Udhalimu wa Utumwa Zanzibar na Pemba: Mababu zetu waliteswa, walihasiwa, walibakwa, na kuuawa kinyama

Udhalimu wa Utumwa Zanzibar na Pemba: Mababu zetu waliteswa, walihasiwa, walibakwa, na kuuawa kinyama

Hivi wata wana changanya mambo ama vipi!!? Kwa sababu, uarab siyo uislam, apo kuna race na religion, na mtu mweusi (mwafrika) siku zote anapo bugi ni kuchanganya vitu hvo kias ana kuwa blinded haoni kabisa, hakuna mtu wa nje ya Africa aliyekuja bara Africa bila kufanya jambo baya, na dini kilikuwa kigezo cha hao wageni (waarab, wazungu) kufunika maovu yao na kutengaisha umoja wa watu weus as a race. Eb tujitambue watu weus kwa kweli
 
Ivi kuna biashara isiyokua na soko .soko na biashara lipi linaanza mwanzo? Nani walikua ndio wanunuzi wa watumwa? Wanunuzi walikua wazungu wakristo na hata hela walikua wakiwapa waarabu ili wakalete watumwa wengi .ila wao walikua wanajificgavili baadae walaumiwe waarabu na dini yao.mazungu makiristo kule south afrika yaliwauwa na juwabagua watu weusi muda mrefu lakini hawasemwi eti kwa sababuvya dini yao .wajerumani waliuwa watu kibao tanganyika .lakini hawasemwi kwa sababu wakiri .acha udini wewe pasco ni mdini mkuu na udini utakuua
 
pasco,

Nilichojifunza kutoka ktk picha kuwa waznz Wa sasa ambao wengi ni weupe Si waasili koz hizo picha hakuna hata mmoja MWeupe aliye mtumwa so mapinduzi yalifanywa na weusi.
 
WE Pasco mimi nikifikiri ni mchambuzi kumbe ni mtu wa chuki na unaleta mambo ya picha za vikatuti na masanamu ya kanisani...
hata hivyi nakuarifu hakuna Mzanzibari aliefanywa Mtumwa. Wafalme wa Zanzibar hawakutesa raia zao hata siku moja .....
Ukweli utabaki Zanzibar ilikua ni kituo cha Biashara ya watumwa walokua wakiletwa na wazungu kutoka ndani Bara ...
Pale ndio ilikua ni soko na wanunuzi na wazungu.

hakuna Mpemba , Mmakunduchi, mdole, Mtumbatu Mkojani alo wahi kufanywa mtumwa...
walikuwepo wafanya kazi wa mashamba ya karafuu nao sio wazanzibari ni manamba kutoka mainland bara ....

hivyo mada iko sahihi kabisa ya Mohamed Said kuwa hakuna Sultan alowahi kutesa wala kuua subject wake hakuna ushahidi huo..ndio maana Masultani waliheshimiwa na wakitembea biloa ya vifaru wala askari ..walikua wakipita mashamba na mitta yote ya zanzibar bila ya wasi wasi.
Mapinduzi yaliuza watu kati ya 15,000 - 20,000
sasa wakati huo znz ilikua ni watu 125,000 sasa wewe fikiria mwenyewe...
Ww muongo eastafrica wazungu hawakufanya biashara ya utumwa
 
Nivigumu kuelewa ukweli halisi generation ya saivi ila tusubir tuu coz kilicho fanyika popte hakita potea yuko aliye yahifandi yote na yeye ndie ajuae, nimbora na muadilifu wa haki.
 
Acha uongo mwarabu hana dharau tusingekua tunaenda kufanya kazi kwao na pia dada zetu siku adi siku wanaenda wakifanya kazi za ndani
 
Mtanzania anathaminika nchi nyingi za nje, mfano ukiwa pale dubei umesimama kituoni na m-Nigeria mkiwa wote mnaitaji taxi basi wewe mtanzania utapanda na m-Nigeria anabaki.
 
Shukran Pasco kwa uzi wako.

Umeandika mengi lkn umeongozwa na allegation badala ya facts.

Kwanza tambua kuwa biashara ya utumwa ilikuwa na siko kubwa Ulaya na Amerika.

Baada ya wazungu hasa Christopher Columbus kuigundua Amerika kama new world,biashara ya utumwa ilishamiri Afrika hasa Afrika Magharibi.

