Uchunguzi: TB Joshua aliwanyanyasa na kuwabaka wafuasi wake
Ushahidi wa unyanyasaji ulionea na mateso kutoka kwa mwanzilishi wa mojawapo ya makanisa makubwa ya kiinjili ya Kikristo duniani umefichuliwa na BBC.

Makumi ya waumini wa zamani wa Kanisa la Synagogue Church of all Nations - watano Waingereza - wanadai ukatili, ikiwa ni pamoja na ubakaji na utoaji mimba kwa lazima, uliofanywa na marehemu TB Joshua wa Nigeria.

Madai ya unyanyasaji katika eneo la siri la Lagos yamedumu kwa takriban miaka 20.

Kanisa la Synagogue Church of All Nations halikujibu madai hayo lakini lilisema madai ya hapo awali hayana msingi.

TB Joshua, aliyefariki mwaka wa 2021, alikuwa mhubiri na mwinjilisti mwenye mvuto mkubwa na mwenye mafanikio makubwa ambaye alikuwa na wafuasi wengi duniani.

Matokeo ya BBC katika uchunguzi wa miaka miwili ni pamoja na:
  • Masimulizi mengi ya watu waliojionea matukio ya ukatili wa kimwili au mateso yaliyofanywa na Joshua, ikiwa ni pamoja na matukio ya unyanyasaji wa watoto na watu kuchapwa viboko na kufungwa minyororo.
  • Wanawake wengi wanaosema walinajisiwa na Joshua, huku baadhi wakidai kuwa walibakwa mara kwa mara kwa miaka mingi ndani ya boma hilo.
  • Tuhuma nyingi za kutoa mimba kwa lazima ndani ya kanisa kufuatia tuhuma za ubakaji na Joshua, akiwemo mwanamke mmoja ambaye anasema alitolewa mimba mara tano.
  • Simulizi nyingi za moja kwa moja zinazoelezea jinsi Joshua alivyodanganya kuhusu "uponyaji wake wa miujiza", ambao ulitangazwa kwa mamilioni ya watu ulimwenguni kote.
Mmoja wa waathiriwa, mwanamke wa Uingereza, anayeitwa Rae, alikuwa na umri wa miaka 21 alipoacha shahada yake katika Chuo Kikuu cha Brighton mnamo 2002 na kuandikishwa katika kanisa. Alitumia miaka 12 iliyofuata kama mmoja wa wale wanaoitwa "wanafunzi" wa Yoshua ndani ya boma lake la kifahari huko Lagos.

"Sote tulidhani tuko mbinguni, lakini tulikuwa katika hali inayofanana na ya kuzimu, na huko kunatokea mambo mabaya," aliiambia BBC.

Rae anasema alinajisiwa na Joshua na kuwekewa aina ya kifungo cha upweke kwa miaka miwili. Dhuluma hiyo ilikuwa kali sana, anasema alijaribu kujiua mara nyingi ndani ya boma hilo.

Kanisa la Synagogue Church of All Nations [Scoan] lina wafuasi wa kimataifa, wanaoendesha chaneli ya TV ya Kikristo iitwayo Emmanuel TV na mitandao ya kijamii yenye mamilioni ya watazamaji. Katika miaka yote ya 1990 na mwanzoni mwa miaka ya 2000, makumi ya maelfu ya mahujaji kutoka Ulaya, Amerika, Kusini Mashariki mwa Asia na Afrika walisafiri hadi kanisani humo nchini Nigeria kumshuhudia Joshua akifanya "miujiza ya uponyaji".

Takriban wageni 150 waliishi naye kama wanafunzi ndani ya boma lake huko Lagos, wakati mwingine kwa miongo kadhaa.

