Ufafanuzi: Kwanini tuliona Lissu anafaa urais 2020 na sasa hafai Uenyekiti?

Lakini nadhani haya ni mafikirio tu, kwani ccm wanahitaji ruhusa ya Mbowe kuendelea kutawala? Tangu lini?

Hata Lisu akiwa Mwenyekiti, tutarudi humu humu JF kulalamika kivingine baada ya uchahuzi 2025.

Watasema Mbowe kamuhujumu Lisu, kwasababu chadema visingizio vimejaa, huwa vinasubiri muda tu vitolewe.

NChi hii hatufanyi uchaguzi, huwa tuna halalisha mtu aendelee kuwa madarakani kwa jina la demokrasoa za uchaguzi.

CCM sio wehu, wanafahamu hawashindi uchaguzi wowote, hivyo ili jamii za kimataifa waridhike, inabidi twende studio tuigize, na waone tumefanya uchaguzi. Na sterling (ccm) hauwawi.

Lisu ashinde, sawa lakini tupunguze promo, uchaguzi utaisha chadema iko hoi sana. Na haitakuwa chadema hii tuijuayo, utanambia muda huo ukifika.
 
Wajibu wangu ni kutoa shule ya siasa na utawala bure kabisa, Narudia kuwajibu nikisema,
Nani kakupa mamlaka haya?
Umehitimu wapi taaluma hizi?
Unapo kuwa tapeli wa kisiasa, hiyo nayo iwe ni sifa ya kujitangaza?
 
WAPIGA KURA HAPANA, MAJORITY OF THEM COULD BE OF "LOW IQ" particularly in this aspect, I say specifically in this aspect
Tunachokilalamikiaga kwa ccm, ndio ww unakitetea bila aibu hapa!
 
Tunachokilalamikiaga kwa ccm, ndio ww unakitetea bila aibu hapa!
Soma post ya Yeriko utajifunza kitu


Mwingine huyu hapa

Mimi kama Mimi, LISSU HAFAI KUWA MWENYEKITI, NI MROPOKAJI, UBABE, UJUAJI, NA HANA HEKIMA NA UVUMILIVU. Na akifanikiwa kuwa m/kiti Chadema ndio mwisho. Siomveni MABAYA lini siasa zake atagombana na wengi, wengi watahama/kupoteza morali.

Sauti kubwa huyu hapa


View: https://youtu.be/NU3b3IYQjhk?si=ZK_baFHAShSaIf9l
 
Kama Magufuli aliweza kuwa mwenyekiti wa ccm na uwezo mdogo vile wa kiutawala, Lisu anashindwaje?
Muulize Samia shughuli ya kujenga SGR, bandari keshagawa kakuta Magufuli (kanunua ship-to-shore cranes), kaongeza kina cha bahari, kaongeza ufanisi, umeme kukatika hadithi, wananchi wanapata huduma kwenye taasisi za serikali, ACCACIA (owners) wanenawa yaishe. To name a few things.

Magufuli level kubwa, huyo Lissu wako hatoshl kwa Mbowe tu.
 
Nisome kwakuwa anaendana na utashi wako?
 
Nasisitiza Magufuli hakuwa kiongozi mzuri, ni kweli alikuwa mtendaji mzuri kwenye miundombinu, ila hakuwa kiongozi mzuri. Sijui unaelewa ninachomaanisha? Mfano mrahisi, mchezaji nyota kwenye team si lazima awe team captain mzuri. Baki humo.
 
I can guarantee you, CHADEMA baada ya miaka mitano ijayo chini ya uongozi wa Mwenyekiti Mbowe; hutaitofautisha na hivyo vyama vingine unavyo vitolea mfano hapa.
Mbinu za uongozi wa kubembelezana na chama tawala wakati hali inapo ruhusu; halafu kuminywa wakati chama tawala kinapo pata kiongozi kichaa; na pasiwepo na njia mpya za kupambana na hali zote mbili; utategemea chama hicho kitakuwa na ufanisi gani?
Tegemeo la Mwenyekiti Mbowe lililo baki sasa ni kumshikilia Samia ili chama kipate nafasi kwenye serikali. Hakuna lingine zaidi ya hapo. Na wengi wenu mnao jitokeza hapa, kutetea uongozi wa Mbowe, mategemeo yenu ni hayo; kuingizwa kwenye ulaji, serikalini. hamna la ziada ya lengo hilo.
 
