Ufafanuzi wa CHADEMA Kuhusu Maazimio ya Kamati Kuu - Novemba 2013

Status
Not open for further replies.
Naona leo mashabiki w dkt slaa watashinda baa kula kitimoto na bia

Sema wazalendo makamanda wa ukweli na wapenzi wa CHADEMA leo ni sherehe kwa kuondoa kirusi. Leo natoa offer ya crate la Lagar na kilo tano za kitimoto.

LEO HADI RAHA vinyamkera vitimuliwe vinachafua anga!
 
HAKIKA KIKULACHO.......! PUUUUUUUUUUUUUU! THE TWO OF U :rip:
 
Mkwe wake mwisho wake 2015 kwisa habari yake...sasa hivi kila mtu yuko busy anahangaika kujiokoa kwenye jahazi lizamalo. Mbona analoo

Nachoshangaa ni kwamba kwanini misukule ya Lumumba haishangilii na kumkaribisha Zitto ccm badala yake wanasikitika sana na kumshauri apiganie haki yake Chadema...!!! kazi kweli kweli...
 
Mkwe wake mwisho wake 2015 kwisa habari yake...sasa hivi kila mtu yuko busy anahangaika kujiokoa kwenye jahazi lizamalo. Mbona analoo

Huu ndo mwisho wake katika medani za kisiasa za bongo, bahati yake kamejikusanyie fedha nyingi kifisadi otherwise.... Mdogo wangu Kitila atulie aimarishe kitivo cha elimu DUCE.
 
Mkuu nakubaliana na theory yako, lakini hapo kwenye bold sikubaliani wewe kabisa. Mfano, tunaambiwa Kinana anaua tembo kukiimarisha chama kwa ajili ya uchaguzi wa 2015 na pia anabebesha punda unga kwa ajili ya uchaguzi ujao pia, je huo ujenzi wa chama una tija kwa Taifa letu?
Siasa ni chama, chama kinajengwa kisha chama chenye serikali kinajenga nchi kwa kuwezesha utawala bora, uchumi mzuri, afya bora, ajira, elimu, miundo mbinu bora na mengine mengi. Kwa hiyo, kujenga chama ni sehemu ya kujenga nchi.
 
Taarifa zilizopo sasa huku MTWARA wananchi wamefurahi sana maamuzi yaliyofanyika CHADEMA,hivi sasa wanafanya maulid kubwa sana hapa na naziona kadi nyingi sana za CHADEMA zikiteketea kwenye moto mkubwa sana.
Kumbe maulidi....
 
Ndo maana maccm yalikuwa yanajigamba CDM lazima ife kumbe yalikuwa yamekamata vichwa 4 vyakuvitumia.
 
CDM ni chama sio mtu, maamuzi sahihi kabisa, kila mtu alikuwa anawashaanga CDM kukaa na Zito....

Sijaandika CHADEMA ni mtu.

Sijaandika kwamba maamuzi si sahihi.

Rudia kusoma nilichoandika maana inaelekea hujakielewa.
 
Hivi hii intelijensia ya chadema ambayo imeshindwa kumgundua huyo wa nne imewezaje kuwa gundua wakina kitila,zitto na mwigamba?


Tundulisu anasema wameigiza sijui wameunda kamati ya kuchunguza na kugundua huyo wa nne. Ina maana hawakufanya uchunguzi toka mwanzo hila wameamua kukurupuka na kuwa husisha wakina kitila,zitto na mwigamba?

Ni wakina nani walio wabaini wao watatu na wakashindwa huyo mmoja?

NI WAZI HUU WARAKA UMETUNGWA NA HAKUNA UCHUNGUZI ULIOFANYIKA NDIO MAANA WAMESHINDWA KUMBAINI MHUSIKA WA NNE.

CC
sixgates, Ritz, Mamndenyi, Pasco, CHAMVIGA.

HIVI

Ni wazi zitto, mwigamba,kitila walipangiwa toka muda.
Hii dhambi ita watesa chadema.
 
Last edited by a moderator:
Nachoshangaa ni kwamba kwanini misukule ya Lumumba haishangilii na kumkaribisha Zitto ccm badala yake wanasikitika sana na kumshauri apiganie haki yake Chadema...!!! kazi kweli kweli...

Huzijui tabia za WACHAWI mkuu..!??
 

only FOOLS can listen to your barbaric songs!
 

Sit back and relax bro. Iache itutese..
 
Lumumba wanampigania Zitto abaki Chadema! ajabu kweli! :A S 39::A S 39::A S 39::A S 39:
 

Na kwa nini maamuzi mazito kama haya yafanyike bila uchunguzi kukamilika?

Maana kama kuna mtu wa nne hajajulikana, uchunguzi haujakamilika.

Tutajuaje kama wamekuwa fair kama hata hawawezi kuwajua wote waliohusika?

Tutajuaje kwamba uchunguzi haujachafuliwa na huyo wa nne?

Tutajuaje kwamba hawamkingii kifua huyo wa nne?

Kama CHADEMA inashindwa kufanya uchunguzi wa ndani ya chama kwa ufanisi itaweza kuendesha nchi?
 
Chadema hongereni kwa kufanya maamuzi magumu,heshima kwenu wote viongozi wangu,nafurahi kusikia kuwa watuhumiwa wamekiri kuhusika na huo mpango kiasi cha kufikia hatua ya kuomba msamaha.

Na waliomba msamaha kwa mujibu wa kipengele kipi cha katiba??
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…