Hello waungwana, mko salama? Poleni kwa shughuli za kila siku, na heri ya mwaka mpya.
Siku hizi mjini kuna biashara nyingi sana. Kuna wakati hadi unajiuliza, je, wanaume wameacha kutongoza au vipi? Maana wanawake wengi kwa sasa wanatafuta waume, na wako tayari hata kugharamia kuunganishwa na mwanaume.
Wanawake wengi, hasa waofisini, wanatamani kuolewa lakini hawatongozwi. Wapo tayari kutenga bajeti ili waunganishwe na mwanaume. Wengine wamefika hatua ya kufungua page zao kabisa Instagram, na hiyo ndiyo kazi yao kubwa wanafanya kukuunganisha upate mke/mume
Ninasema kwa uhakika kwa sababu nina ushahidi. Kuna jamaa aliwahi kunishirikisha kazi hii, na inalipa sana. Unaweza usiamini—unakuta dada yuko vizuri kabisa, ana kila kitu, ila changamoto ni moja tu: hatongozwi. Anakucheki, unamuunganishia mwanaume, ile namba ya simu unauziwa hata kwa laki tano, wanakutana na mambo yanaendelea.
Hapa ndipo panapochanganya: sijui hii ni fursa au ni tatizo kwenye suala la malezi na maadili. Mimi nafanya kazi maeneo ya Mikocheni, kuna jamaa amepanga apartment nzuri yenye hadhi ya juu, hana kazi nyingine—kazi yake ni hiyo tu. Na si kuunganisha watu wa kuoana pekee; anaunganisha hata wale malaya.
Yaani inafika siku mtu akiwa na upwiru, anampigia dalali na kumwambia amtafutie demu mwenye vigezo fulani—awe mwaminifu, aje hotel fulani. Dada analipa, na mwenye upwiru analipia pia; hapo ni 50/50.
Hii kazi ni risk sana. Ukimpeleka demu halafu akaenda kupiga tukio, lazima wewe uwajibike. Na demu akipata tatizo, wewe bado unawajibika. Kwa namna fulani unakuwa mdhamini wa wote wawili. Ni fursa inayolipa, lakini risk yake ni kubwa mno. Mimi mwenyewe nilijaribu kwa kama mwezi mmoja na nusu, nikagundua ni hatari sana. Kuna demu mmoja alikuwa anataka kuolewa, nikapewa mchongo nikamuunganisha na mtu, lakini kilichotokea baadaye ni cha ajabu sana—si rahisi hata kusimulia. Kuanzia hapo nikaamua kuachana nayo.
Mambo haya yanafanyika sana siku hizi.na Si wanawake au malaya tu hata wale magasho au wale wanaokula magasho nao unakuta mtu ana status nzuri mtaan hataki agundulike kam anakula magash anakupa mchongo umtafutie daah ni hatari.Ukipita maeneo kama Sinza, hali inashangaza. Sijui kama ni ugumu wa maisha, au ushirikina umezidi mjini