Rae in a BBC studio interview, wearing glasses and black top

Maelezo ya picha: Rae alisalia kwa miaka 12 katika boma la Joshua

Zaidi ya "wanafunzi" 25 wa zamani walizungumza na BBC - kutoka Uingereza, Nigeria, Marekani, Afrika Kusini, Ghana, Namibia na Ujerumani - wakitoa ushuhuda wenye nguvu wa kuthibitisha waliopitia ndani ya kanisa, pamoja na matukio ya hivi majuzi zaidi katika mwaka wa 2019. Waathiriwa wengi walikuwa katika ujana wao walipojiunga mara ya kwanza. Katika baadhi ya kesi za Uingereza, usafiri wao hadi Lagos ulilipwa na Joshua, kwa ushirikiano na makanisa mengine ya Uingereza.

Rae na waliohojiwa wengine wengi walilinganisha masaibu yao na kuwa katika dhehebu la itikadi kali .
Jessica Kaimu, kutoka Namibia, anasema masaibu yake yalidumu kwa zaidi ya miaka mitano. Anasema alikuwa na umri wa miaka 17 wakati Joshua alipombaka kwa mara ya kwanza, na kwamba matukio ya baadaye ya kubakwa na TB Joshua yalisababisha atoe mimba mara tano akiwa huko.

"Haya yalifanyika kisiri... matibabu tuliyokuwa tukifanyiwa... yangeweza kutuua," aliiambia BBC.
Wengine waliohojiwa wanasema walivuliwa nguo na kupigwa kwa nyaya za umeme na mijeledi ya farasi, na mara kwa mara walikoseshwa usingizi.
Katika kifo chake mnamo Juni 2021, TB Joshua alisifiwa kama mmoja wa wachungaji wenye ushawishi mkubwa katika historia ya Afrika.

Akiinuka kutoka kwa umaskini, alijenga himaya ya kiinjilisti ambayo ilijivunia makumi ya viongozi wa kisiasa, watu mashuhuri na wanasoka wa kimataifa kati ya washirika wake.

Hata hivyo, alizua utata wakati wa uhai wake wakati nyumba ya wageni ya mahujaji wa kanisa ilipoporomoka mwaka wa 2014, na kuua watu wasiopungua 116.Uchunguzi wa BBC, ambao ulifanywa na jukwaa la kimataifa la vyombo vya habari vya Open Democracy, ni mara ya kwanza watu wengi wa zamani wa makanisa kujitokeza kuzungumza juu ya rekodi hiyo. Wanasema wametumia miaka mingi kujaribu kupaza sauti lakini wamenyamazishwa kwa ufanisi.

Baadhi ya mashahidi wetu nchini Nigeria wanadai walishambuliwa kimwili, na katika kisa kimoja walipigwa risasi, baada ya awali kujitokeza kupinga unyanyasaji huo na kuchapisha video zenye madai kwenye YouTube.

Wafanyakazi wa BBC ambao walijaribu kurekodi picha za boma la kanisa hilo Lagos kutoka mtaa wa umma mnamo Machi 2022 pia walipigwa risasi na usalama wa kanisa hilo, na walizuiliwa kwa saa kadhaa.

BBC iliwasiliana na Scoan na madai hayo katika uchunguzi wetu. Haikuwajibu, lakini ilikanusha madai ya awali dhidi ya TB Joshua.
"Kutoa tuhuma zisizo na msingi dhidi ya Nabii TB Joshua si jambo geni... Hakuna madai yoyote yaliyowahi kuthibitishwa," iliandika.

Raia wanne wa Uingereza waliozungumza na BBC wanasema waliripoti unyanyasaji huo kwa mamlaka ya Uingereza baada ya kutoroka kanisani. Wanasema hakuna hatua zaidi zilizochukuliwa.

