hapa nilipo natafuta penye mkaa niichome moto hii kadi ya Chadema.
Nimechoka Upuuzi wa haya majamaa.
Malengo ya Lema div 5 hayawezi kutimia huu ni mwanzo wa mchezo tu na karata ndo zinalambwa ila mwisho wa siku lazima Zitto amalize akiwa mshindi.Ukweli utakuwa wazi tu na hata wafanyeje Zitto amewazidi akili sana tu na kwenye changamoto hii atapita kama alivyop[ita zote zilizomtangulia
zitto aondoke bhaana , watu tukale posho na kupumzika Dubai ! hawajui chadema ni ya kaskazini .....? zile hesab jamaa alikuwa anaitaji kwenye kamati Fulani spidi itapungua sasa........
Well, kama ule waraka ulioko kwenye uzi namba 566 una ukweli, basi yafuatayo ndio yaliyomo:-
1) Utangulizi
Wanamtandao walitoa tafsiri na maana ili kurahisha mawasiliano kati yao. Pia walijikita ktk kutumia neno "taasisi" badala ya neno "chama". Hivyo hata wanachama waliitwa wanataasisi! Lakini kubwa zaidi ni mwelekeo wa kutaka "nafasi ya juu ktk taasisi" i.e. uenyekiti.
2) Hoja za wanamtandao ni 11 hivi. Kisha wakafanya SWOT analysis na baadaye wakaweka mkakati na hitimisho.
3) Performance kwenye chaguzi ndogo. Wameonesha kuwa "taasisi" haikufanya vizuri na walitoa mifano ya kati ya 2010-2012. Kwa makusudi hawakuweka matokeo ya Juni 2013! Pia hawakuguzia changamoto/matatizo yaliyopelekea matokeo kuwa yalivyokuwa bali walijikita kwenye "ubaya".
4) Matumizi ya fedha za taasisi. Hili linajulikana na kila mwana JF kwani matumizi ya maneno, mtiririko wa hoja, mantiki nk vinalandana sana na tuhuma zilizoletwa na akina Shonza, Tuntemeke et al na hivi karibuni na Bw. Samson Mwigamba. hata
4) Taarifa za fedha: hili nalo kama namba 3 linajulikana kwani lilishaletwa na kujadiliwa mara nying hapa jamvini na kwenye media za ndani.
5) Uchaguzi wa ndani (hasa nafasi ya m/kiti): Hili nalo kwa hisani ya "Mkulima Maskini" aka Mwigamba mlikwishalipata.
6) Udhaifu wa Mh. Freeman Mbowe: Hapa kuna tuhuma nzito za yeye kuingilia shughuli za kiutendaji za taasisi na hata kudhaniwa kuwa anafaidika binafsi na mfumo huo.
7) Matumizi mabaya ya madaraka yanayoweza kuhusishwa na ufisadi: Hapa ni mwendelezo wa kipengele No. 6 wenye muktadha wa "uchaguzi na hasa nafasi ya m/kiti" Hapa zimetolewa shutuma nyingi za jinsi manunuzi ya vitu/vifaa, taratibu za manunuzi ya ndani nk zilivyo kiukwa. Aidha kama ilivyo ada F. A. Mbowe ndiye MM (Mtuhumiwa Mkuu); Zitto yeye ni MM (Mhusika Mkuu) sorry for confusing abbrevs!
8) Nani wamuunge mkono (kama mtandao wao wanamtaka nani): Wakatengeneza sifa za mtu wao vs Mbowe.
Eneo hili lilijaa kashfa, dharau, kejeli na propaganda ambazo humu jamvini akina Shonza, Tuntemeke & Mtella wataona fahari kuhusishwa nazo.
9) SWOT analysis: Hapa walijikita ktk kumnadi na kumpamba MM. Uchambuzi ulihitimishwa kwa MM kupata "A-pass marks" na hivyo kuweka mazingira ya MM kuelekea "king".
10) Mtandao wa ushindi: hapa wakaweka mikakati ya namna ya kumpeleka MM "king". Kifupi waliweka structure/miundo mbinu kufanikisha malengo yao. Jambo kubwa linalojitokeza ni namna watakavyotumia chaguzi za taasisi ktk ngazi zote kuweka watu wao. Hili lingeendelea toka ngazi za misingi mpaka kanda na baadaye MM angeingia kingi.
11) Mwenendo wa MM kuanzia sasa, walikusudia yafuatayo
a) MM apunguze ukaribu na viongozi wa CCM na awe mkosoaji wa utendaji wa serikali bungeni na nje ya bunge.
b) Ashiriki kikamilifu shughuli za CHADEMA (?), zikiwemo vikao VYOTE vinavyomhusu, opereshini mbali mbali, chaguzi ndogo nk
c) Aendelee kushusha "nondo" bungeni
d) Ajitahidi kupunguza jazba. Ashauriane na "wazee" (?) kabla/namna ya kujibu tuhuma mbalimbali
e) Kuwawezesha M2 na M3 kifedha, ili kuongeza ufanisi wao ktk majukumu waliyopangiana.
Kwa ufupi (summary) hayo ndio yaliyomo kwenye waraka husika (iwapo utathibitishwa).