Nasisitiza Magufuli hakuwa kiongozi mzuri, ni kweli alikuwa mtendaji mzuri kwenye miundombinu, ila hakuwa kiongozi mzuri. Sijui unaelewa ninachomaanisha? Mfano mrahisi, mchezaji nyota kwenye team si lazima awe team captain mzuri. Baki humo.
Unaweza tofautisha uongozi na utendaji?

Kipimo cha uongozi ni utendaji.

Nyongeza nafasi ya raisi sio ya utendaji, ni decision making.

Ukiona vision zake zinaenda ina maana ana mechanism nzuri za strategic planning and supervision.

Unadhani mafanikio utokea tu kwa Kudra za mungu.

Hata hujui unachoandika, umesharudi kwenye akili zako hovyo za kila siku
 
lisu ni mwanaharakati, aishi humo tu na sio mwanasiasa
 
Kwanza hajajibu Maswali
 
Wewe Yericko na machawa wenzako msiwadanganye watu. Mna maslahi binafsi na kuendelea kuwepo kwa Mbowe ndani ya uongozi. Hamuutaki ukweli kuwa kwa sasa Chadema inahitaji ari mpya maana maslahi yenu yatakatizwa. Hakuna kingine cha zaidi.

Wewe hapa unapiga porojo ila ukweli unaujua. Mimi nikueleze tu kuwa kama mnataka Chadema iwe bai bai basi Mbowe aendelee kukalia tena kiti kwa kipindi hiki ambacho tayari mwenendo wake umedhihirisha wazi kuwa hana jipya tena la zaidi. Nakuhakikishia itakuwa bai bai na hayo maslahi yenu mtayapata kwa muda tu then mtaanza kugawana mifupa.

Wewe na wapuuzi wenzako mnataka kutuaminisha kuwa kwa miaka 20 sasa bado hamna imani na mtu mwingine zaidi ya Mbowe? Mbona sisi tunawaona wapo? Tena wenye ushawishi kwa vijana na makundi mengine? Chagueni moja, Kife au kipone. Mimi nilishaapa siwezi kuunga mkono mgombea anayepigiwa chapuo na maccm. This time Mbowe anapigiwa chapuo na maccm. Hicho ndiyo kifo cha dhahiri. Cha zaidi hata nyie mnaomuunga mkono Mbowe this time tukiwaangalieni ni watu machawa machawa tu wasio na jambo lingine la zaidi.

Yani mimi nije nimuunge mkono mgombea wa aina hiyo? Hapana. Nakuhakikishia kitakufa mkiendelea na huu ujinga anbao mmepewa muda wa zaidi ya mwezi mmoja kutafakari kwa kina.
 
Chadema ikiwa nyie ndio chamba kikuu Cha upinzani lakini pia milijipambanua kama chama Cha demokrasia ni wakati Sasa muidhihirishie Dunia wapi mnapractice hio demokrasia.Mbowe amehudumu miaka mingi inamtosha na apumzike.Haiwezekani eti Chadema nzima mwenye akili,uwezo na haki ya kukiongoza chama Cha Chadema awe mtu mmoja tuu....si kweli.Mchakato huu mkiufanya vibaya Kwa kumpigania huyo Mkurunziza wenu abakie tena madarakani hakika mtakuwa mmeimaliza kabisa Chadema mioyoni mwa Wananchi.Mruhusu ukomo wa madaraka,uhuru wa kugombea hizo nafasi za juu na mumpumzishe mh Mbowe abakie kuwa mshauri na mzee wa chama.
 
