Uchunguzi: TB Joshua aliwanyanyasa na kuwabaka wafuasi wake
3. Alitumia wazungu kuvuta akili za Waafrika wajinga wengi. Kwenye documentary wameongelea hili kwamba Muafrika mjinga mara nyingi hata kama hakuamini, akiona Mzungu kakuamini inakuwa rahisi sana kumkamata, anaona huyu mtu kama hata wazungu wanamkubali basi lazima atakuwa anasema kweli.
Huu mtego ni mkali sana kwa Mwafrika
 
Nilikuwa napitia,Michango ya wadau hapa,naona Wengi hawajazipitia hzo episode/documentary ya BBC...TB JOSHUA
 
Dini ni man made,skushangazwa sana na hayo.JE,Ni kiasi gani cha wendawazimu na upumbavu bwana TB JOSHUA ALIKUWA NAO.TB JOSHUA ALIKUWA MUHUNI/FALA/MWENDAWAZIMU WA KIWANGO CHA JUU MNO.
 
Former Disiciple-Bisola johnson anasema TB JOSHUA alikuwa SADIST & "PYSCOPATH". na mwengine paul agomoh anasema TB JOSHUA alikuwa "OPPOTUNIST".
 
THE TB JOSHUA I KNOW by bisola jonhson...kitabu toka 2018 cha former disciple mwanamama bisola kipo hewani,uhuni,ujanja na wendawazimu wa bwana tb joshua umewekwa wazi..
 
Abdul-fatai tb joshua,lazima afunuliwe vyema na wendawazimu wake.
 
Mambo matatu yalionisikitisha kutoka kwa bwana joshua.
1. Ubakaji aliokua akiufanya kwa wafuasi wake waliokua wanaishi ndani ya hilo boma lake,

2. Kuacha jengo lianguke watu zaidi ya 100 kufariki na alikua anafahamu kabisa jengo lilikua na hitilafu na lingeanguka mda wowote.

3. Mateso kwa binti wa damu.
 
Unapotosha, wengi humo walijitoa 2014-2018 sasa mali zipi walizotaka? Walishaandikaga vitabu huko nyuma kueleza haya sasa unapodai wamesubiri amekufa ni ajabu kidogo unless wewe ndio umewasikia baada ya BBC kuwahoji majuzi.

Kuhusu kushtaki wameeleza humo fear waliokua nayo, na hata ungeshtaki hakuna angeamini zaidi ungepotezwa tu. Kama mwamposa tu watu walikufa hakuna alichofanywa ndio sembuse ukamshtaki si ungegeuziwa kibao wewe!!

Ni ajabu sana hutaki kuwaamini watu waliokua direct subordinates kwake ila unataka tukuamini wewe unayecomment ukiwa Tandale kwa Tumbo!! You can't be serious.
Unapotosha, wengi humo walijitoa 2014-2018 sasa mali zipi walizotaka? Walishaandikaga vitabu huko nyuma kueleza haya sasa unapodai wamesubiri amekufa ni ajabu kidogo unless wewe ndio umewasikia baada ya BBC kuwahoji majuzi.

Kuhusu kushtaki wameeleza humo fear waliokua nayo, na hata ungeshtaki hakuna angeamini zaidi ungepotezwa tu. Kama mwamposa tu watu walikufa hakuna alichofanywa ndio sembuse ukamshtaki si ungegeuziwa kibao wewe!!

Ni ajabu sana hutaki kuwaamini watu waliokua direct subordinates kwake ila unataka tukuamini wewe unayecomment ukiwa Tandale kwa Tumbo!! You can't be serious.
Asante kwa maelezo safi.

Waafuasi na Waumini Wengi(Apologist) wa TB Joshua,Hoja mojawapo ni hii ya Kwanini Wamesubiri Nabii TB Joshua Afe ndio Wanatoa tuhuma zao na Angali hai hawakujitokeza..??

Mosi,Wengi Hawajatazama Documentary Ya BBC.

Na kuhusu tuhuma,Malalamiko au Mashitaka Juu ya TB Joshua,Yalikuwepo muda Toka 90's huko,

Kuna Habari/stori Ya Mzee/Mr.Abiola- Lagos, ya 2019,Ambayo inasema TB Joshua Kunamuda alikaa kwa Mzee huyu na akapewa chumba Cha kukaa na huduma za hapa na pale,huku TB Joshua akiitwa Abdul-Fatai.
Kwa ufupi stori inasimulia njisi TB Joshua alivyoshindwa kumsaidia Mzee katika Hali ngumu ya kiuchumi na kiafya iliyomkuta Mr Abiola maana Mzee alikuwa mfanyabiashara wa Magari/Usafiri.
Lakini kilichotokea Mzee baada ya kufa Bwana Abdul-Fatai (TB Joshua) aliwachukua mabinti zake wawili kama kutaka kuwasaidia, kilichotokea alifanya uharibifu kwa Mabinti hao(Kuwanyanyasa kingono na kisaikolojia),Mke wa Abiola na kijana wake walifanya jitahada ya kupambana na Nabii TB Joshua lakini kama ujuavyo Nchi za dunia ya Tatum,Taasisi nyingi na vyombo vya usalama vimetawaliwa na Rushwa,ufisadi na Ukiritimba.. TB Joshua corrupt system ya Nigeria alikuwa kaikamata mkononi.

