Kwenye food security ni rahisi kwa sababu tayari tuna NFRA. Cha kufanya ni kuhakikisha inawajibika katika najukumu yake ipasavyo. Ikiwezekana iundwe upya kwa kupeleka mswada bungeni na kupeleka watu wenye sifa na wanaoweza kuchapa kazi na kuhakikisha nchi ina akiba ya kutosha ya chakula kwa ajili ya kusupply kwenye uchumi pale panapotokea uhaba.
NRFA anahifadhi nafaka na hasa mahindi na hana uwezo wa maghala kuhifadhi mahindi say kama nchi ina njaa, NRFA ana uhakika wa kutoa mahindi kwa watanzania mil 60.
Food security ni usalama na uhakika wa chakula. Kuna nyakati mafuta ya kula (hasa mfungo wa ramadhani ukikaribia) yakipotea week 2 tu, panakuwa hapatoshi.
Kama kuna eneo kama nchi hatujafanya homework ya kutosha ni food security iwe treated kama national security agenda ambayo sio tu ita-drain mfuko mkuu ila itatunisha mfuko mkuu, ku-cut down imports, kuongeza exports, kupanua tax base, kuongeza mzunguko.
Kuna eneo public sector (mamlaka) haijataka ku-stretch ili kutumia financial instruments kukuza biashara. Bila kufanya biashara na kutengeneza mzunguko uchumi hauwezi kutanuka.
Uchumi bila uzalishaji na kudhibiti ongezeko la thamani kwenye mazao ya kilimo unakuwa ni hadithi, analytics then hamna cha ziada.
Mtoa hoja ana ushauri mzuri sana, bila shaka wenye mamlaka watamtafuta kukaa nae na ku-extract nini kaona, nini anawaza ili nini tufanye.
Kama mtoa hoja angetoa neno lisilo na staha kwa "wakubwa" bila shaka angetafutwa kwa juhudi na nguvu kubwa sana ili ajieleze na ikiwezekana afike mbele ya pilato.
Ila mambo ya kujenga, hawa wasaidizi wa wakubwa huwa wanaona as if sio jambo lao.
Kama mvua zitachelewe kunyesha, au zikawa hafifu, sipati picha "kilio na malalamiko" yatakayofuata. Ila kwanini tusijifunze kwa falasafa ya Farao na Yusuf kuwa na national food reserve system wakati wa neema ili siku hali ikigeuka, Tanzania haitetereki kwenye usalama wa chakula. Chakula sio nafaka pekee (ambayo ndio major task ya NRFA)
Kuna lots should be done ili Watanzania wawe na uwezo wa kuzalisha na kula aina zote za vyakula.