Ndugu umepatwa na Nini? Mbona unapwaya kiasi hiki? Kwenye andiko lako nimeelewa vitu viwili!

1. Kwamba mliruhusu Lissu agombee Urais hata kama hana sifa kwa kuwa mlijua atashindwa na baada ya siku 60 atarejea kuwa mtu wa kawaida. Kwanza haya ni matusi kwa chama Chako. Pili umeonesha hamjali maslahi ya nchi ukilinganisha maslahi ya SACCOS yenu!
2. Mbowe ataongoza milele!
Nadhani ONDOENI neno demokrasia kwenye jina la chama chenu kama mna mawazo ya kiimla kiasi hiki!
3. Wewe Yericko ni chawa unayefuata upepo tu hauna msimamo binafsi! Ulitupiga kamba hapa siku za mwisho za Dr. Slaa mpaka yeye mwenyewe akajitokeza kukusuta !
 
Kwahiyo mnamtaka mtu wa kucheka cheka na kuuma vidole pale atakapokutana na CCM? Mnamtaka mtu wa aina hiyo? Mbowe alidanganywa kuwa CCM itampa viti vya uwaziri walipokaa kwenye maridhiano na Samia. Bila hata kujua katiba ikoje akaingia mkenge. Huyo ndiyo mnataka kutuaminisha kuwa ana jipya la zaidi kuendelea kuongoza? Yani alidanganywa kama katoto kadogo na ndiyo chanzo kikubwa cha matatizo yanayoendelea ndani ya Chadema kwa sasa.

Sisi wengine tumeshasema hatumuungi mkono mgombea ambae CCM wanampigia chapuo. Mbowe aondoke wajitokeze watu wawanie hiyo nafasi apatikane mtu sahihi akiongoze chama kwenye nyakati mpya. Yani miaka 20 iliyopita kungekuwa na machawa kama leo Mbowe angeaminiwa kupewa chama akiongoze akiwa na miaka 40 tu? Hilo liyericko lipuuzi limeshavuka miaka 40 lakini na lenyewe bado halijiamini kuwa linaweza kuongoza Chadema kwenye ngazi yoyote zaidi limebakia kuwa lichawa la Mbowe. Kabla ya hizi porojo zake nilikuwa namuheshimu ila sasa nimemtambua ni mtu wa aina gani. Hovyo kabisa
 
Una minutes za hiko kikao cha Mbowe kuahidiwa uwaziri na CCM au humu JF unadhani kumejaa watoto wa kusikiliza baseless accusations.

Halafu Mbowe wala CDM hawana shida na Lissu kugombea nafasi ya uenyekiti, sikiliza watu wenye kauli za chama. Hizo ndio legit mouth piece zao, katibu mkuu wao John Mnyika kasema nafasi za kuchuana zipo wazi kwa nafasi ya mwenyekiti.

Huku mitandaoni hadithi tu, msitengeneze story kama vile Lissu kawekewa mizengwe toka atangaze kugombea. Mbowe na CDM wala hawana shida mnazotaka kutengeneza.

Kilichombeba Lissu kipindi cha Magufuli ni mafisadi ya CCM kwenye kumchafua, kulinda maslahi yao. Otherwise Lissu sio wa vile zaidi ya kuwa ropo-ropo tu.
 
Zikomo, mbona unatumia nguvu kubwa????
Uzuri wote tunajua.
 
Endeleeni kumsakama Lissu kwa kujifanya ana mapungufu na Mbowe na magenge yake hamna mapungufu.

Kuna dalili ya kuwasilisha orodha ya waliovuta mpunga kwa mama Abdul ili awaoneshe mlivyo dhaifu kuliko yeye.

Kikomo Cha unafiki umekaribia.

Kama kweli Mbowe ana Nia nzuri ya kukisaidia CDM bado anayo nafasi ya kukisaidia hata bila kuwa mkt Taifa, wenzie wameweza kwanini yeye asiweze? Akina zito wameweza, yeye je?

Ondoeni ubinafsi na uchawa wa kijinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…