Huwezi ukatenganisha biashara ya utumwa na Wazungu ambao waliwatumia waarabu kama middle men wao.

Kwa kiswahili cha sasa tunaweza kusema kuwa Wazungu walikuwa mataicoon na waarabu walikuwa pusher.

Kwa upande wa unyanyasaji na ubakaji inawezekana ikawa kweli walibaka.

Lakini hawakubaka kwakuwa wao ni waarabu,bali walibaka kama wabakaji waliopo Tanzania kwa sasa.

Mpaka leo bado kuna matukio mengi ya ubakaji ambayo yanaendelea Tanzania na yanafanywa na weusi wenzetu,ukitaka rejea kasome ripoti ya tume ya haki za binaadamu ya Mama Kejo Bisimba ya mwaka 2011 na kuendelea.

Kuhusu kuzaa na waswahili huenda waliwapenda waarabu,Mbona sasa hivi maeneo yenye ujenzi wa barabara ambapo wachina ndio wahusika watoto waliozaliwa na wachina ni wengi sana.

Yaani Dada zetu wanazaa wachina,Je wanabakwa na wachina au wanazaa kwa hiari?

Kuhusu mateso,hivi kuna maeneo walipo teseka zaidi ya Afrika ya kusini? hivi makaburu walikuwa waarabu?

Mbona mpaka sasa Wapalestina wanauawa kinyama(rejea kauli za Nyerere na Mandela) Wayahudi nao ni Waarabu? Kamuulize Dr Raitama Azavery atakuelezea vizuri kadhia ya mazayuni.

Juzi juzi zilitoka tuhuma kuwa Mashekhe wa Zanzibar aki na Farid Hadi na Aki Shekh Mselemu Ally kuwa wanaingiliwa kinyume na maumbile tena wakiwa ni wanaume wanaoheshimika,Je hao wafilaji ni wanaotuhumiwa kuwafila ni Waarabu?

Hivi umesahau waliomuua Mwangosi?

Ulimboka nae aliteswa na waarabu?

Hivi Mauaji ya Mwembe Chai ya 1998 nayo yalifanywa na Waarabu?

Hivi Waarabu ndio waliomuua Alfonce Mawazo?

Uhalifu ni uhalifu tu,hakuna ushenzi bora uwe umefanywa na Mwarabu au Mweusi.

Mauaji ya Kimbali ya Rwanda ,Afrika ya kati na Yanayoendelea Sudani kusini hayana mkono wa Mwarabu.
 
Eti Waarabu hawakuwatesa wazanzibar? kuna watu dini zinawapumbaza kweli, hivi ni nani aliyesoma history asiyejua unyama wa waarabu? watumwa walikuwa wanatolewa bara wanapakiwa kwenye majahazi wanaenda kutumikishwa.
watumwa wa kiume walikuwa wanahasiwa ili wasizaliane
wazungu na wenyewe walikuwa wanyama hivyo hivyo
leo mtu unayokwa na povu ukiwatetea kisa dini yako?
hata sasa hivi mbona kuna madhila mengi watu weusi wanapitia huko Qatar sababu ya weusi wao?
huko ulaya pia wazungu wanawabagua waafrica nyie mnatokwa mapovu kuwatetea?
yaani hakuna ajabu kubwa kama hii
 
pasco,

Umetuomba tupitie ''A Report on Slavery and Slave Trade...''
Nimeipitia na hakuna kipya kwa kile ninachokijua kuhusu hawa
jamaa wewe unaowategemea.

Hebu soma na tafakari kwa makini kabisa umjue huyu Mmeshinari
Mackenzie mwandishi wa taarifa yako:

''In view of the fact that very little was known of the numbers and condition of the Slaves in the British Protectorate of Zanzibar, and especially of those in the almost entirely unexplored island of Pemba, The British and Foreign Anti-Slavery Society determined last year to send out a Special Commissioner to inquire into the state of Slavery and the Slave trade in that Protectorate. After mature consideration, it was resolved to request Mr. Donald Mackenzie—a gentleman whose long experience of Moham¬ medan customs and Slavery amongst the Arabs in North-West Africa, coupled with some knowledge of Arabic, well fitted him for an inquiry of this nature—to undertake the mission. To this request of the Committee Mr. Mackenzie cheerfully acceded, and proceeded to Zanzibar and Pemba at the beginning of the present year. The result of his inquiries will be found embodied in the annexed Report.''
July, 1895.