Anneka pictured in BBC studio interview, wearing white jumper

Maelezo ya picha: Anneka anasema anaamini kuna waathiriwa wengi ambao bado hawajazungumza

Zaidi ya hayo, mwanamume Muingereza na mkewe walituma barua pepe kwa mashahidi waliojionea ushahidi wao wa mateso na video - ikiwa ni pamoja na rekodi za kushikiliwa kwa mtutu wa bunduki na wanaume wanaojiita polisi ambao pia ni wanachama wa Scoan - kwa Ubalozi wa Uingereza nchini Nigeria mnamo Machi 2010 baada ya kukimbia kanisa hilo. Katika barua pepe yake, mwanamume huyo alisema mke wake alishambuliwa kingono mara kwa mara na Joshua. Aliionya ubalozi huo kuwa raia wengine wa Uingereza bado wako ndani ya boma hilo wakikabiliwa na ukatili.

Pia anasema hakuna hatua zilizochukuliwa. Ofisi ya Mambo ya Nje ya Uingereza haikujibu madai haya, lakini iliambia BBC kwamba inachukulia ripoti zote za uhalifu, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya raia wa Uingereza nje ya nchi, kwa uzito mkubwa.

Scoan inaendelea kustawi leo, chini ya uongozi wa mjane wa Joshua, Evelyn. Mnamo Julai 2023, aliongoza ziara ya kwenda Uhispania.

Anneka, ambaye aliondoka Derby nchini Uingereza na kujiunga na Scoan akiwa na umri wa miaka 17, aliambia BBC kuwa anaamini kuna waathiriwa wengine wengi ambao bado hawajazungumza. Anatumai hatua zaidi zitachukuliwa kufichua vitendo vya Joshua.

"Ninaamini Kanisa la Synagogue Church of All Nations linahitaji uchunguzi wa kina ili kujua ni kwa nini mtu huyu aliweza kufanya kazi kwa muda mrefu kama alivyofanya," alisema.

Ripoti ya ziada ya Maggie Andresen, Yemisi Adegoke na Ines Ward
Kwa usaidizi na taarifa kuhusu unyanyasaji wa kingono, tafadhali wasiliana na Mtandao huu wa BBC Actionline nchini Uingereza. Na kwa habari zaidi juu ya madhehebu, tafadhali tazama The Family Survival Trust

BBC
Pia soma: BBC imepanga kutoa video inayoonesha Unabii Feki wa TB Joshua
Mimi nilitazama video ya ushuhuda ya Binti was kinaijeria mwaka 2012,wakilazimishwa kushija nyeti za huyo jamaa!

Tangy hapo hadi leo sikumuamini tena!hadi leo ni ngumu kuwaamini Hawa watu has wa miujiza!
 
Haya makanisa yanasiri kubwa sana. Nimesikia Leo asubuhi BBC nimrbaki kinywa wazi. Najivunia kusali kanisa moja takatifu katoliki na la mitume. Haya makanisa mengine ni utapeli na ujanja wa namna ya kuishi tu. Hata Hawa akina mwamposa, gwajima, gamanywa nk siku wakifa tutasikia mengi.
Hujawahi kusikia ulawiti wa watoto ndani ya Kanisa Katoliki??
 
Naona na tv yake imetolewa rasmi Dstv

Pia mkipata muda muwe mnamsikiliza mzee wa upako. Anafungua code nyingi sana kuhusiana na haya makanisa ya uyoga
Kanisa la mzee wa upako lenyewe ni la uyoga.
 
Sijaona huo ushahidi
Maelezo yanaaonesha km ni taarifa za kupanga.
Kuna kitu hapo katikati kimejificha.
NB: mimi sio muumini wa manabii na mitume
 
Sijaona huo ushahidi
Maelezo yanaaonesha km ni taarifa za kupanga.
Kuna kitu hapo katikati kimejificha.
NB: mimi sio muumini wa manabii na mitume
Ushahidi gani kwa mfano??
 
