Uchumi wetu unaweza kuanza kuanguka mwishoni mwa 2023: Rais Samia anahitaji "National Security Advisor" aliyebobea sana

Hao watu wachapa kazi,na wenye weredi wanatoka sayari nyingine? Huo muswada unaenda bunge lipi ambalo hua halisahau hata sheria lilizo pitisha.
 
Dah mimi heka zangu 7 tu naziangalia sijapanda chochote mpk sasa hv...hii hali inatishia kwakweli, mama akusikie tu
 
Aruhusu Fao la kujitoa mzunguko wa fedha urudi kama kipindi cha JK .
Kujiajiri kutaongeza mzunguko
Nani alikuambia fao la kujitoa litaongeza mzunguko wa fedha??????
Ili kuongeza mzunguko wa fedha mambo mawili muhimu yabidi kufanyika....... kuongeza government spending, na kupunguza riba ili watu wakope na wewekeze kwenye miradi mikubwa ya kiuchumi
 
Kwasababu ya ukame unaoendelea. Jambo la msingi kwasasa ni serikali ipige marufuku kusafirisha mazao nje ya nchi
 
Ushauri mzuri na uwasilishaji mzuri saana.
 
Mkuu hii timu ya wabobezi wa uchumi watamsaidia mama kuimalisha uchumi wetu.
1. JAKAYA MLISHO KIKWETE
2. LIZIWANI KIKWETE
3. JANUARY MAKAMBA AKA KIGOGO
4. ZITO ZUBERI KABWE
5. NAPE NAWIE
6. MZEE WA VISENTI
 
Popote ulipo, wewe una IQ kubwa Sana. Ningekua mimi ndo Raisi, kwa bandiko hili, ningekuteua kwa nafasi hiyo ya NSA.
Watu wa aina yako ni wachache Sana Serikalin, na hata wakiwepo, mifumo ya Nepotism, Corruption,low iq sindicate na Tabia ya watumishi kufanya jambo Ili kuonekana wanafanya kumbe hawamaanishi.
Tabia hizo Zina wademoralize.

Kwa maana hiyo, ni bora samia akiisha kukuteua, basi akufanye pia personal advisor kwenye mambo ya husuyo Uchumi kwa usalama wa nchi.

Mungu akujalie heri nyingi.
 
Mkuu hii timu ya wabobezi wa uchumi watamsaidia mama kuimalisha uchumi wetu.
1. JAKAYA MLISHO KIKWETE
2. LIZIWANI KIKWETE
3. JANUARY MAKAMBA AKA KIGOGO
4. ZITO ZUBERI KABWE
5. NAPE NAWIE
6. MZEE WA VISENTI
Duh, we jamaa, naomba niishie hapo.
 
Mchina ametupa soko la soya kwa mujibu wa uwezo tulio nao .hakuna limiti ya soko.
Achana na Computer hamia shambani ukalime ilikukuza uchumiwako.
KaribuNjaombe.
 

Usisahau na SGR......naamini hakuna tukachopata zaidi ya kulipa mkopo kwa riba ya juu
 
Ushauri mzuri lakini tayari anayo timu ya ushauri wa uchumi
 
Tunahija 'National Business Intelligence unit and infirmation center 'Kikosi kazi kitakacho fuatilia kwa undani kwanini biashara zinakufa na ninikifanyike pia ukitaka kupata fursa ama taarifa za kibiashara iwe rahisi kuzipata kupitia kwao (The entrepreneur and his/her environments)
 
Wazo zuri ila usisahau adui yetu namba moja huwaga ni serikali yenyewe!!Watu mnatumikia mifumo inayotugandamiza then mnaita hiyo hiyo serikali itusaidie..
1. Serikali ndo hutunga sheria mbovu na kandamizi.
2. Serikali hiyo hiyo ndo hufunga watu na wengine kuwaua kwa sababu watu hao wanapingana nayo.
3. Je mnajua serikali za dunia watu Innocent wapo wangapi magerezani?
4. Je unajua serikali imeua watu wangapi! Wale ambao inawaita ni "criminals" na wale ambao ni Innocent?
4. Serikali ndo imeleta mbolea na kujenga viwanda vya mbolea ili kuharibu ardhi na sasa ardhi zinakataa kutoa mazao bila mbolea, na mbolea imepanda sana bei hivyo kusababisha wakulima wadogo ambao ndo wazalishaji wakubwa wa chakula kushindwa kununua na itasababisha kupungua kwa uzalishaji na kupandisha bei ya mazao/chakula.