Huu utangulizi na lugha na jinsi utangulizi huo ulivyoandikwa
unauondolea sifa kabisa ya kuwa taarifa ya maana na inayoweza
kutegemewa.

Sitokwaambia makosa yaliyoko katika utangulizi huo.

Wewe unaandika kutoka kwenye hisia zako ambazo kwa bahati
mbaya sana hazitegemei ushahidi madhubuti.

Mimi nimefika kunakotoka hizo taarifa unazozitegemea.
Katika utafiti wangu nimefika hadi Blantyre, Glasgow Scotland.

Hiki ni kijiji alichozaliwa David Livingstone na hiki kijiji kizima
kimegeuzwa kuwa makumbusho.

Chanzo cha hizo taarifa zake ma mapicha ya kuchora ya utumwa
yanatoka hapo.

Naamini unamjua Livingstone kuwa alikuwa Mmeshionari na yeye
ndiye inasemwa alikuwa akipiga vita biashara ya utumwa.

Hizi lugha za ''Mohammedan'' chanzo chake ni hao akina Livingstone.
Walikuwa roho zinawauma kuutaja Uislam.

Labda nikuulize Pasco.
Kwa watu kama hawa utategemea kitu gani?

Kwa kumaliza napenda nikufahamisha kuwa nilifanya kipindi cha radio
BBC kuhusu historia hii nikitumia studio za BBC Scotland nikirushwa
Bush House, London.

Hii ilikuwa mwaka wa 1991.

Ukweli wa mengi kuhusu hizi fitna na propaganda tunaujua na haya yote
ni chuki tu dhidi ya Uislam.

Sikuona haja ya kujibu hayo yako mengine.
 
Watu wa South Africa walipitia machungu mengi mikononi mwa Makaburu, ilipofika 1994, pande zote zikasema sasa basi, wakasahau yalopita, wakaganga ya mbele, sote twaabudu maendeleo yao! Tanzania tunahitaji zaidi utawala bora uliowekeza kwenye kuboresha maisha yetu sote. Historia ibakie historia!
 
Ww muongo eastafrica wazungu hawakufanya biashara ya utumwa

Muongo wewe.
Vasco dagama ndio waanzilishi wa slave trade east africa.
Portugese walikuja kutawala coast ya east africa...kuanzia lamu
Mombasa tanga Dar esalam
Zanzibar
Kilwa na wakateremka mpaka mozambique.
Waliwaua maelfu ya wenyeji walo resist ushenzi wao. ..waliuvunja kabisa mji mkuu wa kilwa ulokua mji wa elimu na ustaraabu..wakaua watu wake..
Pale mombasa pia waliua mamia ya waafrika.
Walipo fanikiwa kuzikalia wakaingia ndani mpaka congo na kuchukua slave kuwapeleka kwao lisbon na wengine kwenye trans antlantic route.
Na wazungu walikuja kununua slaves east afrika na route yao ilikua via cape town to europe or America au brazil .
Ni waarabu ndio walowafurusha wareno east africa...wakabakia msumbiji.
Nitakupa darsa murua kuhusu trade hii wewe na pasco mupate kujifunza .
Na kuacha kusoma uongo mlosomeshwa misionary school kuwa vasco dagama
Livungstone
Bethelow mew diaz ni wazumbuzi...
Ujinga mnao someshwa..walikuja kuvumbua nini ? Ibn batuta alishakuja miaka na miaka na kuandika habari za Afrika mpaka ndani kabisa Huko Zumbabwe.
Huyu alikua mwarabu...yeye ndie mvumbuzi ..hawa wengine ni wakoloni na slave traders
 
Acha uongo mwarabu hana dharau tusingekua tunaenda kufanya kazi kwao na pia dada zetu siku adi siku wanaenda wakifanya kazi za ndani
Hakuna MTU katili dunia hii kama Mwarabu...

Mwarabu akiiona ngozi nyeusi anaitemea mate!! Waarabu wamepasua matumbo ya mama zetu wajawazito ili tu waone kilichopo ndani!!

