pasco,
Umetuomba tupitie ''A Report on Slavery and Slave Trade...''
Nimeipitia na hakuna kipya kwa kile ninachokijua kuhusu hawa
jamaa wewe unaowategemea.
Hebu soma na tafakari kwa makini kabisa umjue huyu Mmeshinari
Mackenzie mwandishi wa taarifa yako:
''In view of the fact that very little was known of the numbers and condition of the Slaves in the British Protectorate of Zanzibar, and especially of those in the almost entirely unexplored island of Pemba, The British and Foreign Anti-Slavery Society determined last year to send out a Special Commissioner to inquire into the state of Slavery and the Slave trade in that Protectorate. After mature consideration, it was resolved to request Mr. Donald Mackenzie—a gentleman whose long experience of Moham¬ medan customs and Slavery amongst the Arabs in North-West Africa, coupled with some knowledge of Arabic, well fitted him for an inquiry of this nature—to undertake the mission. To this request of the Committee Mr. Mackenzie cheerfully acceded, and proceeded to Zanzibar and Pemba at the beginning of the present year. The result of his inquiries will be found embodied in the annexed Report.''
July, 1895.
Huu utangulizi na lugha na jinsi utangulizi huo ulivyoandikwa
unauondolea sifa kabisa ya kuwa taarifa ya maana na inayoweza
kutegemewa.
Sitokwaambia makosa yaliyoko katika utangulizi huo.
Wewe unaandika kutoka kwenye hisia zako ambazo kwa bahati
mbaya sana hazitegemei ushahidi madhubuti.
Mimi nimefika kunakotoka hizo taarifa unazozitegemea.
Katika utafiti wangu nimefika hadi Blantyre, Glasgow Scotland.
Hiki ni kijiji alichozaliwa
David Livingstone na hiki kijiji kizima
kimegeuzwa kuwa makumbusho.
Chanzo cha hizo taarifa zake ma mapicha ya kuchora ya utumwa
yanatoka hapo.
Naamini unamjua
Livingstone kuwa alikuwa Mmeshionari na yeye
ndiye inasemwa alikuwa akipiga vita biashara ya utumwa.
Hizi lugha za ''Mohammedan'' chanzo chake ni hao akina
Livingstone.
Walikuwa roho zinawauma kuutaja Uislam.
Labda nikuulize
Pasco.
Kwa watu kama hawa utategemea kitu gani?
Kwa kumaliza napenda nikufahamisha kuwa nilifanya kipindi cha radio
BBC kuhusu historia hii nikitumia studio za BBC Scotland nikirushwa
Bush House, London.
Hii ilikuwa mwaka wa 1991.
Ukweli wa mengi kuhusu hizi fitna na propaganda tunaujua na haya yote
ni chuki tu dhidi ya Uislam.
Sikuona haja ya kujibu hayo yako mengine.