Siasa za Afrika bado ziko katika "early stage". Watu wake wengi hawajui ni sababu zipi zinawafanya wawe wanasiasa, wanadhani labda uwezo wao wa kufikiri unatosha kuwa ni "ticket" ya wao kuwa wanasiasa. Lakini pia siasa zao zinaonesha mtazamo wa waliowengi ambao huwa wafuasi wao. Namna mtu alivyoishi, mazingira aliyoishi, elimu na shughuli mbalimbali azifanyazo zinaweza kumjenga kuamini anaweza kufanya kile anachodhani. Lakini kuna athari kubwa sana ya "mindset", unaweza kukuza akili yako kwa kiwango kikubwa, lakini mindset ikiwa ndogo mambo yako mengi yatakuwa madogo, yenye kuudhi na kurudisha watu katika mzunguko wa uwezo wako. Lakini tuangalie pia nini chanzo cha kuwa na mindset tofauti tofauti. Ni mazingira, imani, elimu, ukubwa wa changamoto zinazokuzunga, na mahitaji ya jamii, vinavyokusukuma kufanya unachofiri. Je Zitto anafanya haya kwa manufaa gani na ya nani labda! Tutafakari