Waarabu wametoboa miguu ya babu zetu wakapitisha minyororo na kuwatesa sana!!

Waafrika wanaofanya kazi huko uarabuni wananyanyasika sana sana sana!! Wanachomwa na pasi visu na mateso mengine makali!!

Waarabu ni wanyama!!
 
Upelekwe na waarabu kutumikishwa nini ja
Eti Waarabu hawakuwatesa wazanzibar? kuna watu dini zinawapumbaza kweli, hivi ni nani aliyesoma history asiyejua unyama wa waarabu? watumwa walikuwa wanatolewa bara wanapakiwa kwenye majahazi wanaenda kutumikishwa, watumwa wa kiume walikuwa wanahasiwa ili wasizaliane
wazungu na wenyewe walikuwa wanyama hivyo hivyo
leo mtu unayokwa na povu ukiwatetea kisa dini yako?
hata sasa hivi mbona kuna madhila mengi watu weusi wanapitia huko Qatar sababu ya weusi wao?
huko ulaya pia wazungu wanawabagua waafrica nyie mnatokwa mapovu kuwatetea?
yaani hakuna ajabu kubwa kama hii
utumwa ulikuwepo dunia nzima kama huelewi,na hata watu weupe pia wapo waliopelekwa utumwani
 
Pasco,
Ukweli wa mengi kuhusu hizi fitna na propaganda tunaujua na haya yote
ni chuki tu dhidi ya Uislam.

Sikuona haja ya kujibu hayo yako mengine.
Mkuu Maalim, bandiko langu hili ni la zaidi ya michango 250 ila bandiko lako ndilo la kwanza kujibu na nadhani pia ndio la mwisho kwa upande wangu!.

Kumbe hizo picha ni fitna tuu na popaganda za chuki tuu dhidi ya Uislamu!.

Asante kutufahamisha, na asante kuchangia uzi wangu huu.

Pasco
 
Shukran Pasco kwa uzi wako.

Umeandika mengi lkn umeongozwa na allegation badala ya facts.

Kwanza tambua kuwa biashara ya utumwa ilikuwa na siko kubwa Ulaya na Amerika.

Baada ya wazungu hasa Christopher Columbus kuigundua Amerika kama new world,biashara ya utumwa ilishamiri Afrika hasa Afrika Magharibi.

Huwezi ukatenganisha biashara ya utumwa na Wazungu ambao waliwatumia waarabu kama middle men wao.

Kwa kiswahili cha sasa tunaweza kusema kuwa Wazungu walikuwa mataicoon na waarabu walikuwa pusher.

Kwa upande wa unyanyasaji na ubakaji inawezekana ikawa kweli walibaka.

Lakini hawakubaka kwakuwa wao ni waarabu,bali walibaka kama wabakaji waliopo Tanzania kwa sasa.

Mpaka leo bado kuna matukio mengi ya ubakaji ambayo yanaendelea Tanzania na yanafanywa na weusi wenzetu,ukitaka rejea kasome ripoti ya tume ya haki za binaadamu ya Mama Kejo Bisimba ya mwaka 2011 na kuendelea.

Kuhusu kuzaa na waswahili huenda waliwapenda waarabu,Mbona sasa hivi maeneo yenye ujenzi wa barabara ambapo wachina ndio wahusika watoto waliozaliwa na wachina ni wengi sana.

Yaani Dada zetu wanazaa wachina,Je wanabakwa na wachina au wanazaa kwa hiari?

Kuhusu mateso,hivi kuna maeneo walipo teseka zaidi ya Afrika ya kusini? hivi makaburu walikuwa waarabu?

Mbona mpaka sasa Wapalestina wanauawa kinyama(rejea kauli za Nyerere na Mandela) Wayahudi nao ni Waarabu? Kamuulize Dr Raitama Azavery atakuelezea vizuri kadhia ya mazayuni.

Juzi juzi zilitoka tuhuma kuwa Mashekhe wa Zanzibar aki na Farid Hadi na Aki Shekh Mselemu Ally kuwa wanaingiliwa kinyume na maumbile tena wakiwa ni wanaume wanaoheshimika,Je hao wafilaji ni wanaotuhumiwa kuwafila ni Waarabu?

Hivi umesahau waliomuua Mwangosi?

