Uchunguzi; Watanzania wengi hujisaidia haja ndogo kwenye makopo usiku

Uchunguzi; Watanzania wengi hujisaidia haja ndogo kwenye makopo usiku

Hii tabia ipo sana mikoani kutokana na watu kuhofia wanyama wakali usiku.
 
Sasa ndo nimepata majibu kwenye hii mada...zamani Kuna mahali nilikua naishi ,nilikua nasikia kila ikifika saa sita au Saba usiku lazima nisikie kelele za michirizi ya kitu Kama maji hivi yakimiminika kwenye ndoo au beseni Tena kwa Kasi Sana hapo chumba Cha jirani,kila siku najiuliza hiyo michirizi ya maji kila siku ninayoisikia chumba Cha jirani (mwanamke)ni vitu gani haswa...nimepata jibu Sasa,lakini choo kilikua kipo ndani ya fensi kabisa siyo nje...

Alafu ndoo hiyohiyo au beseni hilohilo lifulie nguo zako au ulitumie kuogea๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€

Kuna watu hawanielewi hapa
 
kwema Wakuu!

Tuachane na mambo ya Ukraine na Urusi.
Leo sitaki kupotezea muda watu.

Moja ya mambo yaliyonishangaza tangu nilipotoka nyumbani miaka 10 iliyopita ni kuona wakazi wengi kuwa na tabia ya kukojolea kwenye makopo au ndoo nyakati za usiku.

Hivi inakuwaje mtu alale na Mikojo wakati haumwi?
Ni uvivu wa kutoka nje usiku au ni Woga?

Kinachoshangaza zaidi ni kuona tabia hii ipo mpaka Kwa wanaume. Hivi mwanaume mzima unakojolea kwenye kopo au ndoo kweli badala ya kutoka nje na kujisaidia chooni.

Unakuta mtu kaoa kabisa alafu yeye na Mke wake wanakojolea kwenye ndoo au kopo. Kwa kweli hili sio uungwana Kabisa.

Halafu ndoo hiyo hiyo ati mtu anaogea au kufulia๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€ hii kuna uchafu zaidi ya huu? Ukimuuliza atakwambia ati ndoo ameiosha, upuuzi mtupu.

Uchunguzi huu unawahusu zaidi Wale wenye nyumba za kupanga ambazo sio Self-container, isipokuwa Choo kipo Kwa nje kimejitenga.

Pia baadhi ya wenye nyumba ambao vyoo vyao vipo Kwa nje.

Ushauri wangu, unapoenda ugenini kusalimia uwe Makini sana, unaweza ukadhani unaoga kumbe unajipaka mikojo ya watu japokuwa watakuambia wanaisafisha hiyo ndoo.

Mikojo na mavi no uchafu, ni najisi, watu lazima muwe wasafi bhana sio muwe Kama majini.

Wito: wenye tabia hii nawasihi mubadilike, acheni kukojolea kwenye makopo au ndoo, alafu ndoo hizohizo mnaogea na kufulia nguo. Huo ni UCHAFU.

Jumapili njema.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Buza, Dar es salaam
Tabia za Buza usizilete hapa.

Siku hizi nyumba zote Kimara ni self contained unategemea Nani atakojolea kopo?
 
Tabia za Buza usizilete hapa.
Siku hizi nyumba zote Kimara ni self contained unategemea Nani atakojolea kopo?


Ukiona Jambo ninaouzungumzia ujue ni Kwa watu wengi.

Sizungumzii ubinafsi au kuumiza kundi Fulani isipokuwa kuifanya jamii ibadilike.
 
Kuna mmoja kwenye nyumba ya udongo, alitoa udongo kidogo kwenye fito akaweka makaratasi. Usiku anayatoa anaweka mrija wake anakojoa.

Sikumoja akiwa anakojoa kuna aliyekua anaukinga ule mkojo kwenye kopo. Jamaa alistuka alitoka ndani mbio, kufika nje ile njemba ikawa inakimbia na kopo lake la mkojo.

Mwenye mkojo alimkimbiza sana mpaka alimkamata akamwaga mkojo wake anarudi nyumbani. Mwizi wa mkojo aliokota kopo akamwambia umebaki kidogo uatanitosha. Mwenye mkojo akaanza tena mbio.
hahahaha mkuu umetisha sana
 
Na kwanini uamke usiku kukojoa katika hali ya kawaida ukitoa watoto, wajawazito na wale wenye tezi dume au kisukari, wagonjwa wa Pressure wanaotumia diuretics, au waliokunywa pombe, binadamu wa kawaida akisha kojoa kabla ya kulala huwa ana uwezo wa kulala mpaka kunakucha bila kuhitaji kukojoa!

Km wewe unalala kuanzia saa 4 usiku unaweza kuhimili mkojo mpk kufikia saa 12 Asubuhi.
 
Kuna mmoja kwenye nyumba ya udongo, alitoa udongo kidogo kwenye fito akaweka makaratasi. Usiku anayatoa anaweka mrija wake anakojoa.

Sikumoja akiwa anakojoa kuna aliyekua anaukinga ule mkojo kwenye kopo. Jamaa alistuka alitoka ndani mbio, kufika nje ile njemba ikawa inakimbia na kopo lake la mkojo.

Mwenye mkojo alimkimbiza sana mpaka alimkamata akamwaga mkojo wake anarudi nyumbani. Mwizi wa mkojo aliokota kopo akamwambia umebaki kidogo uatanitosha. Mwenye mkojo akaanza tena mbio.
Kidogo nipaliwe na Konyagi.
Jamani๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Hii nchi uhuru umezidi.

Yani mtu akikojoa ndani usiku nayo ni kesi? Mbona self contained houses ni saw na kukojoa kwenye kopo?
Wabongo utawaweza hasa wa JF mambo Safi,. Maisha yenyewe haya ya kuviziana utoke nje vibaka wakulalue yote hiyo ya nini wakati visado vipo unajinafasi bila wasiwasi
 
Back
Top Bottom