Wadau karibuni kuboresha summary kwa kukosoa na/au kuongezea
Vipi kuhusu pesa alizokopa sl kamati kuu imesemanaje?
Malengo ya Lema div 5 hayawezi kutimia huu ni mwanzo wa mchezo tu na karata ndo zinalambwa ila mwisho wa siku lazima Zitto amalize akiwa mshindi.Ukweli utakuwa wazi tu na hata wafanyeje Zitto amewazidi akili sana tu na kwenye changamoto hii atapita kama alivyop[ita zote zilizomtangulia
Semeni ukweli, Kilichowaponza Kitila na Zitto ni;
1. Elimu zao. Kitila na Zito ni kati ya wasomi wachache ndani ya chadema wanaojitambua. Waliokataa kuburuzwa na vihio- Mbowe na Slaa.
2. Makabila na kanda zao. Zitto na Kitila hawatoki na ile kanda ya wamiliki wa chama, na pia hawatoki ktk lile kabila la wamiliki wa chama.
3.
Kama kuna a missing piece of the puzzle uchunguzi haujakamilika.
Kwa mfano, in theory, huyo mtu wa nne anaweza kuwa mtu yeyote, including wanaoongoza uchunguzi, na hivyo kuufanya uchunguzi batili.
Kama hujui hata mhalifu ni nani nyumbani kwako unawezaje kuwa na confidence kuhusu integrity ya nyumba?
Tutajuaje kwamba huyo wa nne hatakuwa masalia atakayeendeleza vita kutoka ndani na kuwapa kina Zitto habari kutoka ndani?
Live Updates: Ndugu Wanachama na Watanzania na wote muda si mrefu tutawaletea Mkutano na Waandishi wa Habari kuwajulisha Watanzania maazimio na maamuzi ya Kamati Kuu iliyokutana kwa siku mbili tarehe 20-21/11/2013 katika Hotel ya Blue Pearl Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam
================
UPDATES
- M/Kiti Mh. Freeman Mbowe ameshawasili na ameanza kwa kusema kuwa Kamati Kuu imemteua Mh. Tundu Lissu kuwa Mwanasheria Mkuu wa Chama na pia Kamati Kuu imefikia maamuzi ya kinidhamu kwa baadhi ya viongozi.
Anamkaribisha Mh. Tundu Lissu kwa ajili ya kutoa taarifa ya maazimio ya Kamati Kuu kwa niaba ya M/Kiti
- Tundu Lissu anaanza kwa kusema kuwa Kamati Kuu imenasa waraka wa mkakati wa siri wa kukipasua Chama vipande vipande unaohusisha watu wanne ambao ni Zitto Kabwe, Dr. Kitila Mkumbo, Samson Mwigamba na mtu mwingine ambaye hajajulikana.
- Anasema lugha iliyotumika katika waraka huo ni ya siri ambapo kuna mtu anaitwa MM ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe, M1 ni Dr. Kitila Mkumbo, M2. Hajajulikana na Dr. Mkumbo alikana kumfahamu kabisa M2, na M3 ni Mwigamba.
Lissu anasema Waraka huo uliojulikana kama Waraka wa Ushindi unavunja katiba ya Chama kwa sababu umepandikiza chuki za kidini, majungu na kukashifu viongozi wa Chama kinyume na katiba ya CHADEMA.
Lissu anasema tuhuma zote zilizoko katika waraka huo hazijawahi kuwasilishwa kwenye kikao chochote halali cha chama kinyume na matakwa na masharti ya katiba yetu
- Anasema Kamati Kuu imeamua kuwavua nyadhifa zao zote watu wote waliotajwa katika waraka huo ambao ni Zitto Kabwe, Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba.
Pia kamati kuu imeunda kamati ya kuchunguza na kufuatilia mhusika mwingine M2 ambaye anadaiwa ni Mtumishi wa Makao Makuu ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yake
Kamati Kuu imeagiza wahusika wote waandikiwe barua za kujieleza ni kwanini wasivuliwe uanachama kwa makosa hayo makubwa waliyofanya.
- Pia Kamati Kuu imeagiza mchakato wa kumvua Zitto nafasi yake ya Unaibu wa Kambi ya Upinzani Bungeni.
- Lissu anasema Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe na Dr. Kitila Mkumbo waliomba kujiuzulu nyadhifa zao zote baada ya waraka wao kukamatwa lakini Kamati Kuu iliwakatilia baada ya kuona kuwa kukubaliana na maombi yao hayo ilikuwa ni kama kuwaacha wajiuzulu kwa heshima ambayo hawaistahili hata kidogo.
- Kamati Kuu pia imeazimia kuusambaza waraka huo kwenye vyombo mbalimbali vya habari ili watanzania waone na kujua ukweli.
Lissu anamalizia kwa kuwaomba watanzania na Wanachama wote wa CHADEMA nchi nzima wasife moyo na waendelee kukijenga Chama na nchi yao.
- Kamati Kuu pia imemteua Wakili Msomi Mh. Peter Kibatara kuwa Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa Chama
- Mh. Mbowe anasema waraka wa siri za Zitto haukutengenezwa wala haukutoka Makao Makuu. Alikuwa akijibu swali la Mayage kuhusu zitakapopatikana fedha za kutekeleza mpango huo