Mkuu labda mimi nitakuwa tofauti kidogo kuhusu udhaifu. Labda nianze kwa tafsiri ninayoielewa Mimi.
Udhaifu ni ile hali ya kiungo au akili kulemaa au kushindwa kujizuia. Hiki kitu hakitokei voluntary binafsi naamini udhaifu ni kufanya jambo involuntary. Mfano Kusahau sahau, Kiungo kimoja kuwa dhaifu, kushindwa kuona katika mazingira Fulani.
Kutokana na tafsiri hapo juu utaona kwamba hivi vitu vinamtokea mtu pasipo kupenda, Yaani mtu hushtuka ameshatenda jambo fulani. Kwangu Mimi huo ndio udhaifu
KUNA TABIA AMBAYO MTU AMESHAJIZOESHA ALAFU ANASINGIZIA UDHAIFU ( HUU NIUITE UPUMBAVU)
Mtaniwia radhi upumbavu sio tusi bali ni hali ya mtu kurudia matendo ambayo yanamatokeo mabaya.
Hizo tabia ulizozitaja sio udhaifu bali ni upumbavu wa mtu katika jambo fulani. Mfano
UVUTAJI SIGARA -: Hakuna mtu asiyejua kwamba sigara inaaddiction hivyo ukianza kuvuta tegemea kwamba hiyo ndio inaweza kuwa ndio tabia yako katika maisha yako yote hapa duniani. Sasa je! Mtu anawezaje kusema uvutaji wa sigara ni udhaifu wake?
Kwamba huyu mtu alizaliwa anavuta sigara? Kwamba hakusoma kuwa uvutaji wa sigara ni hatari na unaleta addiction?
Nafikiri wavutaji wa sigara ni WAPUMBAVU tuu, hakuna udhaifu wowote kwao, wakati wanajifunza kuvuta walijua kabisa sigara inaaddiction pia ni hatari kwa afya Yao. Hivyo wasilete UPUMBAVU wao.
Unywaji WA POMBE -: Hapa pia hakuna udhaifu wowote, mostly of people who are addicted to alcohol are stupid. Huwezi kumkuta mtu anayejitambua/anaejiheshimu na mwenye fedha akakwambia nina udhaifu wa kunywa pombe, ni wale watu WAPUMBAVU PUMBAVU tuu ndio atakwambia maneno ya kijinga kijinga.
WAPENDA NGONO ZEMBE -: Hawa nao ni walewale tuu UPUMBAVU umewajaa, wakiona mwanamke lazima wachukue namba kutongoza, Yaani ni kama biashara au kazi yake kutongoza wanawake ili afanye ngono, huu siuiti udhaifu maana tabia hujenga mazoea hayo mazoea ndio mnataka kusingizia kwamba ni udhaifu hapana huo ni UPUMBAVU.
WAPIGA NYETO -: Hii nayo ni tabia ya kipumbavu ambayo mtu anajizoesha mwisho anakuja kusingizia kwamba ni udhaifu.
MWISHO NIWAKUMBUSHE VIJANA NA WAZEE WENYE TABIA MBOVU MBOVU, kwanini udhaifu wenu usiwe katika mambo haya
KUFANYA KAZI KWA BIDII
KUSOMA VITABU
KUWAZA MAWAZO MEMA
KUSAIDIANA KUINUANA KATIKA BIASHARA