Ushahidi gani kwa mfano??
Nieleweshe wewe km umeelewa.
Yaani raia wa Uingereza wabakwe na kunajisiwa pamoja na kufungiwa tangu mwaka 2010. Serikali ya Uingereza ipate taarifa toka kwa aliyefanikiwa kutoroka na ikae kimya?
Hapa kidogo pagumu.
Labda km ingekuwa nchi zetu hizi zisizojali raia wake hilo lingewezekana.
 
Lakini ndo walioinua madudu ya markenzi pia wa Kenya na baadae ikaonekana ni kweli baada ya nyie kupinga
BBC hawawezi kukurupuka
Mpaka wanatoa hiyo taarifa, wamefanya uchunguzi na wamejiridhisha. Naunga mkono hoja. FUNZO. Kuwa makini na kujihadhari na manabii wa uongo. Hili alionya na kutahadharisha Bwana Yesu, mtume Paulo, Petro, nk. "Be carefull with false prophet"
 
Nimepitia comments za watu wengi hapa nimegundua kitu.

Watu bado wameshikwa na uwongo wa Joshua. Ni atari sana kwani hata baada ya kuona video watu wakisema yaliyowapata mtuu bado hutaki kuamini. Kwamba hawezi kuyafanya hayo? Kwani yeye ni mungu.

Mtu anajiita nabii [emoji1]. Afu bado tu unashindwa kujua kwamba ni mwongo.

Tubadilike
 
Waingereza ni watu madhalimu sana tu.

Udhalimu wao umetapakaa karibia mabara yote.

Naafiki na wengi wanao ona udhalimu huu.
Kinachotafutwa hapa ni kukosekana kwa imani dhidi ya kanisa katika jamii na hakuna lolote la maana.
Jimmygatete, umemaliza yote na hayo maneno Juu. Huo ndio huo udhalimu wenyewe.
 
Mm sijawahi kuwakubali Hawa wanaojiita wachungaji ila hicho walichotoa BBC hakiendani kabisa na hadhi yao, BBC sijui nini kimewakuta hawana tofauti na vyombo vya habari vya udaku.
wanataka kubalance mzani wa kashfa ya ushoga kwa kanisa la Roman.
 
Nakala ya uchanguzi BBC ya (BBC Eye) inamtaja TB JOSHUA kama mhalifu Kwa kipindi Cha miaka 20 hadi mauti yanamkuta alikuwa amesha baka ,kushikiria,kuuwa,kutesa,kubaka na miujiza ya uongo
.

Wengi wa waathirika ni raia wa kigeni na wachacha kutoka Nigeria,uozo huu umeanikwa na waaandishi wa uchanguzi.

Chanzo BBC

USSR

Sent from my Infinix X6511G using JamiiForums mobile app
 
Nimepitia comments za watu wengi hapa nimegundua kitu.

Watu bado wameshikwa na uwongo wa Joshua. Ni atari sana kwani hata baada ya kuona video watu wakisema yaliyowapata mtuu bado hutaki kuamini. Kwamba hawezi kuyafanya hayo? Kwani yeye ni mungu.

Mtu anajiita nabii [emoji1]. Afu bado tu unashindwa kujua kwamba ni mwongo.

Tubadilike
Sawa kabisa
 
Nieleweshe wewe km umeelewa.
Yaani raia wa Uingereza wabakwe na kunajisiwa pamoja na kufungiwa tangu mwaka 2010. Serikali ya Uingereza ipate taarifa toka kwa aliyefanikiwa kutoroka na ikae kimya?
Hapa kidogo pagumu.
Labda km ingekuwa nchi zetu hizi zisizojali raia wake hilo lingewezekana.
Unaelewa chochote kuhusu "human trafficking" ambalao ni tatizo kubwa sana karne ya 21?

Umewahi kusikia Mwarabu yeyote huko Uarabuni amakamatwa kwa kuwatesa na kuwafungia wafanyakazi wa ndani wa mataifa mengine ? Unafikiri hao wafanyakazi nchi zao hawana balozi katika hizo nchi za Uarabuni??
 
Back
Top Bottom