5. Serikali ndo huongeza kodi (hidden tax) kwenye bidhaa muhimu kama za ujenzi na vyakula muhimu ili kufidia mikopo ambayo hukopa kila mwezi kuendesha serikali japo wananchi hawajulishwi...then wanakuja kulalamika viongozi kuwa kwa nini bidhaa zimepandishwa bei..nyoko zenu

Moyo wangu unazidi kuzichukia serikali kwa sababu zinaendeshwa kwa uongo! Manipulation
 
NRFA anahifadhi nafaka na hasa mahindi na hana uwezo wa maghala kuhifadhi mahindi say kama nchi ina njaa, NRFA ana uhakika wa kutoa mahindi kwa watanzania mil 60.

Food security ni usalama na uhakika wa chakula. Kuna nyakati mafuta ya kula (hasa mfungo wa ramadhani ukikaribia) yakipotea week 2 tu, panakuwa hapatoshi.

Kama kuna eneo kama nchi hatujafanya homework ya kutosha ni food security iwe treated kama national security agenda ambayo sio tu ita-drain mfuko mkuu ila itatunisha mfuko mkuu, ku-cut down imports, kuongeza exports, kupanua tax base, kuongeza mzunguko.

Kuna eneo public sector (mamlaka) haijataka ku-stretch ili kutumia financial instruments kukuza biashara. Bila kufanya biashara na kutengeneza mzunguko uchumi hauwezi kutanuka.
Uchumi bila uzalishaji na kudhibiti ongezeko la thamani kwenye mazao ya kilimo unakuwa ni hadithi, analytics then hamna cha ziada.

Mtoa hoja ana ushauri mzuri sana, bila shaka wenye mamlaka watamtafuta kukaa nae na ku-extract nini kaona, nini anawaza ili nini tufanye.
Kama mtoa hoja angetoa neno lisilo na staha kwa "wakubwa" bila shaka angetafutwa kwa juhudi na nguvu kubwa sana ili ajieleze na ikiwezekana afike mbele ya pilato.
Ila mambo ya kujenga, hawa wasaidizi wa wakubwa huwa wanaona as if sio jambo lao.

Kama mvua zitachelewe kunyesha, au zikawa hafifu, sipati picha "kilio na malalamiko" yatakayofuata. Ila kwanini tusijifunze kwa falasafa ya Farao na Yusuf kuwa na national food reserve system wakati wa neema ili siku hali ikigeuka, Tanzania haitetereki kwenye usalama wa chakula. Chakula sio nafaka pekee (ambayo ndio major task ya NRFA)
Kuna lots should be done ili Watanzania wawe na uwezo wa kuzalisha na kula aina zote za vyakula.
 
Sina uhakika kama nchi yetu ina mtu anayeitwa "National Security Advisor". Kama yupo, kuna haja ya kumfukuza kazi. Ila kama hayupo, teua haraka. Yeye ata-design mpango wa muda mfupi kwa ajili ya 2022 to 2024 akilenga kutatua hizi changamoto zilizofungamana na masuala ya usalama wa nchi
 
Ww dada nyuzi zako hua ni very insightful .nakubaliana na ww kabisa.tuombe wahusika wasikie huu ushauri
 
1. Uwepo mjadala wa kitaifa (kwa watu wenye uelewa mkubwa wa mambo) wa jinsi gani ya kutoka hapa tulipo.
2. Kukusanya majiniasi walioko nchini na kuweweka mafichoni na kuwaandalia watakacho kitaka ili wasugue vichwa tupate teknojia yetu wenyewe indigenous technology kwa ajili ya maslahi ya nchi.
3. Tushirikiane zaidi na nchi za Asia na urusi.
 
Serikali ya ccm haina uwezo wa kukabiliana na majanga yanayowakabili watanzania kwa ufasaha.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Kwahiy ulitaka nitoe maoni gani lAbda ili uinjoy broo kiswahili kina utajiri wa misemo kama sijaelewa ni hivi ushauri wake ni mzuri ila huyo anayemshaur ni vigumu kuufanyia
Kwahiyo ukaona utuwekee na li ppicha hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…