Uchunguzi; Watanzania wengi hujisaidia haja ndogo kwenye makopo usiku

Uchunguzi; Watanzania wengi hujisaidia haja ndogo kwenye makopo usiku

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
kwema Wakuu!

Tuachane na mambo ya Ukraine na Urusi.
Leo sitaki kupotezea muda watu.

Moja ya mambo yaliyonishangaza tangu nilipotoka nyumbani miaka 10 iliyopita ni kuona wakazi wengi kuwa na tabia ya kukojolea kwenye makopo au ndoo nyakati za usiku.

Hivi inakuwaje mtu alale na Mikojo wakati haumwi?
Ni uvivu wa kutoka nje usiku au ni Woga?

Kinachoshangaza zaidi ni kuona tabia hii ipo mpaka Kwa wanaume. Hivi mwanaume mzima unakojolea kwenye kopo au ndoo kweli badala ya kutoka nje na kujisaidia chooni.

Unakuta mtu kaoa kabisa alafu yeye na Mke wake wanakojolea kwenye ndoo au kopo. Kwa kweli hili sio uungwana Kabisa.

Halafu ndoo hiyo hiyo ati mtu anaogea au kufulia😀😀 hii kuna uchafu zaidi ya huu? Ukimuuliza atakwambia ati ndoo ameiosha, upuuzi mtupu.

Uchunguzi huu unawahusu zaidi Wale wenye nyumba za kupanga ambazo sio Self-container, isipokuwa Choo kipo Kwa nje kimejitenga.

Pia baadhi ya wenye nyumba ambao vyoo vyao vipo Kwa nje.

Ushauri wangu, unapoenda ugenini kusalimia uwe Makini sana, unaweza ukadhani unaoga kumbe unajipaka mikojo ya watu japokuwa watakuambia wanaisafisha hiyo ndoo.

Mikojo na mavi no uchafu, ni najisi, watu lazima muwe wasafi bhana sio muwe Kama majini.

Wito: wenye tabia hii nawasihi mubadilike, acheni kukojolea kwenye makopo au ndoo, alafu ndoo hizohizo mnaogea na kufulia nguo. Huo ni UCHAFU.

Jumapili njema.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Buza, Dar es salaam
 
Back
Top Bottom