Stori nyingine au tuhuma za bwana huyu TB Joshua ni Ya Pastor Peter kayode ya Mwaka 2009,Huyu Peter alikuwa Disciple wa TB Joshua, Habari yske inahusu TB Joshua alivyochukua Mke wake,na hii nibaada ya huyu bwana na Mke kwenda kwa TB Joshua kupata baraka ya kupata mtoto,walikuwa hawana, TB Joshua baadaye akijinyakuliwa Mke wa jamaa.Kiufupi jamaa alipata changamoto Santa na matatizo kwa ndugu zake na jamaa zake,Kisha akaamua kujiondoa SCOAN,

Pia,Kuna Mwanamama Bisola Johnson,Ex-Disciple...Ametoa kitabu chake kiitwacho the TB Joshua I know, Mwaka 2018.ameelezea Mambo mengi kuhusu TB Joshua Nabii.

Hivyo tuhuma,malalamiko Yalikuwepo muda Sana na wahanga wachache wenye ujasili walikuwa wanaongea na kwenda kwa koti.

TB Joshua alikuwa unaushawishi Mkubwa Africa (Siasa), Episode ya Tatu BBC, Rais Jk kikwete anaonekana yupo na TB Joshua,bila kusahau Marais waliokuwa wapiga debe wa TB Joshua akina Joyce Banda-Malawi.

Jambo la Muhimu na kufahamu Nchi maskini Sana,Mtu mwenye Pesa,Power,... taasisi na mifumo mingi inakuwa haina kazi inabaki kama midoli machoni pake.

Mwisho TB Joshua alikuwa Opportunist/Msaka fursa..!Aliyetafuta Money, Power na Fame,Na hakika alivipata.


Paul Agomoh anasema TB Joshua alikuwa "Evil Genius".
 
Tuhuma zinazomkabili TB JOSHUA zinaweza kuwa za kweli japo hakuna ushahidi wawazi.

Ila ushahidi wa kwamba alikuwa nabii wa uongo upo wazi. TB Joshua amedanganya watu wengi Sana na ndiyo muasisi mkubwa wa haya mafundisho ya mafuta ya upako, maji ya upako, nk.

Yeye ndiyo aliezalisha watu kama Shepherd Bushiri, Mwamposa, Ulbert Angel na wengi wao.

Hawa manabii wa mafuta, maji ya upako wanaambatana Sana na uzinzi kwenye shughuli zao. Hawa manabii ni wazinifu Sana kuliko unavyofikili. Angalia tuhuma zinazomkabili TB Joshua ni zilezile zinazomkabili Shepherd Bushiri South Africa.

Biblia inasema wazi kwamba siku za mwisho kutakuwa na manabii wengi wa uongo na kudanganya wengi (mathayo 24:11) .

Ni jambo la kusikitisha Sana raisi Tunubu wa Nigerian akimtetea TB JOSHUA.

Hawa watu ni wauaji wa kutisha lakini serikali za Africa zipo kimya.
Tunaona Mwamposa alivyoua watu Arusha kwa njia ya kizembe Sana lakini serikali Ilinyamaza kimya.

Tunaona TB JOSHUA alivyoua watu Nigerian baada ya jengo kudondoka lakini serikali IPO kimya.

Tumeona Shepherd Bushiri alivyofanya utapeli mkubwa South Africa lakini serikali zipo kimya.

USHAURI: Ngugu kama wewe ni muumini wa Hawa manabii, umepigwa. Ni matapeli, wauaji, waongo. Miujiza ya YESU inapatikana baada ya kutubu dhambi zako.

Miujiza ya YESU inapatikana kwa kuacha dhambi na kumuamini. Nje ya hapo ni uongo. Umedanganywa. Toka huko.

Kumuamini TB JOSHUA, Mwamposa ni uzezeta mkubwa sana.

Tunapata miujiza kwa kutumia jina la YESU tu.
 
• Hakuna jehanam, Hakuna mbingu Nyingine, Ukifa ni chakula cha Wadudu.

• Mjinga akijileta we mgonge tu. 😎
 
Ushahidi wako?
• Ushahidi wangu wa 1, kwa sababu sijawahi kuona mtu ameenda mbinguni.

• Ushahidi wangu wa 2, kuna baadhi ya maiti yamefukuliwa, lakini tumeishia kuona mifupa tu, nyama yote imeliwa na microorganisms.
 
• Ushahidi wangu wa 1, kwa sababu sijawahi kuona mtu ameenda mbinguni.
Hii sio hoja sababu kuna sehemu nyingi hujawahi ona mtu akienda zikiwemo sayari kwenye galaxy nyingine.
• Ushahidi wangu wa 2, kuna baadhi ya maiti yamefukuliwa, lakini tumeishia kuona mifupa tu, nyama yote imeliwa na microorganisms.
Unapokuwa umelala ukaota upo chooni, mwili wako unakuwa wapi?
 
Back
Top Bottom