Ulimboka nae aliteswa na waarabu?

Hivi Mauaji ya Mwembe Chai ya 1998 nayo yalifanywa na Waarabu?

Hivi Waarabu ndio waliomuua Alfonce Mawazo?

Uhalifu ni uhalifu tu,hakuna ushenzi bora uwe umefanywa na Mwarabu au Mweusi.

Mauaji ya Kimbali ya Rwanda ,Afrika ya kati na Yanayoendelea Sudani kusini hayana mkono wa Mwarabu.

Mpangawangu, mbona unaleta mechanical comparison kati ya unyama kwa mwafrika kwa vile tu yeye ni mweusi na mambo mengine? Sikubaliana pia na unyama wowote ule uwe kwa mwafrika kwa mwafrika au kwa binadamu mwingine yeyote. Ebu tutoke huko kuutetea unyama huu usio na mfano kwa misingi ya kisiasa, kidini, kiitikadi, etc. Swala hapa ni huo udhalimu dhidi ya rangi nyeusi ambao haukujali siasa, idini, itikadi, na mangineyo. Ulikuwa ni unyama dhidi ya ngozi nyeusi kutokana kuamini kwao kuwa siye sio binadamu tosha na ni haki kutendewa kama wanyama. Sio Mohamed Said wala Pasco mwenyehaki ya kusema eti kati yao kulikuwa aliyekuwa afadhari katika kutufanyia unyama huu. Naona na wewe umeingia katika ujinga huo huo eti Wazungu walikuwa mataicoon na waarabu walikuwa pusher! Ni kizazi gani hiki cha Tanzania jamani?

Mimi nafikiri swala lingekuwa ni moja kuwa walikuwa wanyama kwetu kwa haya waliyowafanyia babu na bibi zetu! You are all looking for justification of this barbaric act through your political and religious affiliations na kutakasa ushenzi huu. Hatuwezi kutenganisha haya mambo! Kwa hiyo kwako hakuna tofauti ya unyama wakati wa utumwa na hayo unayotaja hapo juu? I wish ungepata hata dakika moja tu ya kushuhudia mateso na manyanyaso ya babu na bibi zetu.

Nimeona posting moja inasema historia ya utumwa imejaa uongo! Kweli? Swala la utumwa limegeuzwa uhalisia wake toka posting za huyo Mohamed Said na mwenzake Pasco na sisi bila akili tunaingia na kutafuta upande kwa misingi ya siasa, dini, itikadi, na mangineyo. Tumefikia hatua hata ya kukashfiana katika dini zetu ili kuonyesha kuwa hao washenzi wenye imani moja na sisi walikuwa sahihi! Mtume Mohamed (SAW) na Bwana Yesu walikuwa against na uonevu na udharilishaji wa aina yoyote ile.

Walikuwa ni sauti ya wanyonge, maskini, walioonekana kuwa ni najisi, na dhuruma yoyote. Mzungu na mwaarabu waliamini kuwa mtu mweusi ni najisi na mnyama asiyefaa kutendewa kama binadamu! Anayebisha anisahihishe kwa hili! Ujinga mkubwa ni kutojitambua na kuwa zobe kwa wengine! Mwaarabu na mzungu toka lini akamthamini mweusi kama sio ujinga na ushenzi wa kufikiri! Mauaji ya Kimbali ya Rwanda ,Afrika ya kati na Yanayoendelea Sudani kusini hayana mkono wa Mwarabu! Kwa hiyo mwafrika alikuwa na haki ya kuwa mtumwa kwa conclusion yako?

Ndugu zangu kwa heshima na taadhima ebu tutofautisha unyama waliofanyiwa babu na bibi zetu kwa sababu ya rangi zao na huo ushenzi mnaofananisha nao eti tu kwa sababu historia ya utumwa inagusa hisia zenu za kisiasa, kidini, na itikadi! Leo hii denial ya Holocaust ni kosa la kufungwa jela na ninakubaliana na hilo!

Leo sisi wenyewe waafrika wahanga wa utumwa tuanthubutu kujikejeli kwa kumtetea mzungu na mwaarabu kisa ni mislam au mkristo! Hivi unyama na udharilishaji wa mtu mweusi wakati wa utumwa una mfano wowote wa kuulinganisha? Naumia.
 
Back
Top Bottom