhangaika kuzunguka dunia yote kwa kisingizio cha kufungua nchi wakati hapa ndani mambo ndio kwanza yanazidi kujifunga?
Namshauri Rais aache kufanya kazi kwa kukariri, habari ya kufungua nchi sasa imeshafeli; kuna tatizo kubwa sana la ukosefu wa ajira, halafu on top of that gharama za maisha zinazidi kupanda, atulie chini na wataalamu wa uchumi wamuoneshe namna mambo yanavyotakiwa kwenda, kuliko kuendelea kupanda ndege kila siku wakati impact ya hizo safari zake kwa mtanzania wa kawaida ni zero.
Kikwete licha ya kupanda ndege miaka yake yote bado uchumi wa nchi ulikuwa mbaya na nchi ikageuzwa shamba la bibi, huu ushauri anaopewa ni vyema sasa atulie chini achanganye na zake, atuoneshe yeye kama yeye ana kitu gani kwenye kichwa chake, anataka kuiona Tanzania inaelekea wapi kwa mipango mipya ipi, sio hii ya kufungua nchi kila siku na kuhutubia kila aendako huku mambo yetu ndani yanazidi kuwa magumu.